kyagata
JF-Expert Member
- Oct 18, 2016
- 10,406
- 19,892
Sio kwamba nimesimuliwa hapana.
Huyu jamaa yangu alihitimu bcom in accounting kutoka pale udbs miaka kadhaa iliyopita.
Basi majuzi kati tuko nae ghetto tunapiga mvinyo tukaona tangazo kutoka kwenye kampuni kubwa mafuta lenye makao makuu yake huko Uingereza wakihitaji mhasibu kigezo ni uwe na degree ya uhasibu na uzoefu wa miaka minne wa kufanya kazi za kihasibu.
Mshikaji chap akaingia kwenye portal ya hiyo kampuni husika akajaza taarifa zake kisha akaapply ile kazi. Basi bana baada ya siku chache akapokea email kutoka kwa wahusika ikimpa maelekezo ya lini interview itafanyika na wapi.
Siku ya interview kaenda zake na Mungu wake tu, kafika pale anasema akakuta wadau wengine kama 10 hivi na katika kudadis akagundua baadhi yao walikua na cpa akati yeye hata cpa hana.
Basi interview ikaenda vyema tu na akawa anajua hawezi kupata ile kazi sababu ya cv za baadhi ya washindani wake kuwa nzuri kuliko yake pia wenzie walikua na matokeo mazuri ya shule.
Ila Mungu huyu ni wa ajabu jamaa jana akiwa zake kwa mhindi wake anachapa kazi akapokea simu akijulishwa kuwa kafaulu ule usahili na tayari amepokea offer letter ambayo nimebahatika kuiona. Salary yao sio haba kabisa ni salary inayokuweza kuishi vizuri tu kwa maisha yetu ya kitanzania.
Nilichojifunza kutoka kwa huyu msela wangu ni kuwa na ujasiri na kumtanguliza Mungu. Kuna watu kumbe wana matokeo mazuri ya shule ila interview zinawatoa knock-out na kuna watu wenye matokeo mabovu kama huyu jamaa angu ila ni wajanja wa kujibu vyema maswali ya usaili.