Wakuu nashukuruni sana kwa mawazo yenu. Kiukweli huyu jamaa nimeamua kumsamehe na kuendelea na maisha. Nilijaribu kumsihi sana kama ndugu kuwa uaminifu ndiyo mtaji mkuu wa mjasiriamali ila naona hakuelewa.
Siku zote nitapenda asipate matatizo ili aweze kupata moyo wa kujutia na kujifunza maana inawezekana ameanguka kwenye tamaa na bado hajajitambua.
Nitaomba wale wote tuliotapeliwa tumsamehe kama ikiwezekana na tujipange upya maana hapa jamvini kuna watu wengine wengi tunaweza kufanya nao hii biashara ila kikubwa niwaombe uaminifu ili hizi online b/ness zizidi kuaminika hapa jamvini
Mwishoni kabisa nitaomba hii iwe changamoto kwetu wote (wanunuzi na wauzaji) na tusife moyo kwenye kufanya hizi biashara za online maana kuna theorem moja ya hesabu inasema "a singular cited example can't prove the entire theorem". Mtu mmoja mwenye tabia mbaya asiharibu mambo yetu mazuri. Naamini hii ni case ya kwanza kabisa kutokea kwenye jukwaa dogo la ujasiriamali
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki JF, Mungu bariki wajasiriamali
Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums