Mahita πWacha uboya wee! Kwani Mahita siyo jambazi?papaa musofe? Kwani ni machagga hayo?
Hakuna cha karma wala nini, alipangiwa atakufa hivyo pindi tu alipozaliwa.Sema karma inachelewa sana jamani 13 yrs!
Tayari hukoNgoja afe utasikia "Billionea mwingine afariki Arusha", "mazishi yake yagharimu millioni mia mbili", "jeneza lake linatumia android..."
2026Ngoja afe utasikia "Billionea mwingine afariki Arusha", "mazishi yake yagharimu millioni mia mbili", "jeneza lake linatumia android..."
Sawa kaka jambazi.tumekunywa naye sana hapo miaka hiyo...na vitoto vya IAA-tulikua tuna vi-import kuja hapo maeneo ...tukitoka hapo tunaenda Sarafina kula kitimoto choma.
I real miss Arusha,
Alipangiwa na nan? π€£π€£Hakuna cha karma wala nini, alipangiwa atakufa hivyo pindi tu alipozaliwa.
Wewe uliponea chupuchupu ulipowekewa vipande vya chupa kwenye msosi.Sawa kaka jambazi.
Siyo anko yako Kingai?Mahita π
Ameshaingia tayariHata hivyo ni kwamba ajaingia tu kwenye anga za baadhi ya watu maana angeshaondolewa fasta
Haya mkuu.... nimekusomaHiki nini? Ungeandika kwa Kiswahili ungepata hasara gani?
EheeIla sasa hivi litauwawa!
Hii jamiiforum ni zaidi ya Wikipedia na encyclopaedia BritannicaJamii forums ina kila kitu,ni vile wanaofanya doria humu huwa wanapuuzia taarifa nyingi.
Kiko wapi sasa? Na macho wamemtobowa.Banjoo mbona alitoka kitambo sana,
ana nyumba za kupangisha, anashinda kwenye bar wanazokaa polisi hasa maeneo ya kijenge na moshono.
anapiga watu na kuwahi polisi na kusubiri ukireport mnamalizana kwa makofi hapo mbele ya polisi ila ukiwa mjanja unalipwa hela ya usumbufu.
inasemekana anatumiwa na polisi kuvujisha siri za majambazi na matukio yao kama anavyofanya jambazi mstaafu kwa jina Mojaa ambaye pia ni rafiki wa uyo Banjoo mara ya mwisho walikua pamoja Blue House Fire Sinoni.
Hakuna polisi mkubwa mwenye uwezo wa kumuua Banjo labda askari wa chini sana au raiya wa mtaa aliyechafukwa sana.
Hatimaye yametimia, ukiishi kwa upanga, utakufa kwa upanga.Mkuu nduu/mamaya baada ya hapo ilibidi daktari wa zamu akishirikiana na uongozi wa hospital utoe taarifa polisi kwaajili ya uchunguzi.
Marehemu Major Makange Baba wa marehemu mtaalamu wa mizinga aliyesomea India na kushiriki kikamilifu katika operesheni ya kug'oa utawala wa Idd Amin wa Uganda na kwa wakati fulani akitumika katika jeshi la Uganda chini ya utawala wa Musevenii alikuwa mtu wa mwanzo kufika Mt Meru Hospital kushuhudia mwili wa Baby ukiingizwa chuma cha kuhifadhi maiti.Bila kuchelewa aliwaambia polisi mwanangu atakuwa ameuwawa na Sadiki Mkindi na lazima angelipa kisasi kwa kuapa kwamba Baby angekuwa mtu wa mwisho kuuwawa na Sadiki Mkindi.
Uchunguzi wa polisi ulianza mara moja kwa kuvamia makazi rasmi ya Sadiki kwaajili ya upekuzi na mahojianao ya majirani ambao walikiri kusikia vishindo na makelele ya malalamiko ya Marehemu Baby lakini hakuna jirani aliyethubutu kutoa msaada kwa marehemu kutokana na kuogopa ukatili wa Sadiki.Majirani waliendelea kufunguka zaidi walishangaa nyumba ya Sadiki ilikuwa na utulivu mkubwa wa zaidi ya wiki moja kitu ambacho si cha kawaida.Katika upekuzi polisi walifanikiwa kukuta nguo za marehemu zilizojaa damu nyingi sana hali iliyoashiria kwamba marehemu kabla hajapelekwa hospital alibadilishwa nguo ili kuwaadaa madaktari,wauguzi na dereva taxi wasigundue au wasihisi kitu chochote.
Msako wa kumtafuta Sadiki Mkindi ukaanza mara moja,iliwachukua polisi wiki kadhaa kumnasa Sadiki Mkindi Jiji Dar es Salaam na kumrejesha Arusha kwajili ya kumfungulia mashtaka ya kuuwa kwa kukusudia.Ukoo wa mkindi ambao tayari ulikuwa unanuka kwa maovu mbali mbali haukuwa na nafasi ya ushawishi tena juu ya yote mtu pekee alibaki na ushawishi alikuwa marehemu Brigedia Mkindi wakati akihudumu ofisi ya mkuu wa mkoa kama mshauri wa mgambo wa mkoa.
Kesi ilianza kunguruma mahakama kuu Jiji Arusha,Mashahidi muhimu walikuwa mlinzi wa Hospital ya Mt Meru ambae alikuwa akimfahamu vizuri Sadiki Mkindi kutokana na kulazwa kwa muda mrefu Hospatal ya Mt Meru akisumbuliwa na TB aliyoipata wakati akitumikia kifungo gereza la mkoa wa Arusha kwa makosa mengine ya mauaji.Daktari aliyeufanyia mwili wa marehemu uchunguzi pia alitoa ushahidi uliomtia hatiani Sadiki Mkindi na kuhukumiwa kunyongwa na mahakama kuu na baadae mahakama ya rufaa ilikubaliana na hukumu ya mahakama kuu ingawa mpaka leo bado hajanyongwa na hadhabu yake imekuwa kifungo cha maisha huku mwenyezi Mungu akimtandika kwa ugonjwa wa kupooza upande mmoja wa mwili.
Hawa ndiyo unaweza kusema walikuwa majambazi wa kutisha kwasababu kwanza walikuwa wameende shule,wakati mwingi walikuwa wanasoma vitabu mbali mbali kwaajili ya kuongeza ujuzi.walikuwa wakiangalia picha za kimafia ambazo pia zilikuwa kuwasaidia katika operesheni za ujambazi.Sadiki Mkindi mara kadhaa alikuwa akijitetea mwenyewe mahakamani mara anapobaini mwanasheria wake anashindwa kufikia kiwango anachokitaka isitoshe alikuwa na exposure ya kuishi Ulaya na kufanyabiasha kwa kipindi kirefu.Ukimweka Banjoo katika level ya Sadiki Mkindi ambae hata maafisa magereza wanakwambia ni mtu hatari asiyetakiwa kupewa nafasi hata kidogo ni kujinyima ufahamu wa mambo kwa kujitakia.Sadiki Mkindi ni jambazi anayefanya ujambazi kwakuwa ni sehemu ya maisha yake aliiba wakati alikuwa ameachiwa urithi wa nyumba nyingi katikati ya mji nadhani unafahamu thamani ya viwanja vya mjini ni shilingi ngapi,kodi za vyumba vya mjini ni shilingi ngapi......Banjoo ni kajambazi kwaajili ya kuganga njaa hana kitu hapa mjini,hana elimu,hana biashara,hana kazi hana analoweza kufanya kwa sasa hana network amebaki akijificha jificha kwenye vigrosaries na kuomba omba bia za wanaume wa mujini.