Jamaa anamuoa mchumba wa rafiki yake kama mke wa pili

Nitumie namba ya huyo dogo inbox nimshauri direct maana asije akaaga dunia please mkuu Kama ishu iko serious
Ingekua vema USHAUR Hapa Hapa tu mkuu[emoji120]

USHAUR wako Unaweza wasaidia hata wengine pia[emoji120]
 
Ashukru Mungu kwa yaliyotokea,Wala Haina haja ya kulazimisha amtangulize Mungu mbele ,afanye maisha yake mengine Kuna kitu kikubwa sn Mungu kamiepusha nacho
Kweli mkuu,
Huwez jua mungu kaepusha nini
 
Kiumbe mwanamke kumuelewa ni ngumu sana na ukiona unaanza kumuelewa mwanamke ujue siku zako za kuishi zimeisha hapa duniani
 
Na yalianza muda mrefu. Haiwezekani ndani ya kipindi kifupi waoane.
Ukitaka kuishi kwa amani na mwanamke usimuone wivu, mpe mahitaji yake ila usimuoneshe km unamhitaji sana.
Usemalo Lina ukweli kabisa, Hawa hawakuanza hivi karibun..

Huenda kulkua namahusiano ya Siri yanaendlea hapa katkat
 
Mpuuzi mpuuzi TU,
sijajua uko kwenye uke wenza kafuata nini.

Na sijui Ni Nani alimshaur kua uke wenza atafurahia maisha
Yaani hapo kwenye uke wenza sijamuelewa kabisa huyo dada, kumuacha kaka wa watu kwenda kuolewa mke wa pili mmh. Si kwa wivu huu nilionao mke wa pili ni big no bora kubaki single tu. Ila siku atalia machozi ya damu , malipo soon tu
 
Mambo mazito haya.Mapenzi!

Ngoja kwanza niangalie The expendables,nitarudi
 
Mimi hata sioni kama huyo binti anampenda huyo jamaa kiukweli naona alikuwa anapenda tu pesa zake.
Hivi mtu aliyekufanyia hayo yote na unajua kinachoendelea kwenye familia yako unashindwaje kumwambia yanayojiri ili mkae mjue mnafanyaje ili kumpa nafasi ya kurekebisha pale alipopwaya angalau kumpa muda akishindwa ndio uchukue maamuzi mengine ila tayari ulimshirikisha ashindwe tu mwenyew kutetea penzi kama kweli alikuwa serious ila hata huko mbele kusiwe na wakulaumiwa.
Huyo bidada alikuwa na mahusiaono ya siri muda mrefu tu ila kwa huyo mchumba alikuwa anazuga mana huduma anapata.
Huwezi nambia process zote kuanzia barua,mahari mpaka ndoa inakaribia anashindwa kumweleza mpenzi wake kama kweli anampenda.
Mwambie huyo dogo akimbie tena asigeuke nyuma hapo hakuna mwanamke mana unaanzaje kumchukua huku unajua kabisa amekusaliti.
Atafute mwanamke kwingine wapendane huyo mchumba tayari ni mke wa mtu aachane nae atamsumbua tu yeye na familia yake.
Kuna familia zinatia aibu sana mana misaada na hela za watu wamekula sana ila wakaona binti yao aolewe na kwingine wao kama wazazi walishindwa nini kumuita huyo kijana kumuuliza ana mpango gani mana inaonekana wanamjua fika.
Aachane nao kwanza kuna familia ukioa unaenda kubebe matatizo na stress mfano mzuri ni hiyo.
Sorry nimeandika kwa hasira kama vile namjua huyo dogo.
 
Kwenye miti hapana wajenzi

Halafu bado binti anajitetea eti hamuelewi jamaa!

Ndomana watu wengine wanaamua kuroga

Jamaa achukulie changamoto hii in positive way japo inauma sana na itamchukua muda kua sawa lakini ajitahidi kumove on

Amshukuru Mungu hata kwahilo maana kila kitu kitokeacho hua kuna sababu nyuma yake. Hivo hajui Mungu kamuepushia nini ama kamuandalia nini kizuri mbele

Mi naamini wakati mwingine mpaka uje umpate yule perfect match huna budi kupitia changamoto hizi za kuumizwa ili utakapompata yule sahihi ujue namna ya kumthamini

Wakati huu ninyi kama marafiki zake wa karibu ndo muda wa kua nae bega kwa bega katika kumtia moyo mwenzenu ikibidi kumpeleka kwa mwanasaikolojia ama kwenye nyumba za ibada
 
Unaweza kukuta anaridhishwa kwenye ile sekta nyeti Mana kuna watu wazima sio haba wanajua anatakiwa afanye nini plus maexperience kibao kampagawisha bidada.
Labda dogo alikuwa anagusa gusa tu akaona anazingua.
 
Haupo sahihi! Acheni aolewe na huyo jamaa aliyetoa helaa. Hilo mnalotaka kufanya sio njia sahihi, na si dawa ya hilo tatizo.
 
Uncle ni mkubwa kwangu sana tu....hatuna malengo makubwa zaidi ya kupeana raha
 
Nakaziaaaaaaa

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Sema pamoja na kumpa pole jamaa etu,lkn na yeye alizidi mbwembwe nadhan hadi bint akawa na waswas nae,yaan umpangie dem nyumba nzima alaf usiishi nae kweli???

Unaeza kukuta hata huyo broo hajamchezea dem ila n swaga tuu,kumbuka demu anafanya kazi sheli means anakutana na jamaa mara kibao,

Muhimu n kumuelekeza dogo uhalisia baada ya hilo asonge mbele kama ambulance

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kuna haja ya kuangalia yumba(familia) unayo enda kuposa au kuanzisha mahusiano nayo.

Angalau iwe na hofu ya Mungu ata kido au iwe familia ye heshima kidogo, utaepuka mambo mengi.

Jamaa anaoneka ni mtu mstaarabu kwa mujibu wa maelezo yako. Hivyo basi Mungu amemuepusha na hiyo familia ya kikora. Kwamaana imeandikwa "Bwana atakupa msaidizi wa kufanana wewe" kwaiyo huyo muhuni mwacheni aolewe na muhuni mwenzake.

Jamaa awe na subira miaka 39 bado hajachelewa sana wala hajawai. Amuombe Mungu ampe anayemfaa, mstaarabu kama yeye.

Tokea juzi uzi ulipo anza nilijua kabisa uyo dada anadanganya kuwa kalazimishwa na asingetokea hiyo jioni. Lakini shukuruni hakutokea kwa sababu kuna uwezekano mkubwa kama angepata mualiko huo wa kuonana na nyie, siku tatu kabla au mbili, angewapangia tukio la ajabu kama siyo criminal basis la udhalilishaji.

Hampendi uyo dogo na inawezekana hajawai kumpenda. Kama angekuwa anampenda angemwambia tokea yeye mwenyewe kwa mdomo wake, kuwa rafiki anamtongoza, haiingii akilini adi anafikia hatua ya kuposwa. Huyo dogo ana habari. Alafu anadai kalazimishwa na nyie bado mna muamini na kutaka kuonana naye.

Sheria zipo kulingana na Sheria za ndoa "Marriage Act" dogo anaweza kudai malizake na gharama alizo tumia kipindi cha uchumba wao, ikiwa ni pamoja na zawadi na gharama nyingine kama vielelezo vipo. Ila kwa upande wa kiroho tunashauri aachane navyo na asemehe yaani asibebe manung'uniko moyoni "akomboe nafsi yake" hii njia ya kiroho ndiyo nzuri zaidi. Maana unaweza kutumia sheria ukarudishiwa mali zako lakini ukabaki unateseka moyoni miaka yote.

Mwisho kabisa Nina swali. Yule binti aliye zaa nae utotoni hadi wakaacha shule,hakufaa kuwa mke wake?. Mtoto aliye zaliwa anamtunza kama inavyo stahili?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…