Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kwema Wakuu!
Nimeamini Mjini mipango. Haka kajamaa bhana kama ungebahatika kukutana nako Mwezi wa Saba mwishoni ungeelewa Kwa nini Wazazi na ndugu Zake walikakatia TAMAA.
Ungeelewa Kwa nini hata Mchumba wake alimbwaga.
Kajamaa kalikuwa kamejichokea haswa.
Moja haisomi Mbili haikai.
Sasa mwanzoni mwa Mwezi wa nane kaliposikia tangazola Ajira za sekta ya Afya na waalimu kakaja nyumbani.
Nakumbuka jinsi kalivyokuwa kamechangamka Sana tofauti na Siku zingine àmbapo kalikuwa kanakuja kanatia huruma kakiwa hakajala. Yàani nikikaona mida ya Mchana najua kamekuja kugongea urimbo Lunch kwangu.
Nikakaambia kulikoni, kakaniambia kamepata mchongo wa Pesa ya Kumtoa kimasomaso.
Nikabaki nakaangalia,
Kakaniambia nikakope kama Laki Mbili hivi. Mmmh! Nikagoma, nilijua hakana uwezo wa kunilipa Kwanza hakan Kazi hizô Laki Mbili katanilipaje.
Kakaniambia Kwa kunihakikishia, nikikapa Laki Mbili katarudisha Laki na hamsini ndàni ya wiki Mbili. Mmh!
Nikakuuliza, Pesa kanataka za nini?
Ñdipo kakaniambia kanaenda kuanzisha huduma ya Usangoma.
Nilicheka Sana! Unajua nimemaliza nako chuo Miaka kadhaa Iliyopita, semà mambo yake kidôgo hayajamwendea vizuri tangu amalize hajawahi kupata Dili hata la Laki Mbili na nusu Kwa Mwezi.
Kutoka degree Mpaka kuwa Mganga WA kienyeji WA mchongo siô pouawa.
Kakaniambia, hiyo Laki Mbili kanaenda kununua mahitaji ya Usangoma.
Kakaanza kuyataja kakiwa kametoa karatasi iliyokwisha andikwa mahitaji Kwa Hati yake akawa ananisomea;
Usinga, Buku Mbili pale vingunguti.
Upembe Buku Mbili vingunguti.
Upembe mdogo WA mbuzi buku pale vingunguti.
Kibuyu na shanga elfu tano.
Mafuta ya mnyonyo elfu 15.
Kaniki nyekundu elfu 20
Kaniki nyeusi elfu 25
Udi na uvumba elfu 50, huu atanunua kwèñye Duka Kule posta kûna udi maalumu wa shughuli hizô.
Chungu elfu 15
Kinyago cha mzimu wa kolelo elfu 40
Gamba la konokono, hili alikuja nalo kwèñye mfumo.
Kuwatisha Stori nikaona isiwe Kesi maana ameniomba Sana. Wewe Mpaka Mtu amenipigia Magoti kisa Laki Mbili unusu. Nikampa.
Nikamuuliza Kwa hîyo shughuli zako utapiga Wapi. Akaniambia anaenda kutafuta pori Huko mabwepande.
Akaprinti matangazo ya Mganga mtaalamu wa kulegeza vifungo na kung'arisha Ñyota.
Kweli baàda ya Siku kadhaa nikaanza kuona matangazo yake kwèñye Nguzo za umeme maeneo mbalimbali jijini Dsm.
Hakuweka Namba Yake ya Simu alisajili Namba ñyiñgine kimagendo yàani kupitia mawakala wasajili laini àmbao wananjaa kama yeye.
Kisha akajiunga na Magrupu ya waombaji Kazi za Afya ya WhatsApp na Telegram.
Akadizaini vizuri tangazo lake Kisha akatuma Huko.
Maadmin walimmaindi kichizi . Kûna Wengine walim-remove kûna Wengine walimpuuza lakini kumbe siô wôte waliompuuza.
Kajamaa kanambia kanashangaa Simu Yake inaanza kuita. Kheee! Kumbe kweli inafanya Kazi. Unaambiwa kalifurahi kweli.
Kakasafisha koo vizuri Kisha kakaanza kuongea sauti ya kisangoma, "Habari yako Marii! Mizimu imekuona Marii"
Sasa Mimi nikawa nacheka anavyonisimulia maana jinsi alivyokuwa anaongea ungedhani ni kweli. Nikamuuliza Sasa Marii inamaana gàni. Akanijibu ati yeye mwenyewe hajui ila alijikuta amejitamkia ndîo ikawa neno lake Kuu.
Duuh!
Akaanza kunionyesha pîcha jinsi alivyovaa maleba(mavazi ya Sanaa yake ya usangamo).
Nikamwona akiwa kavaa kaniki nyeusi kama kanga, lady kapitisha lubega la kimasai Kwa kaniki nyekundu.
Kichwani akiwa kavaa manyoya ya kanga na jogoo mweup, alafu jicho Moja kajipakq alama ya Ñyota rangi nyeupe.
Nusu ya kifua chake kikiwa wazi.
Miguuni hakuwa amevaa vikuu vya shanga na kata mbuga. Sijui hata katambuga zile alizipata Wapi😀😀 maana Mimi hapa Mjini ninamiaka Kumi sijaona katambuga.
Jamaa anakuambia Eneo lake la Kazi liko Huko mapori ya mabwepande,
Anasema yeye mwenyewe haamini kama kweli au anaota.
Jamaa kanunua Bajaji mpyaaa ya Milioni nane. Dadeki.
Alafu mkononi anaLaki tisa.
Anakuambia Kazi yake ataifunga hizi karibuni baàda ya kumalizana na waalimu.
Sasa nikamuuliza alikuwa anawapa masharti gàni. Hapo ndîo nikachoka.
Wengine alikuwa anapiga chale Mpaka za matakoni, Wengine anawapa hirizi wanazifunga kwèñye Mikono au viunoni.
Wengine anawaogesha Kwa Madawa ya kuchanganyachanganya.
Kûna mmoja alimwekea upupu kidôgo ati alivyokuwa anawashwa akawa anasema Wachawi ndîo wamemwekea gundu, hivyo Mwili unavyowasha ndîo gundu linatoka.
Taikon nikawa nashangaa hizi Akili za ràfiki yàngu kazitolea Wapi. Unajua hakuwa hivi. Kumbe kweli usimdharau Mtu ukamwona kaishiwa step, Hana ujanja Maisha yamemmaliza, kumbe haijaisha Mpaka iishe
Jamaa anakuambia kama mambo yatakaa vizuri anampango wa kuagiza gari Aina ya IST.
Daah!
Pesa yàngu Laki Mbili unusu akanirejeshea laki tatu.
Haya bhana!
Mimi Acha nipumzike tuu
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam