Jambazi aliyetuibia TV mwaka 1988 nimemuona leo akiwa mzee

Jambazi aliyetuibia TV mwaka 1988 nimemuona leo akiwa mzee

Kweli milima haikutani jambazi lililotuibia tv mwaka 1988 raskazone tanga nimeliona Leo limezeeka linaishi kwa mtoto wake pale mabibo jeshini linaumwa Figo miguu imevimba balaa.

Kilichofanya nimtambue ni kovu lake Juu ya jicho na huyo mwanae anaeishi nae japo wao wamenisahau.

Moyo unaniambia nimfwate mshkaji nimueleze kwamba ujambazi wa baba yako ulituletea umaskini kipindi tv za kwanza ndio zinaingia Tanzania.

Jamaa hawezi kunifanya lolote am now powerful than them I may do anything to them and leave unharmed.

Lengo nimlipie kisasi marehemu baba yangu.
Sifarajii kuwadhuru ila hata nikikumkumbusha huyu mzee uhalifu wake moyo wangu utaridhika.
Pole Sisi miaka ya 198x... maeneo ya Kilimaewa Manzese Midizini Dar es salaam, Binti alitutapeli Mikate ya SIA( national milling breads) minne(4) Breads!!!

Mimi After 4 Years nikamwona Sehemu, nikaita wazazi tukamkamata.....Alilipa zaidi ya mikate....pole na Hongera no mercy no fear Alipe
 
Umeshindwa hata kuchukua kapicha ulikuta hata sisi wengine umeshawahi kukwala vitu vyetu
 
Chukulia kawaida tu mkuu maana muda ushapita na huwezi jua yule wa jana na leo ni watu tofauti na ninaamini pia hata wewe kuna vitu ulivifanya kutokana na situations ama umri ambavyo nina uhakika huwezi kuvifanya leo. Chukulia ni ubinadamu tu na cha msingi zaidi hakuwadhuru au kutoa uhai wa mtu maana ingekuwa issue ingine.
on point
 
Kule mbeya kwenu wakati kasusura anakamatwa pale Soweto 3 in 1 Mimi nilikuwa kwenye kiuchochoro kinachoelekea gereza la watoto liko hapo Soweto ile muvi ya kasusura niliiona nusu tokea hapo majizi na mawezi nimeyagawa sehemu mbili wenye akili Hawa huiba bank na wajinga hawa hutuibia sisi maskini wenzao kama hili zee la hapa mabibo. Ni jizi jinga.
[emoji23] [emoji23] mchane tu
 
Msamehe tu,kwa magonjwa na umri wake muda si mrefu atarudi mavumbini huyo
 
Sasa mambo gani haya yakunianika humu.?Njoo basi uniue kuliko kulialia humu. Sina cha kupoteza. Njoo uniue Njoo ulipize kisasi moyo wako ufurahi na utulie.
Watu wa chuga mibange Sana kwasauti ya mbasher
 
Usilipe baya kwa baya cha msingi nenda kawajulie hali ikiwezekana mpeleke hospital kama anashindwa kumudu gharama na msaidie kumuuguza...

Ethics especially based on natural law theory inasisitiza kuwa tusihalalishe baya kwa baya ila pia kumbuka

"Do unto others as you would have them do unto you...."
 
forgive and forget

kwenda kwa huyo mzee kumsuta ni kujitakia the unthinkable...move on achana nao

fikiri kama mtoto naye ni jambazi au bado pamoja na ugonjwa wake mzee bado ni jambazi mstaafu...eehh

au unataka mwanao kuja kusimulia namna nawe baba ulivyoibiwa kama babu yake na familia ya jsmbazi yuleyule!?
 
Lazima uniue hamna namna. Sitakubali uniache Hai. Hii ndio fursa ya kufa kwasababu siwezi kujiua. Bora kuniua kuliko kunianika humu. Sina cha kupoteza Figo zimefeli kugegeda siwezi tena. Njoo nimalize mazima ufurahi upate amani. Njoo ulipize kisasi kuliko kulialia humu.

Kamoooonn
U r learning to write scripts keep it up mkuu
 
Jambazi mstaafu mtungie riwaya chapisha...

Gusia matukio yote mhimu aliyoyafanya...

Jina la kitabu... Kisadifu picha ya kwenye jalada..

Baada ya hapo fungasha nakala moja ya kitabu... Na vizawadi kidogo vya kuboost maisha...

Hakika atatubu mbele ya kaumu ya watu.
 
Back
Top Bottom