Loly
JF-Expert Member
- Mar 10, 2011
- 522
- 221
Wapendwa wana Jamii Forum naombeni msaada wenu kuhusu huyu baba yangu mzazi.
Kwa kifupi mimi ni mtoto wa nje ya ndoa ninatambulika kwenye familia na kwenye ukoo ninashirikishwa kwenye kila kitu kwenye majukumu ya hela na mambo mengine.
Baba yangu huyu hakuwa na uwezo siku za nyuma alikuwa ananisumbua sana kuniombaomba hela na nilikua nampa japo nikishingo upande maana hajanilea toka aliponitelekeza nikiwa mtoto kwa mama yangu hadi nimemaliza shule nimekuwa mtu mzima nafanya kazi ndipo alipo nitokea nakujionyesha ananipenda nikawa namjali kwa chochote nilichonacho. Sasa hivi baba huyu kapiga bingo ana hela kama uchafu cha ajabu hana time na mimi.
Anawasaidia watoto wake wengine mitaji na mambo mengine mengi mazuri kasoro mimi, kanitenga kama mtu baki jamani na hajawahi kunifanyia chochote kama mzazi kwenye maisha yangu. Nimelelewa na mzazi mmoja toka utotoni sijui ladha ya baba ikoje ila nilivyokua ndio kaanza kujipendekeza kwangu na wala sio kwa upendo ni kwa ajili ya shida zake.
Hivi majuzi bila aibu aliniambia nimsaidie kumtafutia mtoto wake sehemu nzuri ya kufanyia biashara anataka kumpa mtaji bila hata kujiuliza huyu nimeshamtendea lipi kwenye maisha yake.
Jamani huyu ni baba anaestahili kuonyeshwa upendo kweli? Maana sijawahi kufikiria au kuzania kuwa siku huyu baba yangu mzazi akiwa na hela atanidharau hivi.
Jamani wana jamii naombeni mchango wenu.