Jamani hivi huyu baba ana upendo namimi?

Pole sana mpendwa kwa hayo yaliyokukuta,
Mzazi siku zote ni mzazi na ananafasi yake so hata akikutendea ubaya haifai kumpotezea la msingi mpe heshima yake kama inanvyositahili na msaidie pindi atakapotaka msaada kama una uwezo wa kumsaidia, hata kama hakupendi ipo siku atakuja kuona umuhimu wako

Kama hukutelekezwa na baba yako göod for you, kwakifupi hujaielewa mada yangu

Nashukuru kwa mchango

Thanks dark city

Pole sana Loly.....I completely understand your feelings....will be back

sijasema nataka kumfanyia ubaya ila nimeuliza mzazi wa aina hii ni kweli ana upendo kwangu? au thamani yangu inakuwepo wakati anashida zake tuu?

Sijui wewe ni wa jinsia ya "ke" au "me". Lakini jambo hili linataka mazungumzo baina yako na baba yako. wenzetu wanaita "father to son/daughter talk". Mweleze unavyofikiria na yeye atakueleza anavyofikiri kisha mtafikia muafaka au mtakubali kutofautiana. Hii itakusaidia kutoa vitu vilivyojaa kifuani na utagundua kuwa mambo mengine yalikuwa ni hisia zako tu wala hayana ukweli ndani yake. Ukifanya kosa la kumpotezea kama wengine wanavyokushauri haya mambo yaliyojaa kifuani mwako hayataisha au kupotea yenyewe yataendelea kukutafuna tu na kamwe hautakuwa huru. Kunatakiwa kuwepo na ukweli na maridhiano "Truth and reconciliation" baina yako wewe na baba yako ili muweze kuanza upya.

hapo jibu unalo, wewe ni mtu mzima unayejitegemea, hebu hilo libaba tupa kule concentrate na maisha yako... mlee mama yako, baba yako unachoweza kufanya ni kumheshimu tu... na hulazimishwi kushikamana naye.. in this life unamthamini anayekuthamini asiyekuthamini tupa kule.... afterall heri kumjali mtu baki mbaye anakuthamini na kukusaidia=kukupenda kuliko ndg/mzazi asiyekupenda na kukuthamini. maisha ni yako na si ya mzazi wako, naamini mama yako amekulea kuwa strong nk, move on, ila siku mdingi akikuuliza kwa nini umechange mueleze ukweli

kwa sasahivi hana time na mimi yaani akinitafuta ni shida yake lakini sio vinginevyo na haoni haya na wala hakuna mtoto wake yeyote anaenidokezea kuwa siku hizi dingi mambo safi tukikutana wananichora tuu wanajikausha mbaya sijuhi tatizo ni nini nanilikua nawaona ni ndugu wenye upondo kwangu hata kunidokezea ??

0

Badili tabia thanx so much mchango wako ni mzuri naufanyia kazi

Pole sana Loly, unatakiwa kujua kwamba kuna watu wana tabia hii kwamba, akiona una hela anafikiri kwamba huhitaji tena msaada wa fedha japokuwa umesema mwanzo ulikuwa unamsaidia, sasa kapata yeye anajua wewe una uwezo kana kwamba huhitaji tena msaada wowote wa fedha.

Pia inawezekana kabisa sio kwamba hakupendi au hakujali ila anaona wewe kwa vile ndio ulikuwa unamsaidia una hela za kujitosheleza

Ushauri wangu kwako, muombe hela kiasi chochote uone kama atakupa au atasemaje, huenda atakupa bila kipingamizi chochote, akionesha negative responce ndio unaweza kufikiri hayo uliyosema kuwa ni kweli

Mimi kabla sijachangia ningependa kujua juu ya status ya maelewano baina yako na ndugu zako(hao wanaotaka kuanzishiwa biashara) ikoje?

unatakiwa ushukuru kwa kila kitu na hasa kwa kuwa na mzazi .... chochote unachokifanya kwa mzazi hutakiwi kukihesabu wala kutegemea malipo kulingana na uyatendayo kwake .. unatakiwa uelewe kwanza nini jukumu lako kwa mzazi wako na nini unatakiwa kukifanya bila kujali yuko katika hali gani .. pili ondoa dhana ya kujiona mnyonge au kuona wengine wana nafasi kubwa zaidi kuliko wewe .
kama una nafasi ya kufanya maendeleo yako wewe fanya na kama una ziada kwa ajili ya mzazi na nduguzo wasaidie pasi kutegemea kulipwa chochote

1. Ulitakiwa kumsaidia kwa roho moja............madhara ya kutoa msaada kwa shingo upande ndio hayo! Tenda wema uende zako usingoje shukrani.
2. Kimtazamo inaonekana baba bado anakuona uko fit kifedha hivyo anaelekeza msaada kwa wale wasiojiweza. La kama unahisi mambo yako hayajakaa sawa, muombe msaada husika. Ng'ombe anaelia ndio hupewa majani

baba ni baba tu na atabaki kua baba.hayo mengine ni mapungufu yake binafsi lakini hayafuti cheo chake cha ubaba kwako. kwanza msamehe tu na umuone ni mtu mwenye mapungufu asiyejua nini anafanya lakini bado ni baba yako!ukishamsamehe endelea kumuheshimu na endapo utakwama au utahitaji msaada wake mfuate tu umwambie face to fece kua nahitaji hiki na hiki then msikilize atasemaje.kwa ninavyoona anakuona tayari unamafanikio makubwa kimaisha so huitaji msaada ndio maana akakuletea hata ishu ya kumsaidia ndugu yako kupata sehemu ya kufanyia biashara.kakuona umeshakomaa kimaisha ndio maana amekushirikisha ktk hilo.so usifanye mambo kwa assumptions!!!mfate umwambie unashida then uone atasemaje!

maisha yangu ni yakubangaiza siko fit wala nini? Watoto wake wanaofanya kazi pia amewapa misaada kasoro mimi? Yaani yeye anajua mimi sijui kama kapiga bingo
anaminya kiaina

maisha yangu ni yakubangaiza siko fit wala nini? Watoto wake wanaofanya kazi pia amewapa misaada kasoro mimi? Yaani yeye anajua mimi sijui kama kapiga bingoanaminya kiaina
we jipange wewe kama wewe huna sababu ya kutegemea baba akuwezeshe

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…