Jamani huku makazini mwetu kuna kazi

Aahaa, kumbe ndicho unachopanga kwenda kudanganya.

Na-screendhot hii jumatatu ukileta za kuleta naitoa kwa bosi. Lazima utie adabu unaniita mimi njaa kali, basi tutajua kati ya mimi na wewe ni nani njaa kali.


NB: Hivi unapoandika km hivi unajuaje kuwa bosi au msaidizi wake hawapo JF?

Ungepita kimya na kusubiri j3 kukutana na hao watu na wewe kufanya uliyopanga bila kupost hapa ingepunguza au kuongeza nini?!! Stress!!!!!
 
Subiri hiyo j3, ila Duu kumbe ndiyo maana watu wanatekana
 
Sema unaweza kuta jamaa hajamwambia kweli bosi wako. Bosi anakupanga tu ili awafarakanishe na kuvunja nguvu yenu. Yeye ndiye amezingua kwa kutaka kuwakata mpunga, deal naye yeye. Achana na msaidizi wake.
 
me nakumbuka waligawana pesa mbele yangu kimya kimya,
na kazi tumefanya wote na mimi nikaamua kukaa kimya;
baada ya kumaliza miezi ya probation wakaja kunikalisha kikao kuwa walikuwa wananipima ile siku nilipewa bahasha Iko na dollar 500, tokea hapo Kuna deals zilikuwa zinapigwa mtu hujui ila jioni unakutana na bahasha.
 
Hata mimi huwa natumia akili sana...
Kiufupi tu haya mambo ukienda kichwa kichwa utaishia kujambia hiko ulichosema kweli wala sio uwongo bichwa...

Kingine bichwa wewe una akili sana leo ndo nagundua hili aiseeeee 😁😁😁😁😁😀😁😀😁
 
Aisee inafikirisha Sana -je hizo ndo tamaduni za Kampuni ?UPIGAJI.
 
Wewe na mabosi wako wote wawili jipelekeni TAKUKURU (ingawa huenda nao ni walewale)...
 
Akimwaga ugali sheik we mwaga mbogaa.iweejee mlemchongo akuzungukee.mi kuna watu wawili katika maisha na subiria tu..walinamwagia ugali
 
MREJESHO: Nilimfata bosi tukaongea kabla ya kikao tukaongea yote jamaa nimemwaga mboga yote ya yule mnafiki nimeyasema na baada ya hapo kikao kikawekwa na muda huu ndio kimeisha.

Mkuu kamuonya jamaa kumbe jamaa kachomesha wengi na hiyo ndio tabia yake huyu msaidizi wake kazi yake ni kuchomesha wengine.
Na kibaya zaidi anaongeza na chumvi sasa picha inaanza kila mtu alipewa muda wa kujieleza na ndhani kwa kilichomkuta jamaa sidhani kama atarudia umbeya maana stafu wote wamemchana mbele ya mkuu wa kitengo.

Baada ya kikao bosi kaniita chemba tukamalizana na najua humu hayumo hata msaidizi wake humu hayumo.

Mwisho.nyie wenye tabia zq kujipendekeza kwa mabosi acheni unajua hata mabosi wanawaona nyie niwapumbavu aise najua hata humu wamo wenye tabia kama hizi .acheni mnaboa mtakuja kurogwa bure wapumbavu nyie
 
Acha matusi wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…