hii thread imenifunulia mengi sana juu ya mioyo ya wanadamu.

1. yaani upendo siku hizi ni (officially) conditional upon how much money someone gives you (hata kama ni mzazni wako wa kukuzaa)!

2. kumbe hata baadhi ya watu wanaojifanya kuwasaidia wazazi ni kwa sababu walipata chochote toka kwao au wanataka kujionyesha tu kwa jamii kuwa wanatimiza wajibu wao lakini mioyo yao iko mbali kabisa!

3. undugu wa damu tena hauna nguvu, bali pesa kwanza, hakuna pesa, undugu unatupwa kule mbali!

4. nk

halafu eti watu wanajifanya kushangaa mfano kwa nini siku hizi mapenzi yamekuwa ya pesa tu, bila pesa hakuna mapenzi ya dhati. sasa kama ubaba/umama/undugu vyewnyewe vinaamuliwa kwa pesa, leo itakuja kuwa mapenzi?

na kama pesa ni muhimu kiasi hicho, kwa nini watu wasifanye ufirauni wa kila aina ili wapate pesa, kwa nii yasitokee mauaji, ushirikina, ukahaba, ushoga, ufisadi, rushwa nk. kwa nini tunawalaumu, jairo, chenge, shimbo, rostam nk wakati bila hela ama ufisadi yatawakuta haya yanayoendelea kati ya Loly na baba yake?

mmh, kwa kweli maisha haya bila Yesu ni hasara moja kwa moja!

wapendwa, mrudieni Mungu muweze kuyaona tena maisha katika maana yake halisi na katika makusudi ya Mungu.

muwe na amani na mbarikiwe wote