Jamani mjitahidi sana kutunza magari yenu

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2020
Posts
3,381
Reaction score
9,744
Kiukweli leo nimesikitika sana baada ya kukutana na gari iliyoingia nchini mwaka jana(2021), Ni zile namba D za mwisho mwisho lakini tayari ina majanga makubwa mno.



Gari yenyewe ni Porsche Cayenne na ina Kilometre hazijafika hata laki, lakini tayari ilishaua control box (DME control unit) na wire zishakatwakatwa (Labda hii ndio sababu).



Tumezoea kwenye gari zingine za kijerumani Control Box zinakufa na maji, mtu anaenda kurekebisha gari, ikishafunguliwa sehemu ya Control box wakirudisha hawarudishi na raba au wanarudisha vibaya. Baada ya muda kwisha habari yake.

Lakini hii gari control box yake iko sealed sana. Sijui waliipigisha shoti. Sijui.

Gari inapendeza nje bodi halina hata mkwaruzo ila faults za kutosha baada ya kuifanyia diagnosis. Zaidi ya fault 60.



Kusema ukweli shida siyo gari, Ila shida ni sisi ngozi nyeusi. Kuna mtu yupo humuhumu JF ana Porsche Cayenne namba C lakini hajawahi pata major issues.





Kwa Diagnostic na Repair ya gari ndogo kampuni yoyote 0621 221 606 au 0688 758 625.

Nipo Dar.
 
Kaka umenena. Huwa tunasingizia barabara mbovu lakini barabara inahusiana vipi na kuharibika hasa vitu vinavyohusiana na umeme.

Au engine? Shida ni service za magumashi na vifaa vya kuunga unga. Nimenunua gari used bongo ila sitakuja kurudia tena huo upuuzi.
 
Nini kimekukuta mzee ?
 
Toyota was made for tanzania
Ukweli usiopingika. Nina toyota moja tangu 2014 mwishoni imported from Japan mbaka leo huwa ni service tu labda control box nilibadili 2018 basi ila ni mwendo tuuu....toyota ndio gari zetu ngozi nyeusi hazsumbui sana....hata wenye pochi nene hizo british na germans znawasumbua sanaa tuu
 

Hii ni diesel? Fault moja hapo inaonyesha kama vile ‘fundi Maiko’ alijaribu kufanya programming kwenye ecu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…