Jambazi aliyetuibia TV mwaka 1988 nimemuona leo akiwa mzee

Jambazi aliyetuibia TV mwaka 1988 nimemuona leo akiwa mzee

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
Kweli milima haikutani jambazi lililotuibia tv mwaka 1988 Raskazone Tanga nimeliona leo limezeeka linaishi kwa mtoto wake pale Mabibo jeshini linaumwa figo miguu imevimba balaa.

Kilichofanya nimtambue ni kovu lake juu ya jicho na huyo mwanae anaeishi nae japo wao wamenisahau.

Moyo unaniambia nimfwate mshkaji nimueleze kwamba ujambazi wa baba yako ulituletea umaskini kipindi tv za kwanza ndio zinaingia Tanzania.

Jamaa hawezi kunifanya lolote am now powerful than them I may do anything to them and leave unharmed.

Lengo nimlipie kisasi marehemu baba yangu.

Sitarajii kuwadhuru ila hata nikikumkumbusha huyu mzee uhalifu wake moyo wangu utaridhika.
 
Kwa hayo maradhi muache tuu au kama alimdhuru baba yako mwambie kuwa unakumbuka alichofanya hakikuwa kizuri na atubu kwa mola wake.
Hakumdhuru baba ila jiwe fatuma lilivunja mlango likaharibu Sana Mimi nilikuwa mdogo na tv aliyoiiba ilituuma Sana. Mnaokaa mabibojeshini mnaweza kuliona hilo zee semakota ni nyingi.
 
Kinachoniuma ni baba yangu kashafariki halafu ndio namuona huyu mbwa.

Chukulia kawaida tu mkuu maana muda ushapita na huwezi jua yule wa jana na leo ni watu tofauti na ninaamini pia hata wewe kuna vitu ulivifanya kutokana na situations ama umri ambavyo nina uhakika huwezi kuvifanya leo. Chukulia ni ubinadamu tu na cha msingi zaidi hakuwadhuru au kutoa uhai wa mtu maana ingekuwa issue ingine.
 
Kamshauri aandike kitabu cha maisha yake ya ujambazi. Hasara na mikosi na ubaya wa uovu wake
Kule mbeya kwenu wakati kasusura anakamatwa pale Soweto 3 in 1 Mimi nilikuwa kwenye kiuchochoro kinachoelekea gereza la watoto liko hapo Soweto ile muvi ya kasusura niliiona nusu tokea hapo majizi na mawezi nimeyagawa sehemu mbili wenye akili Hawa huiba bank na wajinga hawa hutuibia sisi maskini wenzao kama hili zee la hapa mabibo. Ni jizi jinga.
 
Ebana eeh!

Duniani kuna Mambo

Ila kua makini na uyo dongo.
 
Back
Top Bottom