Jamaa yangu alilewa madaraka mwisho wake ukawa aibu

Jamaa yangu alilewa madaraka mwisho wake ukawa aibu

DeMostAdmired

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2017
Posts
1,579
Reaction score
3,798
Hii code ni nyepesi sana kuna baadhi ya watu wataing'amua.

Nilipokuwa advance form 5 jamaa yangu/ rafiki yangu alinishirikisha kitu kwamba anahitaji kugombea kuwa head prefect wa pale skul.

Mimi sikumpinga, huyu mwamba tulikuwa ni watu wa utani sana na kuzinguana sana ila mwisho wa yote tukiwa tunadiscuss mambo ya msingi huwa tunaweka tofauti zetu pembeni na kufikia muafaka.

Mimi honestly nilikuwa mzuri kwenye ngeli japo advance hatukuwa tunasoma combination za arts means hiyo ngeli nilitoka nayo o level.

Jamaa yangu akaniomba tushirikiane tuchore barua nzuri ya kuomba kugombea uongozi. Bila hiyana tukakaa tukaiandika vizuri kwa kingereza, mwamba kasubmit.

Sasa pale skuli kulikuwa na utararibu kwamba uchaguzi ni kwa hp, gs(mshindi wa pili nafas ya hp), academic na discipline ila nafasi zingine zote ni hp ndo anateua kwahyo kulikuwa na teuzi za hp.

Sasa mimi nikastuka mapema nikamuita jamaa tukakaa chini nikamuuliza kuhusu return yangu ni nini endapo tukipambana akapata kuwa hp yani nitafaidika nini.

Jamaa akanambia anafahamu hilo na hataniacha bila nafasi yoyote. Kwasababu jamaa namfahamu ni mtu wa siasa sana na ni kigeu geu sana nilimbana aniahidi atanipa nafasi gani.

Jamaa akaniahidi kwamba hataniacha bila uteuzi chakufanya tupambane tu.

SIASA NI MCHEZO MCHAFU WAZEE.

Ukifuatilia threads zangu za nyuma utagundua kuwa mimi skuli nilikuwa dancer mzuri sana.

Jamaa alichokifanya alinifata mimi na wenzangu kwenye kikundi cha dance, akawafata washkaji wangu wengine walikuwa kwenye kuimba na wengine walikuwa kwenye kucheza mpira.

Skuli ina o level na advance na jamaa ni alikuwa mtu wa jamii hiyohiyo ya huko na o level alisomea skuli jirani na ile skul tulokuwa tunasomea.

Yani o level alisomea skul ya serikali inayopatikana karibu na skul aliyochaguliwa kusoma advance.

Kwahiyo jamaa aliona kabisa kwamba kura nyingi atazipata kutokea o level na siyo advance kwasababu yule mpinzani wake alikuwa anakubalika sana na washkaji wa advance ila o level hakuwa na political bases na power kubwa kumshinda mshkaji wangu.

Jamaa akatukusanya washkaji ambao tulikuwa na influence na mashabiki wengi kutoka upande wa o level kutokana na vipaji tulivokuwa navyo. Kifupi jamaa alijua kuitumia rasilimali watu aliyokuwa nayo na tuliyokuwa nayo sisi washkaji zake.

Wale ma footballer wa advance walikuwa na washkaji wao o level ma footballer wenzao akiwemo huyu jamaa mchezaji wa zamani wa Yanga na Sasa yupo JKT (ni fullback namba tatu left footer watu wa boli washamjua) jina lake kapuni japo huyu yeye hakuwa anajihusisha sana na kampeni za huyu mwamba wetu(mgombea)

Kwahiyo tulikuwa tunazunguka madarasani hasa o level tunacheza mziki, wakuimba wanaimba na wa kuchezea mpira kwa danadana na control za kiufundi walifanya yao lengo kuuteka umma ili tupate kura siku ya uchaguzi.

Siku ya uchaguzi ikafika.

Tutaendelea...
 
Hii code ni nyepesi sana kuna baadhi ya watu wataing'amua.

Nilipokuwa advance form 5 jamaa yangu/ rafiki yangu alinishirikisha kitu kwamba anahitaji kugombea kuwa head prefect wa pale skul.

Mimi sikumpinga, huyu mwamba tulikuwa ni watu wa utani sana na kuzinguana sana ila mwisho wa yote tukiwa tunadiscuss mambo ya msingi huwa tunaweka tofauti zetu pembeni na kufikia muafaka.

Mimi honestly nilikuwa mzuri kwenye ngeli japo advance hatukuwa tunasoma combination za arts means hiyo ngeli nilitoka nayo o level.

Jamaa yangu akaniomba tushirikiane tuchore barua nzuri ya kuomba kugombea uongozi. Bila hiyana tukakata tukaiandika vzur kwa kingereza ikakaa noao mwamba kasubmit.

Sasa pale skuli kulikuwa na utararibu kwamba uchaguzi ni kwa hp, gs(mshindi wa pili nafas ya hp), academic na discipline ila nafas zingine zote ni hp ndo anateua kwahyo kulikuwa na teuzi za hp.

Sasa mimi nikastuka mapema nikamuita jamaa tukakaa chini nikamuuliza kuhusu return yangu ni nini endapo tukipambana akapata kuwa hp yani nitafaidika nini.

