Jamani inawezekana vipi nikachaguliwa chuo ambacho sikukiomba

Dorah87

Member
Joined
Aug 23, 2022
Posts
20
Reaction score
7
Jamani inawezekana vipi nikachaguliwa chuo ambacho sikukiomba Yan nilichaguliwa chuo Cha Kampala dirisha la kwanza na mimi sijawahi kukuomba hiki chuo niliomba udsm ,ardh na mzumbe lakini sikuchaguliwa.

Nilirudia dirisha la pili tena ndo nasubilia matokeo Sasa Leo napigiwa na chuo Cha Kampala eti nilichaguliwa kuangalia majina ya waliochaguliwa Kampala na mimi nimo wakat sna hata account.

Yaani ufupi sijui chochote wakaniuliza waconferm au wakansel me nimesema wanifute maana coz nimechaguliwa ambayo hata vyuo nilivoomba sikuwahi ijaza sasa walivonifuta siku zimebaki nne tu selection zitoke hapa nna hofu Kama ntachaguliwa jamn nifanyeje?
 
Itakuwa Kuna mtu ulimpa information zako,

Alikusaidia kuapply,(na yawezekana alifanya hivi,kuepusha wewe kutokupata chuo sababu ya competition)

Matokeo yako yapoje?
 
Bora usingewaambia wa cancel wakati unasubiri miujiza huko kwingine katika hizi siku 3
 
Usikubali kwenda uko hao watu wa selection wanapewa rushwa kupewa wateja na kampala

Nenda TCU kalalamike
 
Hata Mimi niliapply mwenyew nahakuna mtu mwenye details zangu lakini nshapogiwa simu na vyuo ambavyo hata sikuomba taarifa sijui Huwa wanazichukua wapi
 
Bora usingewaambia wa cancel wakati unasubiri miujiza huko kwingine katika hizi siku 3
Me niliona Bora kuwabiwa ku cancel make siwez enda chuo ambacho sikitaki ngoja nisubilie majibu kwanza
 
Hata Mimi niliapply mwenyew nahakuna mtu mwenye details zangu lakini nshapogiwa simu na vyuo ambavyo hata sikuomba taarifa sijui Huwa wanazichukua wapi
Hapo hapo tcu..maafisa wa tcu wanapewa rushwa na wamiliki wa vyuo vya private ili wapate info.

#MaendeleoHayanaChama
 
Pole kuna taarifa kwamba baadhi ya vyuo binafsi vinafanya lobbying TCU vipangiwe wanafunzi ili vipate fedha iether kutoa HESLB au kwa mwanafunzi mwenyewe
 
Hiki kitu mimi sikubaliani nacho, mimi najuwa maombi unatuma kwenye chuo kwa kuingia website ya chuo husika,kuhusu kupigiwa simu mimi mwezi uliopita kampala na Mihayo ya Tabora walinipigi simu nikawaambia sijaomba kisoma chuo chochote, hili sielewi wao taarifa wanazitoa wapi mpaka wakuconfirm wakati haujaomba
 
Back
Top Bottom