Jamani huku makazini mwetu kuna kazi

Jamani huku makazini mwetu kuna kazi

shuka chini

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2024
Posts
842
Reaction score
1,928
Aise wadau salama kabisa.

Aise nimeishiwa pozi jamani. kazini huku kuna kazi aise ni balaa ipo hivi hapa ofisi kwetu mm ni mtu wa tatu kiutawala sasa yupo mkuu wa idara na msaidizi wake halafu nafuata mimi.

Sasa kuna jambo fulani lilifanyika hapa ofisini ikabidi nishirikishwe sasa baada ya jambo kutiki msaidizi akanifata akaniambia kuwa inabidi tupate fungu na hata katika makubaliano ya mwanzo ilikuwa mchongo ukitiki tupate mgao kidogo.

Sasa baada ya mchongo kutiki mkuu wa idara akawa kama vile analeta chengachenga msaidizi wake akanifata na kuniambia kuwa tumfate jamaa atupe chetu .tulipo mfata akasema atatupa leo.

Sasa leo nikaona kamuita msaidizi akampa chake bwana ikabidi nimfate msaidizi kumuuliza kama kapewa akasema amepewa kumuuliza ngapi akanitajia kiasi.

Sasa ikabidi nimtafute bosi akasema tutaonana nae jioni.

Aise kanipigia anakoroma eti hapendi kufatiliwa. Kumbe msaidizi wake alimpigia akamwambia kuwa nimemfata nikamuuliza kiasi eti nalo limekuwa kosa kwamba namfatilia.

Tuishi kwa umakini na baadhi ya watu sasa jamaa kumwambia vile sijui lengo lilikuwa ni nini? Hivi hapa bosi kasema jumatatu kikao maana ameniuliza nikakataa kuwa sikumfata jamaa nimemwambia kuwa jamaa ndio alinifata kuniuliza na mimi nashikilia msimamo huo. Jamaa anataka aonekane mzuri kwa bosi wakati ananjaa balaa.
 
Vitu kama hivyo vikitokea unatakiwa kukaa kimya na kujifanya hujui kinachoendelea hata kama umeshiriki, yeye mwenyewe mgawaji hawezi akawa anapishana na wewe bila kuona aibu na lazima awe na swali kichwani kwake kua kama ikitokea ishu nyingine ata i operate vipi
 
Back
Top Bottom