Jamaa akanambia anafahamu hilo na hataniacha bila nafasi yoyote. Kwasababu jamaa namfahamu ni mtu wa siasa sana na ni kigeu geu sana nilimbana aniahidi atanipa nafas gani.
Jamaa akaniahidi kwamba hataniacha bila uteuzi chakufanya tupambane tu.

SIASA NI MCHEZO MCHAFU WAZEE.

Ukifuatilia threads zangu za nyuma utagundua kuwa mimi skul nilikuwa dancer mzuri sana.
Jamaa alichokifanya alinifata mimi na wenzangu kwenye kikundi cha dance, akawafata washkaji wangu wengine walikuwa kwenye kuimba na wengine walikuwa kwenye kucheza mpira.

Skuli ina o level na advance na jamaa ni alikuwa mtu wa jamii hiyohiyo ya huko na o level alisomea skuli jirani na ile skul tulokuwa tunasomea.
Yani o level alisomea skul ya gvment inayopatikana karibu na skul aliyochaguliwa kusoma advance.

Kwahiyo jamaa aliona kabisa kwamba kura nyingi atazipata kutokea o level na siyo advance kwasababu yule mpinzani wake alikuwa anakubalika sana na washkaji wa advance ila o level hakuwa na political bases na power kubwa kumshinda mshkaji wangu.

Jamaa akatukusanya washkaji ambao tulikuwa na influence na mashabiki wengi kutoka upande wa o level kutokana na vipaji tulivokuwa navyo. Kifupi jamaa alijua kuitumia rasilimali watu aliyokuwa nayo na tuliyokuwa nayo sisi washkaji zake.

Wale ma footballer wa advance walikuwa na washkaji wao o level ma footballer wenzao akiwemo huyu jamaa mchezaji wa zamani wa Yanga na Sasa yupo JKT (ni fullback namna tatu left footer watu wa boli washamjua) jina lake kapuni japo huyu yeye hakuwa anajihusisha sana na kampeni za huyu mwamba wetu(mgombea)

Kwahyo tulikuwa tunazunguka madarasani hasa o level tunacheza mziki, wakuimba wanaimba na wa kuchezea mpira kwa danadana na control za kiufundi walifanya yao lengo kuuteka umma ili tupate kura siku ya uchaguzi.

Siku ya uchaguzi ikafika.........

Tutaendelea..........
Huu upuuzi ndo wa kutusubirisha kweli?? Eti itaendelea.... Andika yote ndo ulete
 
Junior ananisumbua hapa na wewe unataka pia kunisumbua.
 
MUENDELEZO.......

Siku mbili kabla ya siku ya uchaguzi jamaa alituita watu wake tulikuwa mchanganyiko o level na advance tulikutana darasani kupanga mipango ya jinsi gani tutashinda.

Of course jamaa hakuwa na presha kubwa kivile kwasababu kwa dalili zilivokuwa zinaonyesha ni kwamba jamaa kulikuwa na probability kubwa ya yeye kushinda kwasababu alikuwa anakubalika sana o level na o level walikuwa nu wengi kuliko advance.

Tulipanga mipango ya jinsi ya kuzilinda kura zake na alochagua wasimamizi wa uchaguzi yani watu watakaoratibu uchaguzi na kuhakikisha kura zake haziibiwi wala hakuna kura zitakazokuongezea za yule mpinzani.

Kesho yake ndo kampeni zilikuwa zinafungwa na siku hiyo usiku tulipata taarifa kwamba kuna watu wanawazungukia watoto wa form one na two kuwapa pencil na pen moja moja na kuwasisitizia wasome kwa bidii wt hizo ni zawadi kutoka kwa mgombea 😆😆 eti mgombea yule (mpinzani wa mshikaji wangu) alikuwa anajinadi kwamba yupo tayari kuwasapot watoto wa o level nao wafike advance na anaanza kiwasapot kwa kuwapa pencil na pen (rushwa hii 😄😄)

Jamaa yangu alipozipata hizi taarifa akili iliwaka ila tulokuwa naye karibu tukaanza kumcomfort kumpa moyo na kumpamba kichawa chawa mwamba akaanza line.

Siku ya uchaguzi ilipofika uchaguzi ulifanyika na kumalizika salama na jamaa akashinda kwa kishindo.
Mpinzani wake mkubwa yeye akawa mshindi wa pili na akawa GS.
Skul kwetu kulikuwa na utararibu wa kuwaaposhaa viongozi wakubwa na kulikuwa na barge begani.

HP barge sita, kushoto tatu kulia tatu, GS, academic na discipline barge 4 kulia mbili na kushoto mbili then viongozi walobakia mbili huku moja na kule moja. Na viongozi wa juu walikuwa wanapiga tai nyekundu.

Siku hiyo jamaa anakabidhiwa MADARAKA ilikuwa ni furaha sana hasa kwa upande wetu kwasababu tulikuwa tunasherehekea ushindi na nguvu zetu na mipango yetu ilionekana kuzaa matunda.

HP alikuwa na jukumu la kuteuwa viongozi wateuliwa katika nafasi mbalimbali kama mazingira, michezo, afya, ulinzi, library na laboratory.

Haya sasa uteuzi ukafuata.........
 
Back
Top Bottom