Jamani yule njiwa alieingia nyumbani nikamtoa nje leo tena amerudi

Jamani yule njiwa alieingia nyumbani nikamtoa nje leo tena amerudi

Mkarimu, usimtoe nje ya geti ataliwa ! Mpe chakula n maji,,,, hopefully ni mgonjwa, na huenda walipata ajali na mwenzie akauwawa, sasa yeye akafanikiwa kukimbia na alijeruhiwa,,,,upweke ni kwa sababu huwa wanakaa wawili wawil ! Akipona anaweza kuendelea kukaa hapo ama akaenda kwenye destination zone yake,,,
 
Kama kuna kakibanda sehem salama ambayo hawez shambuliwa muweke humo, ama chukua box kubwa kiasi toboa vitobo vya hewa muweke,,,, maji chakula usisahau ,,,,
 
Njiwa ni rafiki hana shida mpe msosi mtengenezee na banda!
unaogopa njiwa wenzako tunatembelewa na bundi na tunawaifadhi tu!
 
Jana niliandika uzi kuhusu njiwa kuingia nyumbani kwangu wakati wa mvua na alionekana wala hata hagomi kushikwa alikuwa mtulivu tu, hata akiruka anarudi mahala flani kwa muda huo

Sasa jana tulimtoa nje usiku leo asubuhi mida ya saa tano karudi , sasa tumemuacha tu.

Tusaidiane mawazo wakuu

Usiogope ndugu yangu. Ngoja nikupe ushuhuda wa kweli. Mimi kuna mnyama wa ajabu sijawahi kumuona maisha yangu yote. Nilimuona nje ya mlango wa kuingia ndani ya nyumba. Ana umbo dogo kama mpira wa tennis, ila kwa chini yuko bapa kidogo. Hana miguu wala kichwa wala mikono wala macho. Amejaa manyonya madogo madogo mwili mzima. Hasogei mbele wala nyuma. Anapumua kwa namna ambayo unaona waziwazi mwili unatanuka tanuka. Nadhani ungemuona huyo hapo kwako angekutisha zaidi. Mimi nilishuhudiwa moyoni kwamba huyo sio mnyama wa kawaida. Ametumwa na wachawi kunifadhaisha. Nilichofanya, nilichukua koleo nikamchota, nikamtupa nje ya nyumba huku nikitamka "Kwa Jina la Yesu" ili kama ni mnyama aliyetumwa kwa njia za kichawi basi uchawi huo ushindwe. Hakuonekana tena mpaka leo. Hii ni faida mojawapo ya kuokoka. Nimeorodhesha humu maajabu ya maisha ya watu waliookoka, na mojawapo ya maajabu hayo ni kwamba "Hawalogeki," lakini wengine wamebeza eti ni "chai"
Kwa kawaida njiwa wa kufugwa huwa wanarudi 'nyumbani kwao', na wewe umesema hakuna jirani hapo anayefuga njiwa. Ulisema pia njiwa huyo alikuwa hawezi kuruka. Sasa jiulize amerudije tena ndani wakati ulimtoa nje ya geti?

Usikubali mtu akudanganye uende kwa waganga. Hapo ndio utajiharibia kabisa.

Nakushauri uamue kuokoka leo. Ukifanya hivyo sasa hivi utakuwa na mamlaka ya kukemea nguvu za kichawi kwa Jina la Yesu. Jina la Yesu linapotamkwa na mtu aliyeokoka linaharibu kazi zote za kichawi. Lakini likitamkwa na mtu ambaye hajaokoka, halileti matokeo.

Ukiishaokoka, mchukue huyo njiwa umrushe nje ya geti huku ukitamka "kwa Jina la Yesu." Kama ni njiwa wa kichawi hutamuona tena akirudi nyumbani. Kama ni njiwa wa kawaida amepotea njia, akirudi hutaona madhara yoyote hata akiendelea kukaa hapo. Na utakuwa na amani sana.

