Kirode
JF-Expert Member
- Mar 25, 2011
- 3,566
- 84
Mkuu weka picha yake hapa tumuone mimi mdau mkubwa sana wa madini
aina ya makaa ya mawe na sio tanzanite......
Mkuu weka picha yake hapa tumuone mimi mdau mkubwa sana wa madini
unamjua huyo jamaa? aisee inabidi tukae meza moja tunywe bia ngongo, halafu banjoo mwenyewe siku hizi joka la kibisa tu, hajitokezi mjini, "Anless pub" ndio bar yake kubwa, mle ndani si unajua palivyo?
Acha urongo, zenii ni mdebwedo full
mtaishia kumwagia tindikali mapadre na vischana vya kizungu tu
cowards
Hapo kwenye red nikukosoe kidogo.
Banjoo ana vinyumba kadhaa vya kupanga, pia kazi yake bado ni ujambazi(anatumia manyoka yeye binafsi hazmi front sana) na kazi nyingine anayofanya ni kuwauza majambazi kwa polisi.
Inshort za kubadilisha mboga zipo.
Mkuu Mwana Kwetu
Banjoo si hatari kihivyo,huyu hana vigezo vya majambazi yaliyosifika kwa uwezo mkubwa wa kupanga mipango ya kijambazi.Kifupi huyu ni mtu wa kutumwa na kutumiwa huwezi kumweka kundi moja na akina Marehemu Juma Kipisi au mfungwa wa maisha Sadiki Mkindi.
Matukio ya ujambazi wa Banjoo mengi ni ya kutumwa si mipango yake mwenyewe.Hakuna ujambazi uliowahi kufanywa na Banjoo ukasema kweli huyu jamaa ni kichwaa sana sana anatumiwa fedha nyingi zinaingia anakatiwa kiasi cha mboga anachapa mwendo sasa huyu kamwe hawezi kuwekwa katika kundi la majambazi sugu ni kumkweza kwa sifa asizokuwa nazo.Mimi namwona kama mshamba fulani asiyekuwa na uwezo wa kusoma alama za nyakati.[/QUOTE
Duh, Mkuu Ngongo yaani apo umepiga goli la kisigino. Enzi za Sadiki Mkindi ilikuwa balaa. Akiingia Baa, yaani kila mtu anachomokea mlango wa uani. Huyu jama alikuwa Nuksi sana. Afadhali aendelee kukaa huko aliko. Hafai hata kidogo kuishi uraiani.
Mkuu paradiso ha ha ha ha yaani virooms na deals alizopiga za mamilioni is there any corelation ?.Hizo project alizonazo hata wale wadada wanaofanyakazi A to Z mbona wanazo.Jambazi anayeshirikiana na polisi kuchakachua vijisenti angekuwa na zile nyumba zenye hadhi ya kukaa wafanyakazi wa UNICTR ungesemaje ?.
Ngongo & paradiso
Kwa kweli weekend hii ningewapata mlipo ningewapatia chochote kile mnachotumia.
Nasema hivyo kwa sababu ya kuwa makini na yote haya mliyopost katika thread hii. Huyu Banjoo nakwambia siyo kwamba ni mbabe Mi naweza kusema ni mpumba.vu tu kwani hata elimu yenyewe nafikiri ni ya darasa la tano tu ila kinachomsaidia ni uwenyeji tu ila nawaambia siku huyu Mungu mwenye uwezo wa yote akisema no mambo yake huyu yatakua mwisho.
Ngongo paradiso
Kuna huyu mwingine anayeishi hapo Ngarenaro corner maarufu kwa kuitwa Jumanne Mjusi naye namsikia ni soo very danger na ana group lake la vijana ambayo ndiyo sasa hivi anataka kunyanyua kichwa hapa jijini. Habari yake mnaisikiaje? Maana Mi naona hata akipelekwa gerezani leo kesho unamwona mtaani tu.
Nyamayao
Marehemu Baby alikuwa ni binti mwenye sura nzuri ambaye kila mwanaume mwenye mafanikio angetamani awe mke wake,bahati mbaya akaangukia mikononi mwa jambazi sugu Sadiki Mkindi.Wakati huo Sadiki Mkindi alikuwa amerejea nchi baada ya kufungwa na kufukuzwa nchini Sweden kwa makosa ya kumjeruhi vibaya sana mke wake raia wa Sweden pia aliwahi kuhukumiwa kwa makosa ya kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.
Kabla ya kwenda Sweden tayari alikuwa na sifa za kuhusika katika matukio kadhaa ya ujambazi yaliyoambatana na mauaji ya kutisha.Kuna tukio moja Sadiki akishirikana na majambazi wenzie Marehemu Alididi,Juma Kipisi na jambazi mwingine jina limenitoka walivamia nyumba ya mzungu mmoja maeneo ya USA RIVER nje kidogo ya mji wa Arusha waliba vitu vya thamani kubwa na kummiminia risasi Baba,Mama na watoto.
Kwanini mkono wa sheria ulichelewa sana kumfikia Sadiki Mkindi,Ukoo wa Mkindi enzi hizo ulikuwa maarufu na tajiri sana Arusha.Ilikuwa ni vigumu sana kwa maRPCs wa enzi hizo kuigusa familia hii waanzilishi wa mji wa Arusha.Majina ya maeneo mengi ya mji wa Arusha kama Kaloleni yalitolewa na familia hii.Kiwanja cha Msikiti wa Bondeni kilitolewa na familia ya Mkindi ndiyo maana mpaka leo mapato na uendeshaji wa msikiti umebakia kama mali ya familia ya Mkindi.
Kabla Sadiki Mkindi hajakutana na Marehemu Baby Makange aliishi na binti mmoja matata akikaa mitaa ya Kaloleni,baada ya muda wa kama miaka miwili binti wa watu alikuwa hatazamiki kwa mikiki ya Sadiki na matumizi ya unga.Alipoachwa Baby akaingia kwenye himaya ya Sadiki Mkindi kila mtu alimkanya hakusikia mtoto wa watu.
Mauaji ya Baby yalisababishwa na wivu aliokuwa nao Sadiki baada ya kutoka jela alimtuhumu Baby alikuwa akitembea na wanaume wengine akamwangishia kipigo cha nguvu kilichosababisha kuvunjika shingo na mbavu.Baada ya mauaji Sadiki akaendelea kukaa na maiti hadi ikaanza kuharibika.Si kwamba alikuwa hafanyi juhudi za kujivua msala hapana alijaribu mara kadhaa kutaka kuuzika mwili wa marehemu Baby bila mafaniko.Mpango wa mwisho uli hivi,alikodi taxi hadi Mt Meru Hospital akauwacha mwili ndini ya taxi akakimbilia mapokezi kuomba msaada wa wheel chair wauguzi bila kufanya ajizi wakaingia mkenge wakachukua mwili wa marehemu wakidhani ni mgonjwa aliyezidiwa wakati wanaendelea na mikikimiki ya kumwngiza mgojwa kwa daktari Sadiki akasepa zake akawaachia msala wakati daktarai anamkagua mgonjwa akagundua ni marehemu alishakufa zaidi ya wiki moja iliyopita.
Heshima yako mkuu Ngongo! Hakika wewe unaijuwa vizuri sana hii familia. Yaani hapa kama nauona ukoo mzima wa Mkindi na umaarufu wao.
Dada inamaana mji (Jiji)wa Arusha huujui? hauna mwenyewe RPC ukiwa mkali maandamano, RC au DC ukikemea wanakuja juu Machalii (Bilionea wetu mara junk wetu wanamuonea wivu na utajiri wa madini)
Mimi nilitembele gereza la Isanga nikamkuta huyo Nyari ni balaa matumizi ndani ya Gereza na alituhakikishia Mji wa Arusha kaushika na atatoka tu, kweli leo anawatoa na wahalifu wenzake.
Huku kwetu watu km hao ni kuchinjiliwa mbali kumbukua enzi za zelothe
sasa hivi kwesha habari, watoto wana kula unga kama chakula vile.
aina ya makaa ya mawe na sio tanzanite......
Mkuu Jumanne Mjusi ni kuku mdogo sana.
Huyu ni mwizi wa kuvunja mastore na magodown kwa vikundi vya kujikusanya kutoka mitaa kadhaa na alijisalimisha bungeni miaka ile nakusamehewa.
Sasa hivi ni green guard na ndiye aliempiga shoka la bega kamanda wa chadema maeneo ya Elerai kwenye uchaguzi mdogo wa kata 4.
Jumanne mjusi kwa sasa anatumiwa na CCM kuleta fujo hasa maeneo ya soko la ngarenaro ila diwani wa Levolosi Ephata Nanyaro amefanikiwa kumtimua hapo.
Huyu dogo ana roho ngumu na sura mbaya tu lakini hana akiili ya umafia , anatumia nguvu zaidi na hirizi kwa sana tukiamua hata sasa hivi tunamuua kama kuku bila hata kutumia risasi.
Jambazi anatembea na pikpik wakati nimajifunza shabaha kwa miaka 3??
Zelothe Stephano ameshastaafu hapahapa Dodoma baada ya kazi kubwa ya kuusafisha Mji huu, ingawa alifiwa na mtoto wa ke aliyekuwa akisoma UDOM, alianza kunyong'onyea akipunguza makali kwa wale tena majambazi na matapeli hasa ya Viwanja vya CDA, Tunaye Misile naona anakomaa nao.Hapo ndipo nashangaa. Zeloth ni askari hodari na mwenyeji wa Arusha. Kwa nini asipewe huu mji aunyooshe? Mara Dodoma, mara Mtwara. Sielewi hata kidogo.