Jamani huku dagaa tayari zimeanza tusilale kizembe ziwa la watanzania

Wakukaanga kilo nauza shingapi??

Nipo mkolani hapa stand
 
Hapana😄😄,.
Wanaweza kukaangwa yaani namaanisha wakiwa hawajakauka kama hivyo
wanaweza kukaangwa tena wanakuwa wazuri sio kama hao waliokauka!.. ukiwachapa na ugali wa dona uliochanganywa na unga wa muhogo halafu kachumbari pembeni unaweza kujikuta unaniambia "Baby nitongoze tena!"..😂
 
wanaweza kukaangwa tena wanakuwa wazuri sio kama hao waliokauka!.. ukiwachapa na ugali wa dona uliochanganywa na unga wa muhogo halafu kachumbari pembeni unaweza kujikuta unaniambia "Baby nitongoze tena!"..😂
Umepatia vilevile nlivyokua nawaza..
Napenda sana dagaa aisee
 
Siku nyingine wachana na karanga kisamvu weka nazi .... Kiandae jioni au usiku halafu kiliwe siku ya pili 😋😋😋
Niweke mimi tena!!!, Baby hivi nani huwa anapika mimi au wewe..?😂
 
Mh! Kono, kono hasa ukinikamata si waweza kunivunja wewe!
Hongera sana kwa kujitafuta, tupe bei ya gunia na location tutathimini kufanya biashara.
 
Hao wa mafuta means unawaandaa wakiwa hawajakauka kabisa si ndyo??

Sijawahi kuonja hao dagaa wakiwa wabichi nataka nitaste nione ladha yake inafananaje
Labda uwakaange kwenye mafuta kwa namna ya kuwakausha kama ifanyikavyo kwa samaki. Vinginevyo dagaa wa ziwa Viktoria ukiwapika wakiwa wabichi (binafsi walinishinda~sio watamu) kama wakikaushwa au hivo nilivoelezea hapo juu.

Dagaa watamu kwa kuwachemsha wakiwa wabichi ni dagaa Mchele (wale wa maji chumvi). Niliwala kwa mtindo huu nikiwa bagamoyo ni watamu sana. Unawachemsha unanyunyizia mafuta kwa mbaaali na kitunguu kwa mtindo wa chukuchuku. Ni watamu balaa, japo hawafikii utamu wa dagaa nyasa wale wanaitwa LUPAMBU unawajua?
 
Dagaa nyasa ndio tunawala huku saizi watamu sana,. Hivi Lupambu ni wale wanaochemshwa hadi wanaganda au ni wale wanaochomekwa vijini wanabanikwa??
Huku kwetu hao ndio msimu wake huu saiz
 
Wa huku mwanza wanakaangwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…