ninakaka yangu wa pekee ktk familia ya watu 5.ameoa mwanamke wa kioldmoshi.jamani dada huyo hafai.kwa uchoyo,mdomo na ubinafsi.kuna siku kaka yangu alitoa elfu 50 kumpa mama yangu imsaidie amefanyiwa oparation .mwanamke akachapa lapa kwao.yani hataki msaada wowote uende kwa mama yangu.ameshatusababisha ndugu wote tugombane na kaka yetu.ili aweze kufaidi peke yake kwa kumtawala.juzi mama yangu aliomba pesa ya kununua jiko kwa kaka.mkewe akatuma msg kwa mama.kwamba mumewe anabanwa sana na ujenzi kama hana mahali pengine pa kupata hela akavunje mahali aibe.ikabidi ndugu tuingilie kati kumuuliza wifi yetu kulikoni jamani anatutukania mama yetu aliyetulea kwa shida toka afariki baba yetu miaka 23 iliyopita.cha ajabu kaka alisaport alichokifanya na kukisema mkewe.yaani tumebaki midomo wazi. Na mshangao juu.jamani huyu kaka kalogwa au ni upoyoyo wake mwenyewe?
Disclaimer: Sitetei wala kuunga mkono tabia chafu na ukosefu wa heshima kwa mzazi..Ok tuendelee..
Kwanza post imeshamuhukumu huyo mke wa kaka, hivyo nadhani sisi wadau ambao hatujui kinachoendelea inabidi tuwe waangalifu kwani kwa kutegemea source ya info ya upande mmoja twaweza kujikuta tunalalia upande mmoja.
Niki- assume hayo ya kwenye post ni sahihi basi huyo dada amemkosea mzazi heshima na hafai. Hata kama mapenzi ni ya watu wawili hata Mungu ametupa amri ya kuwaheshimu baba na mama. Kama mke wangu atakosa kumuheshimu mzazi wangu basi atakuwa amenikosea mimi, familia yangu na Mungu hivyo inabidi ategemee adhabu kali kama hatoomba msamaha kwa vitendo. Kwenye post hujasema kama baada ya kumsema alikubali na kuomba msamaha au iliishia vipi kwani hiyo issue lazima iishe kwa furaha au uchungu.
Pili, nikisoma naona mama aliomba jiko kwa kaka lakini jibu lilitoka kwa mke. Nadhani ni vizuri kabla ya ku-attack mke ilibidi muwaite kaka na mke kwa pamoja mbele ya mama na kumuuliza kwa nini kaka akumjibu Mama (kaka ajue yeye ni kaka, Baba ameshafariki hivyo kaka amebeba majukumu ya baba). Kama mke alikuwa kimbelembele kumjibu mama..basi ni muunganiko wa nilichoeleza hapo juu..Tabia chafu labda tu kama angejibu kwa niaba ya kaka kwa majibu ya busara..
Labda mmeshafanya hili lakini nadhani inabidi wakati mnampa kaka vijembe vyake inabidi mke wake awepo na muweke wazi kuwa ninyi binafsi hamtaki kula mali zake (inapingana kidogo na ulichosema
"ili aweze kufaidi peke yake" ) ila mnachotaka ni kuwa kaka ajijue kuwa yeye ni kaka na anamajukumu ya ukaka hamna nia na mali zake. Kutokana na mila zetu za kiafrika kaka akiwa hata mdogo anasehemu yake na heshima yake katika familia. Hamuwezi kumlazimisha lakini mnaweza kumsaidia ajue hilo. Jaribuni kuweka wazi kuwa kaka sio lazima atoe hela yake kwa mama kama yeye ajisikii aache na Mungu atamuadhibu binafsi kama sio leo basi ni kesho.
Kikubwa ni kuwa mtambue nyinyi ndugu mna limitation (wigo) katika maisha ya kaka na mke wake. Lakini mkumbuke pia mna ushawishi na wadau..mnaweza kumsaidia kaka yenu lakini inategemea kama kichwa chake kina akili au kimejaa mkamasi. Mama asaidiwe na wote. Ukosefu wa adabu wa mzazi na mmoja wenu iwe mtoto, mke, mume, kaka,dada hauvumiliki.