Ukiomba sala hii ya toba, sasa hivi utakuwa umeokoka na utakuwa na mamlaka ya kuharibu nguvu za giza. Tafadhali omba sasa kwa moyo wako wa dhati sala hii ya toba. Omba kwa kufuatisha sala hii:
“Ee Mungu Baba, nimetambua mimi ni mwenye dhambi. Leo nakuja mbele zako nikiomba msamaha wako. Natubu dhambi zangu zote na kuziacha. Nakiri kuwa Yesu Kristo ni Bwana, na Yeye ndiye Mwokozi wa ulimwengu. Yesu karibu moyoni mwangu utawale maisha yangu kuanzia leo. Naomba unipe nguvu ya kushinda dhambi na kuishi maisha matakatifu. Namkataa shetani na kazi zake zote. Asante Yesu kwa kuniokoa. Katika Jina la Yesu Kristo, ninaomba na kushukuru. Amen.”

Kama umeomba sala hiyo kwa moyo wako wa dhati, tayari umeokoka. Chukua hatua ile sasa ya kumtupa nje huyo njiwa kwa Jina la Yesu.

Baada ya hapo anza kusoma Biblia kila siku na kumuomba Mungu akusaidie kuendelea vizuri kiroho na kukuepusha na hila zote za shetani na wachawi. Tafuta pia Kanisa linalohubiri wokovu na kufundisha utakatifu, ujiunge nalo, watakupa msaada zaidi wa jinsi ya kukua kiroho.

Mungu akubariki, Mungu akulinde, nami nitakuombea mipango yote ya wachawi dhidi yako ishindwe kwa Jina la Yesu. Amen.
 
Alkasusu1.jpg
 
Pole kwa kilichotokea!

Njiwa ni ndege mzuri sana! Ambaye kwenye vitabu vya dini ameelezewa kama ndege wa Amani, utulivu na furaha!

Wengine wamediriki kusema njiwa hakai mahali pasipo na Amani.

Lakini hata hivyo pia njiwa amekuwa akitumika zamani kwenye dola za kale kupeleka habari kwenye dola nyingine, kwa kufungiwa barua miguuni mwake!

Hata hivyo wachawi au washirikina nao pia wamekuwa wakimtumia njia pamoja na viumbe wengine kama paka, bundi, nyoka, mijusi, vipepeo, nge, majongoo, maduduwasha, n.k. Kwenye kazi zao mbalimbali.

Ndio njiwa huyu huyu amekuwa anatumiwa sana kishirikina, mimi bibi yangu mzaa mama, alizaa watoto wenye akili sana pale kijiji, kwa wivu, akiwa shambani analima ghafla alitokea njiwa akamgonga kichwani/usoni, bibi akachanganyikiwa, tangu hapo akawa kichaa akaumwa mpaka akafa!

Dada yangu ninayemfuata alikuwa anaumwa lakin sio sana! Mara siku moja amekaa kibarazani akatokea njiwa wa kijivu blue, anakidude chekundu mguuni tunamfukuza hakimbii, alianza kuishiwa damu hadi akafa!
 
Jana niliandika uzi kuhusu njiwa kuingia nyumbani kwangu wakati wa mvua na alionekana wala hata hagomi kushikwa alikuwa mtulivu tu, hata akiruka anarudi mahala flani kwa muda huo

Sasa jana tulimtoa nje usiku leo asubuhi mida ya saa tano karudi , sasa tumemuacha tu.

Tusaidiane mawazo wakuu

Njiwa tu unaogopa, na angehamia bundi?
 
Njia ni alama ya Roho mtakatifu,pia alitumiwa na Nuhu duniani akarudi na jani kwa Nuhu kuashiria kuwa maji yamekauka kwa hiyo dunia ni salama,baada ya kunguru aliyekuwa ametumwa awali na Nuhu kuzamia hukohuko kwa uroho wa kutafuna mizoga ya binadamu.ningekuwa ni mimi ningemjengea kibada kabisa aishi kwa amani.
 
Kuna njiwa alitua kwenye kordo watu wakiwa sebleni halafu hawana hata habari wakajua njiwa hawezi kupa,mpka nilipo fika mimi nakumuangalia vizuri nilikuta mguu wake wa kushoto ulikua nakitambaa cheusi ebwanaa eeeh 😂 hapa ndo palikua patamu maana kila mtu anamuliza mwenzake kama kuna ishu yoyte imetokea
 
Back
Top Bottom