Jamaa anamuoa mchumba wa rafiki yake kama mke wa pili

Jamaa anamuoa mchumba wa rafiki yake kama mke wa pili

Kuna maisha nje na baada ya, mapenzi, asonge mbele na lazima maisha yaendelee.

Ila huyo nae Dogo 4yrs uchumba tyuuh why hakumuoa kabisa? Huenda binti alichoka kusubiri lol.

Nwei poleeeh yake.
 
Update....
Ni kwamba mwanamke alinyang'anywa simu ya awali alokua anatumia na kapewa simu mpya yenye line mpya ya Airtel.

Nmefanikiwa kuipata hio namba na nmempigia na kuongea mwanamke mwenyewe.

Anasema,
"Shem mi sio kwamba simpendi rafiki ako, nampenda sana na nilitamani awe mme wangu. Sema rafiki ako hakua serious na Mimi. Miaka 4 yote tangu ameleta barua hamna kinachoendelea. Familia inanisumbua Sana afu nikimwambia hataki kunielewa anadai mpaka amalizie nyumba yake. Nyumba imeisha anadai finishing bado. Hivi kweli shemej nyumbA inaweza mzuia mtu wasifunge Ndoa? Hivi kweli anachonifanyia mwenzako unaona Ni sahii."

Nikamjibu,
"Kwaiyo meji ukaona Njia rahisi Ni kuolewa TU na rafki yake, hujui itamuumiza Kias gani?"

Akasema,
"Shemej nikwambie TU ukweli, uyu B tangu mwanzoni ashaonesha ananipenda Sana. Afu tangu zaman keshaonesha Nia ya kunioa MDA mrefu. Sema Mimi TU ndo nilikua kikwazo, afu kingine uyu B anakubalika Sana uku nyumban.

Shemej presha kwa familia yangu kuhusu B Ni kubwa Sana, Baba na mama na dada zangu wote wanataka niolewe na B. Imefkia mpaka mama ananambia uyu alonichumbia Ni mhuni TU miaka 4 Ni uchumba sugu huo. Imefkia mpaka baba haniongeleshi kisa sitak kuolewa na B. Na wote washanambia nisipoolewa B Mimi sitokua mwanao Tena na watanifuta kwenye ukoo.

Shemej yang mi mwenywe Niko Njia panda apa, moyoni mwangu B hayupo kabisa ila nalazimishwa TU na familia yangu. Uto rafiki yako hawamtaki kabisa ata kumskia uku nyumbani."

Nikamwambia,
"Kwaiyo shemej uko serious kabisa umelazimishwa Hii ndoa?"

Akasema
"Ndio Shem, yaan naomba TU uniombee msamaha TU kwa rafk yako. Mi bado nampenda Sana."

Nikamwambia,
"Bas Shem naomba ufanye jion tuonane ata kwa jamaa tujue tunaliwekaje hili"

Akasema,
"Sawa, ila Mimi kwa jamaa siwez kuja tena.italeta balaa. Labda yeye ata aje kwako niwakute apo kwako"

Nikasema,
"Sawa"

Ninachowaza Sasa,
Kama ni kweli uyu mwanamke kalazimishwa. Na kweli ANAMPENDA jamaa.

Nawaza kumshauri rafiki yangu, ashirikiane na uyu mwanamke.
Kisha binti atoroshwe akawekwe mafichoni kwa sikU kadhaa Hadi ile harusi ilopangwa itakapopita.

Uyu B atakapomtafuta akakosa Basi Iyo Ndoa ya kulazimisha itakua imeota manyoya.

Afu Sasa uyo B aje kwetu kulalamika kwetu katoroshewa MKE, na sisi tuje tumuoneshe kua upumbavu hatutaki.

SIJUI KAMA NIKO SAHII AU LAH[emoji848]

ushauri wenu tafadhali
Duuuuuh usisahau mrejesho.
 
Ushauri wangu:
1
)Kuwa makini na mkeo na huyo B inawezekana kaishamtafuna
2)Mnunulie mkeo na huyo shemeji yako zile dildo ulizoziona Kariakoo
3)Mnunulie dogo zile chupi zenye uchi kwa wachina
4)Fanya Biashara,pata faida,nenda kwa mkeo na umpende sana la sivyo atat[]mbwa na B

Nakutakia biashara njema !
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa anachojua tangu awali ni kwamba yeye Ndo anatambulika atakuja kumuoa binti yao.

Sidhan kama aliwai kua na ugomvi wowote na wakwe zake maana mwezi wa sita alkua akigharamia matibabu ya mama ake binti pale Ocean road.
Inashangaza sana[emoji848]

Kingine pia
Yupo na dada ake binti Ni mtu wangu wa karibu Sana, na tuna heshimiana sana.

Na juzi nmeonana nae ofsin kwangu.

sema nmeshangaa sana kwanini na yeye kanificha hili suala na inasemekana sikU jamaa anatoa mahali uyo dada mtu alikuepo na ndo alkua mpishi mkuu kwenye shughuli nzima[emoji848].
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mwanamke kafanya uamuzi sahihi 100% Hakuna uchumba wa miaka 4 ni ubabaishaji. Halafu kama yeye amepanga alishindwa nini kuoa wakaendelea kuishi hapo wakimalizia nyumba? Haimaanishi huyo dada kapata mume Bora anaweza achwa baadae ila sio issue angalau alichagua mtu anayetaka kumuoa.
Kabisaaa yaan.
 
Kosa analo huyo mnayemuita dogo.
Kwann kaleta malaya kwenye urafiki wenu ulioshibana?

Malaya katambulisha mtu nyumbani halafu anasema analazimishwa kuolewa naye[emoji23].

Ilikuaje mpaka akampeleka kwao?

Sikia, HUYO MALAYA ATAWAUA.
AMESHAUA URAFIKI WENU, SASA BADO ROHO ZENU.

NA NINAVYOKUONA NA AKILI ZAKO MGANDO ZA KUMTOROSHA KAMA HAMTOUANA BASI MTAPAKANA MAFUTA WE SUBIRI TU.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Lakini huyo mwanamke mwenzetu hakutumia akili kwasababu mleta mada kasema bibie amesomeshwa , akatafutiwa kazi, akapangiwa nyumba nzima plus gari la kutembelea,.. hakuna mwanaume ambae Hana malengo na ww anaweza kukufanyia hayo yote ilikuwa ni uvumilivu ndo ulihitajika Kwa huyo mdada ..
Km aliweza kuganya yote haya, alishindwa vipi kumuoa? Kuna kitu hakipo sawaa hapa.
 
Huku mbele sasa nahisi kuna chai.

Mafuta ya 350,000 kwa gari gani?

Semi tella?

Na kama ana gharamia hivyo, kwanini familia ya binti haimtaki na inamtaka huyo mwingine? Tena si wa dini yao? Na walianzaje kumtaka? Aliwatambulisha?
Yaan maswali mengi ni fikirishi mno, nashindwa hata kuwazua.
 
Kwani michepuko hawafanyiwagi hayo?

Lakini naona harufu ya chumvi kidogo.

Umpangishie nyumba, umnunulie na gari, halafu usioe kisa unasubiri nyumba iishe....thubutuuu

Na hakuna binti wa hivyo akubali kuolewa mke wa pili, kisa ndoa tu?
Nina mashaka.
Yaan hata mie nashangaa hapa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Yap Kama chai hivi unajiuliza kwann ndani ya miaka hiyo minne asipate hata mtoto??

Hata hiyo reaction ya wazazi wake ya kutokumkubali kabisa jamaa na kumruhusu mtoto abadili na dini juu [emoji1][emoji1787]

Halafu hao wazazi hawakumuonya jamaa kuhusu kukaa mda mrefu bila kumuoa mtt wao ?? Kwamba walimpa jamaa kimya kimya ?

Hii kweli yaweza kua ni chai na karoti [emoji1787][emoji1787]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Dah! Jamaa huwez Amin alkua anamgharamia Yule mwanamke utadhan mke wake wa Ndoa.

Jamaa yangu Ni form four, ila alipambana kumlipia Ada mpaka binti uyu kamaliza chuo kikuu.

Kibaya Zaid ata hapo sheli anakofanya kazi uyu binti, jamaa ndo kamuunganisha na ndo mdhamini wake.

Binti kapangiwa nyumba nzima, anaishi kwa Raha Sana.

Jamaa alkua analipa kila kitu khs mahitaj yake yote ya nyumbani mpaka dharula za familia yake.

Gari anayotembelea kamnunulia uyu jamaa,
(Tena nilishiriki ipasavyo kwenye mchakato mzima wa kuiagiza mpak kuitia mkononi)

mafuta juzi juzi TU tunatoka gym alipitia she'll kumuwekea ya 350,000 kwa ajili ya mizunguko yake.nikishuhudia mwenyewe.

Mshahara anaolipwa sidhan hata Kama uwa anaugusa kabisa.

Kwakweli,
alichomfanyia jamaa Ni zaidi ya unyama[emoji26]

Hiyo gari au lori ?! Gari gabi inaingia mafuta ya laki 2 na nusu mie tu inaingia 180000 full na ni gari kubwaaa
 
Update.....

Tulipanga leo saa Moja kamili tukutane nyumban kwangu na uyo binti pamoja na dogo. Tukampigia Ila akawa hapatikani.

Baadae Kwenye saa 1 na nusu,
Kaja kupatikana akasema anakuja sawa tumsubiri anakuja.

