Raskazoni Tanga, mwaka 1988 au ni mwaka 1998? Mlikuwa mnatumia Satellite Dish?. Kwa mji kama Tanga kuwa na TV enzi hizo, basi familia yenu ilikuwa ni ya kiongozi mkubwa sana tena wa ngazi za juu sana, asiyepungua kwenye rank ya Uwaziri. Hata Dar es Salaam, japo sikuwepo, ni watu wachache sana waliokuwa na Satellite Dishes, na ninadhani labda walikuwepo Masaki na Mikocheni tu, na ciy centre, possibly.
Dr. Rginald Mengi (RIP) ameanzisha TV kwa mara ya kwanza hapa nchini mwaka 1994. Eneo nililokuwa naishi mimi maeneo ya Manzese Tip Top kulikuwa na nyumba mbili tu zenye TV. Sasa jaribu kuu-retrospect ukweli huu na hali ya Tanga, na si Dar es Saalam. Unaweza kuwa umekosea bali ni mwaka 1998, kama ni kweli!