Jamal Musiala Vs Jude Bellingham unaenda na nani?

Jamal Musiala Vs Jude Bellingham unaenda na nani?

Wote ni bora kutegemea na mchezo wenyewe mwingine anasema lampard mwengine xavi
Walikuwa ni viungo wawili tofauti wanacheza namba tofauti lampard sana sana ungemkuta namba 8 xavi yeye sana sana 6
6 ilikua namba ya jezi tu, ila Xavi alikua anacheza 8 akilindwa na Busquets nyuma yake.

Hata mashabiki lialia wa Chelsea hawawezi kukwambia Lampard alikua bora overall kuliko Xavi, ingawa alikua ana magoli mengi kuliko Xavi.
 
Jude amepunguziwa majukumu anatumika kuongeza creativity kwenye attacking
Nakukumbusha Jude akiwa Madrid match kumi na goli kumi kafikisha na ni kiungo .

Kingine nadhani Jamal ni mkubwa kuliko Jude hiyo sio sababu sanaa
Wachezajj waliomzunguka Jamal Bayern utafananisha na wale wa hovyo pale bvb? Lakini dogo bado akashine.
 
6 ilikua namba ya jezi tu, ila Xavi alikua anacheza 8 akilindwa na Busquets nyuma yake.

Hata mashabiki lialia wa Chelsea hawawezi kukwambia Lampard alikua bora overall kuliko Xavi, ingawa alikua ana magoli mengi kuliko Xavi.
Kiukweli xavi alikuwa ni holding midfielder a kind of kiungo nusu mkabaji nusu mchezeshaji.

Same to lampard
 
Jude Bellingham.

Ni mchezaji Mzuri mno mchezaji wa Daraja la Juu sana.

Anaweza akacheza Kila Aina ya mchezo.

1. Akiamua kukaba anakaba. (Tough game atakupa)

2.akiamua KUKIMBIA anakimbia.

3. Akiamua UFUNDI ni hatari.

4. Akiamua Kuishambulia Atashambulia..

5. Akiamua kufunga atafunga pia.

6 Pia akiamua kuchezesha timu Kwa Kila temple ataichezesha,
Passing za Kila namna Fupi na ndefu.

Kiungo Bora kabisa ana Technicalities za Hali ya Juu Mno.

Changamoto
Sema waingereza hawana guarantee.............
Umenikumbusha Theo Walcot,Jack Wilshare,Childwick,Wayne Rooney nk.
 
Wote ni bora kutegemea na mchezo wenyewe mwingine anasema lampard mwengine xavi
Walikuwa ni viungo wawili tofauti wanacheza namba tofauti lampard sana sana ungemkuta namba 8 xavi yeye sana sana 6
Xavi alikua Central midfielder ukiongelea mambo ya namba 6 ni vitu viwili tofauti na Central midfielder.. lampard alikua attacking midfielder na sio namba 8 kama unavosema
 
Kiukweli xavi alikuwa ni holding midfielder a kind of kiungo nusu mkabaji nusu mchezeshaji.

Same to lampard
Uongo mtupu na huwenda haufaham mpira ila umejiandikia tu.

Xavi hajawai kuwa holding midfielder ila alikua ni Central midfielder.

Naweza kukupa sifa za baadhi ya viungo ili ujue kutofautisha maana haufahamu.

Holding midfielder-- muda mwingine unaweza muita deep lying midfielder huyu ni kiungo ambaye hafanyi sana movement nying uwanjani,kazi kubwa ni kuzuia na anakaa karibu na mabeki na kuchezesha team akiwa chini. Kiungo huyu ni tofaut na kiungo mkabaj huyu anaweza asiwe na mwili nguvu nyingi mfano joginho ila tu awe na uwezo wa kupiga past fupi na ndefu.. mfano halisi wa holding midfielder bongo ni aucho.

Mpaka hapo jiulize xavi alikua na sifa hizo au alikua anacheza hivo mpka usemeni holding midfielder!!

Cntral midfielder-- huyu ni kiungo wa kati mara nyingi huwa anapatikana kati kati na majukum yake uwanjan ni kuichezesha team kupitia yeye, anaweza kusaidia kukaba au kishambulia lkn majukum yake mama uwanjan ni kuochezesha team. Mfano halisi wa Central midfielder ni xavi.. Barcelona ilimgeuza xavi kama ukuta kila mtu akiwa na mpira angongesha kwa xavi na kutembea na yeye xavi ndo alikua anaamua team ichezeje. Viungo wengine ni kama tonight kroos au rakitic baada ya xavi kuondoka akachua majukum hayo.

Kabla haujasema huyu ni holding midfielder kwanza jifunze ujue sifa za holding na majukum yake.
 
Mkuu ujue kunakuwaga na Central midfielder ambaye huwa anccheza nane au sits lakini majukumu tofauti

Ndiyo huyo central midfielder kwani holding midfielder unaelewa vipi?
Ndio huyo sasa
Holding na Central midfielder ni vitu viwili tofauti na majukum tofauti kabsa uwanjan
 
Xavi alikua Central midfielder ukiongelea mambo ya namba 6 ni vitu viwili tofauti na Central midfielder.. lampard alikua attacking midfielder na sio namba 8 kama unavosema
Mkuu naona umekuja juu sana soma sawia hujaelewa

Lampard namba 6 nani kasema?
 
Xavi alikua Central midfielder ukiongelea mambo ya namba 6 ni vitu viwili tofauti na Central midfielder.. lampard alikua attacking midfielder na sio namba 8 kama unavosema
Hivi bado huwa mnaongelea kuhusu mpira kwa kutaja sijui namba sita mara namba nane? Muelezee mchezaji kwa role yake uwanjani na sio namba.

Hivi hawa ma wing backs kwenye mfumo wa 3-5-2 kwamfano utawaita namba 3 na 2 au 11 na 7? Tuongelee role ya mchezaji uwanjani na sio sijui namba ngapi au ngapi.
 
Back
Top Bottom