Jamani kosa langu lipi hapa

Jamani kosa langu lipi hapa

mama pita

Member
Joined
Jul 20, 2012
Posts
97
Reaction score
139
Sijui kosa langu lipi hapa iko hivi,

Kuna kijana hua anafanya kazi na me wangu sasa hua anatabia yakuja kila siku jion kula nyumban. Yeye kapanga nadhan mvivu kupika tumeshamzoea ni kama mwaka sasa na hatoi hata mia, Sasa mume wangu huaa anatoka saa 3 kazini, mimi hua natoka saa 2 usiku dukan
Kama wiki hivi, nimemleta mtoto wa dada angu anisaidie majukum ana 17yrs.

Sasa huyu kijana alivyoona kuna mtu nyumban akawa anakuja nyumban saa 12 anakaa mpaka tunamkuta usiku. Mimi nilichofanya nimemwambia asiwe anakuja kukiwa na watoto peke yao maana yupo bint huyu na mtoto wangu wa 7yrs, awe anasubir mimi nirudi au awasiliane na rafiki yake waje nae sababu hapa kuna mtoto wakike dunia haieleweki hii.

Kachukia kanishataki kwa jamaa, mume wangu kanuna et ninaroho mbaya sitaki huyu kaka aje kula. Wakati mimi nimemwambia awasiliane na rafiki yake ambae ni mme wangu waje pamoja maana wanafanya kazi pamoja et nimekosea?
 
Mumeo nae fala nini, yeye ni mwanaume gani asiejua akili zetu wanaume, hicho ulichoamua ni sahihi kabisa, hakuna kuja mapema mapema, una binti wa miaka 17.

Ndio maana kwenye mafundisho imekemewa mtu kukaa na mtu ambae si halali yake(ambae anaweza kumuoa)
 
Ulipaswa umshirikishe kwanza mumeo Kisha huyohuyo rafiki yake ndo wangeelezana makubaliano yenu.. by the way mnawezaje kulea kitu kama hicho..?
Kiukweli angekataa sababu jamaa akisafir hua anakuja kunisubir dukan twende wote nyumban nikapike ale then aondoke, nikamwambia jamaa amwambie kua sio tabia nzuri mimi sio mke wake ni bora awe anakuja jamaa akiwepo ...alikuja juu safar hii nikajilipua
 
Kiukweli angekataa sababu jamaa akisafir hua anakuja kunisubir dukan twende wote nyumban nikapike ale then aondoke, nikamwambia jamaa amwambie kua sio tabia nzuri mimi sio mke wake ni bora awe anakuja jamaa akiwepo ...alikuja juu safar hii nikajilipua
Pambana nalo hilo usikute huyo ndo mlinzi kawekwa..😂
 
Eehe lakini sasa ndo aheshimu sheria unazoweka kwenye nyumba yenu
Mkuu rikiboy
Sio kwamba uyo jamaa anaeongelewa na mtoa mada Ni mwanachama wako kule kwenye ule Uzi wako wa kimasihara.

Anavizia akatekeleze ilani kwa yule binti wa kazi,ikiwezekana na kwa mama mwenye nyumba kabisa?[emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom