Mlaleo
JF-Expert Member
- Oct 11, 2011
- 16,378
- 13,198
"Banjoo" NI jambazi sugu la Silaha hapa Arusha lililokuwa linatumiwa kama kijana wa kazi na Nyari kuwapora wafanyabiashara madini ya TANZANITE yaliyokuwa yakipelekwa KIA kusafirishwa nje. Jambazi hili hatari ambalo linanuka damu za watu lilihukumiwa siku moja na Nyari mjini Arusha kifungo cha miaka 30 jela kwa ushahidi uliokuwa hauna shaka yoyote. Cha ajabu baada ya miaka michache tu Nyari aliachiwa na bila shaka yeye ndiye aliyeshughulika hadi swaiba wake Banjoo kuachiwa hata bila kukaa jela kujutia madhambi yake angalau kwa miaka 10 tu.
Banjoo namwona akitamba hapa mjini bila hofu yoyote.
Swali
Ni vipi tutatokomeza wizi wa silaha na mauaji ya watu wasio na hatia kama sheria zetu zitaendelea kuwa dhaifu kiasi hiki?.
Banjoo kwa vile vyovyote atarudi tena mitaani kuendelea na kazi yake ya wizi na mauaji jambo ambalo lingeweza kuzuilika kama mahakama zetu zingekuwa responsible kuwapa core criminal kama Banjoo adhabu inayostahili.
Huyu Jamaa kama namfahamu alikuwa nimtoto wa mama sana nadhani baba yake alikuwa kibopa na nyumba yao ipo karibu na mahakama kama sikosei ilikuwa na uzio mkubwa wa senyenge na yeye alikuwa akiishi kwenye servant kota akazoeana na wahuni wote wa mtoni.... pengine ndio alijifunza maisha yale