Ethan Wayne
Member
- Nov 29, 2013
- 52
- 8
Mweeeee
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
wazo la jf kuact kama paypal na kushikilia pesa hadi costumer aconfirm delivery ni wazo mwafaka na litakua la faida wa jf kama kunakua na fee(service charge).Poleni sana jamani, inarudisha nyuma wengine. Halafu pia inaharibu sana biashara hapa maana kuna wasio member pia watakuwa wameathirika hawawezi report hapa na itawaogopesha hata kufanya biashara na sisi. Binafsi nilipigia debe sana kuanzishwa mfano wa gulio la bidhaa zetu nadhani tukio hili ni changamoto tunayopaswa kuiangalia kwa makini. Kuanzia tu iwepo onyo hapa kutofanya malipo na mtu usiyemjua, kama ilivyo kwa Alibaba nk mtu atayetaka kufanya biashara kwa malipo ya awali awe verified user na tuombe JF ikae na fedha hadi mnunuzi areport amepokea alicholipa na iwepo commission fulani inalipwa kwa mmiliki JF. Vinginevyo mnunuzi mwenyewe fanya tathmini yako hadi uridhiki ndio ulipie. Nimeuza kiwanja na nikanunua kiwanja hapa, nimenuniua vifaranga na pia kuku wakubwa kwa member hapahapa. Sio wote wezi lakini tunashkuru sana kwa taarifa na lolote likitokea kinyume na makubaliano tafadhali tutoe taarifa ili hao wapuuzi wasirudie kuchafua hapa. Niwatakie kazi njema wote
wazo la jf kuact kama paypal na kushikilia pesa hadi costumer aconfirm delivery ni wazo mwafaka na litakua la faida wa jf kama kunakua na fee(service charge).
aisee asante sana mleta mada, umetuokoa wengi, maana nilikuwa nami kwenye mchakato wa kuagiza hao bata mzinga mbona ningelia. Anyway alichofanya kitomari2 ni kibaya sana na imetia doa ili jamvi letu pendwa la ujasiriamali. wengi tumefaidika kwa kufanya biashara na watu ambao tumewajua kupitia ili jamvi na hatujawahi pata matatizo kama haya.
on a second note, sasa wapi naweza pata hao batamzinga, maana bado nawahitaji. SIKATI TAMAA
Kama bado mawasiliano,mwambie aje jukwaani ajibu ,sina nia ya kumtetea bwana kitomari2 ila nahisi atakuwa ameingiwa na tamaa ya kujipatia kipato bila kuwa na mzigo wa kutosheleza wateja wake. Binafsi nina experience nzuri naye ingawa hatujawahi kuonana. Nilimtumia pesa kwa m-pesa akanitumia vifaranga wengi kuliko thamani ya pesa niliyomtumia, nikamuona mwaminifu sana! akasema hivyo vilivyozidi nimtatutie pesa zake, nikaona poa sana. Tayari nimeishamlipa lakini bado ananidai pesa kidogo tu nimalizie hao waliozidi.
Sasa hizi habari za utapeli wake zimenikatisha tamaa sana kuendelea nae. Nahisi ananilia timing ndo anitapeli, nilimwambia najipanga then nimtumie hela anisafirishie mzigo mkubwa zaidi ya huu wa kwanza. Duh, imenikatisha tamaa sana aisee, nitamtafuta kwa simu nimwambie haya malalamiko maana mimi nikimpigia anapokea, hata nikituma sms ananijibu, nahisi bado narushiwa punje za mahindi niingie mkenge!!!!
Kama bado mawasiliano,mwambie aje jukwaani ajibu ,
Sio tu kuja jamvini anatakiwa arudishe pesa za watualipwatapeli au awatumie mizigo yao waliyoagiza kwakenilimwambia akashangaa sana, alionyesha kutokuwa na taarifa kuwa limebumbuluka, ila akasema atakuja manake alikuwa hajawa na access ya internet
Mimi ninaanza kuamini kuwa ndugu kitomari2 atakuwa tapeli la kimataifa. Kama mtu hakuyatenda haya angekuja hapa fasta kukanusha. Tena ukizingatia simu za wengine anaotaka kufanya nao biashara anazipokea. Shetani amtangulie ndugu kitomari2 kwa utapeli wake.
0757662401
Umempigia anasemaje?Kweli Mamamkwe, bado yupo hewani kabisa kwa namba hii 0757662401. Wala hana wasi wasi kabisa.
Umempigia anasemaje?