Sahivi tunampigia simu haipatikani.

Tumebadili mpaka namba, tunapiga ila bado hapatikani.

Tumejaribu kupigia shoga Ake wa karibu, mama P akamcheki kwake.

MDA si mrefu kasema kafika kwake hayupo,

Kasema anaelekea kwao kuona Kama atampata.

BADO TUNAMSUBIRI[emoji17]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] duuuh hii ngoma nzito.
 
Kabisa mkuu[emoji848]
Jamaa alimtunza binti utadhani malkia.

Kuna MDA tulkua mpk tunamlaumu kwa matumizi ya ovyo ya pesa na kumdekeza.

Maana nyumba alompangia alimuwekea housegal wakati hata kazi za maana pale hamna na nyumba nzima anakaa yeye na mdogo wake anaerisiti form six
Eeeeeh mbna unatuchanganya sasa, yaan had wadogo zake wanaishi ktk nyumba anayolipa kod dogo, afu wazazi hawamtaki? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] duuuh hii kali. Sasa
 
Kingine Cha kujiuliza,...
Mama Ake binti mwaka huu kalazwa pale Ocean road mwezi na nusu-jamaa kagharamia

Katolewa pale,
Kahamishiwa Agha khani, wiki 3 jamaaa katoboka bill zote.

Ila bado mama uyu baada ya kupona kabisa kashindwa kuthamini mchango wa dogo hata mwaka haujaisha anafanyia hivi[emoji26]

Duniani watu wema hulipwa vibaya, uyu dogo kalipwa vibaya Sana.[emoji26]

Naandika hivi Hadi machozi yananilenga.
Duuuuh mbna hii ngoma n nzito kuicheza.
 
Mkuu, nikikwambia jamaa alkua ANAMPENDA Sana uyu mwanamke unapaswa kuniamini.

Uyu jamaa alijitoa kwa Hali na Mali khs uyu mwanamke.

Jamaa tangu amekua na uyu mwanamke amekua karibu na kila kitu Cha jamaa,

Mkuu,
Kuna watu wanapenda sijawahi ona.

Mwakani alkua amepanga pia kuibadilisha nyumba ya wazazi wake binti akidai kila akienda anakosa hata pa kufikia
(Ni mipango TU ilokuepo khs uyu MKE wake mtarajiwa)

Nyumba nnayokwambia alkua anajenga, ikifika mwakani itakua inamaliza mwaka wa 3 inajengwa non-stop.
Mafundi wako saiti daily na material hayakatiki saiti.

Ukiambiwa nyumba,
uelewe Ni nyumba kwelikweli na sio hivi vibanda vyetu tunavyojenga kina sisi pangu pakavu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wakwe walikua wanajua hayo mambo?
 
Ukimpenda mwanamke toa mahari na kufunga ndoa muda ukiwa tayari

Lakini mwanamke unaetembea nae miaka yote kama hawara tu akipata wa kumuoa anaangalia maslahi yake

Huyo wa kukusubiri na miaka 4 sidhani kama ana nia ya kuolewa na wewe bali ni girlfriend tu

Hongera zake huyo jamaa kwa kutoa mahari
Ukipata mwanamke wa kuoa ni kuoa tu sio unaishi nae kama kimada halafu akuolewa unalialia
Huyo ni wa wote mpaka uoe period
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] maneno makali haya jaman, ila ndo ukweli.
 
Sijawahi kuandika nyuzi za ovyo mkuu,
Nnapokwambia alkua mchumba wake miaka minne namaanisha minne kweli.

Dogo tayar alkua na mtoto nje, alimzaa akisoma shule na ndo sababu ya dogo kuishia form 4 maana alikimbia miaka 30 jela ndo akaingia uko Kwenye kubangaiza.

Uyu mchumba wake amempata akiwa chuo mwaka wa 1.
Miaka 2 yote ya uchumba wao binti alkua anasoma chuo mkoa mwingine kabisa.

Mwaka 1 wote binti aliajiliwa Kama mtendaji wa tarafa mkoani uko vijijini,

Jamaa ndo kamtoa uko na kamuunganisha na kazi ya sheli kwa rafiki yake mmoja hapa mjini

Mwaka 1 tu ndo wamekua wote hapa mjini, yaani namaanisha mwaka huu 2021 unaoishia. (Yaani tangu mwezi octoba mwaka Jana mpaka leo Hii)

Na jamaa alompangia maksudi na hakutaka kuishi na kwake kwa maana jamaa yeye bado anaishi kwao (nyumba ya familia)

Ndo alipanga akishamaliza ujenzi wakahamie Kwenye nyumba yake anojenga sahvi.
Mmmmmmh hapa pagumu sasa, kwani alishindwa kupanga? Yaan unazidi kutuchanganya wachangiaji wenyewe. Lol
 
Back
Top Bottom