Jambazi Sugu "BANJOO" larudi uraiani

Jambazi Sugu "BANJOO" larudi uraiani

Mkuu nduu/mamaya baada ya hapo ilibidi daktari wa zamu akishirikiana na uongozi wa hospital utoe taarifa polisi kwaajili ya uchunguzi.

Marehemu Major Makange Baba wa marehemu mtaalamu wa mizinga aliyesomea India na kushiriki kikamilifu katika operesheni ya kug'oa utawala wa Idd Amin wa Uganda na kwa wakati fulani akitumika katika jeshi la Uganda chini ya utawala wa Musevenii alikuwa mtu wa mwanzo kufika Mt Meru Hospital kushuhudia mwili wa Baby ukiingizwa chuma cha kuhifadhi maiti.Bila kuchelewa aliwaambia polisi mwanangu atakuwa ameuwawa na Sadiki Mkindi na lazima angelipa kisasi kwa kuapa kwamba Baby angekuwa mtu wa mwisho kuuwawa na Sadiki Mkindi.

Uchunguzi wa polisi ulianza mara moja kwa kuvamia makazi rasmi ya Sadiki kwaajili ya upekuzi na mahojianao ya majirani ambao walikiri kusikia vishindo na makelele ya malalamiko ya Marehemu Baby lakini hakuna jirani aliyethubutu kutoa msaada kwa marehemu kutokana na kuogopa ukatili wa Sadiki.Majirani waliendelea kufunguka zaidi walishangaa nyumba ya Sadiki ilikuwa na utulivu mkubwa wa zaidi ya wiki moja kitu ambacho si cha kawaida.Katika upekuzi polisi walifanikiwa kukuta nguo za marehemu zilizojaa damu nyingi sana hali iliyoashiria kwamba marehemu kabla hajapelekwa hospital alibadilishwa nguo ili kuwaadaa madaktari,wauguzi na dereva taxi wasigundue au wasihisi kitu chochote.

Msako wa kumtafuta Sadiki Mkindi ukaanza mara moja,iliwachukua polisi wiki kadhaa kumnasa Sadiki Mkindi Jiji Dar es Salaam na kumrejesha Arusha kwajili ya kumfungulia mashtaka ya kuuwa kwa kukusudia.Ukoo wa mkindi ambao tayari ulikuwa unanuka kwa maovu mbali mbali haukuwa na nafasi ya ushawishi tena juu ya yote mtu pekee alibaki na ushawishi alikuwa marehemu Brigedia Mkindi wakati akihudumu ofisi ya mkuu wa mkoa kama mshauri wa mgambo wa mkoa.

Kesi ilianza kunguruma mahakama kuu Jiji Arusha,Mashahidi muhimu walikuwa mlinzi wa Hospital ya Mt Meru ambae alikuwa akimfahamu vizuri Sadiki Mkindi kutokana na kulazwa kwa muda mrefu Hospatal ya Mt Meru akisumbuliwa na TB aliyoipata wakati akitumikia kifungo gereza la mkoa wa Arusha kwa makosa mengine ya mauaji.Daktari aliyeufanyia mwili wa marehemu uchunguzi pia alitoa ushahidi uliomtia hatiani Sadiki Mkindi na kuhukumiwa kunyongwa na mahakama kuu na baadae mahakama ya rufaa ilikubaliana na hukumu ya mahakama kuu ingawa mpaka leo bado hajanyongwa na hadhabu yake imekuwa kifungo cha maisha huku mwenyezi Mungu akimtandika kwa ugonjwa wa kupooza upande mmoja wa mwili.

Hawa ndiyo unaweza kusema walikuwa majambazi wa kutisha kwasababu kwanza walikuwa wameende shule,wakati mwingi walikuwa wanasoma vitabu mbali mbali kwaajili ya kuongeza ujuzi.walikuwa wakiangalia picha za kimafia ambazo pia zilikuwa kuwasaidia katika operesheni za ujambazi.Sadiki Mkindi mara kadhaa alikuwa akijitetea mwenyewe mahakamani mara anapobaini mwanasheria wake anashindwa kufikia kiwango anachokitaka isitoshe alikuwa na exposure ya kuishi Ulaya na kufanyabiasha kwa kipindi kirefu.Ukimweka Banjoo katika level ya Sadiki Mkindi ambae hata maafisa magereza wanakwambia ni mtu hatari asiyetakiwa kupewa nafasi hata kidogo ni kujinyima ufahamu wa mambo kwa kujitakia.Sadiki Mkindi ni jambazi anayefanya ujambazi kwakuwa ni sehemu ya maisha yake aliiba wakati alikuwa ameachiwa urithi wa nyumba nyingi katikati ya mji nadhani unafahamu thamani ya viwanja vya mjini ni shilingi ngapi,kodi za vyumba vya mjini ni shilingi ngapi......Banjoo ni kajambazi kwaajili ya kuganga njaa hana kitu hapa mjini,hana elimu,hana biashara,hana kazi hana analoweza kufanya kwa sasa hana network amebaki akijificha jificha kwenye vigrosaries na kuomba omba bia za wanaume wa mujini.
shukrani sana mkuu kwa kutiririka vya kutosha.:becky:
 
niukweli usiopingika kwamba serikali yetu inalea wezi.

kundi la "wachaga wezi" linajulikana toka enzi za MAHITA lkn linavumiliwa na kuendekezwa tuuu na serikali sijui wana guts zipi

Serikali yenyewe imejaa wezi
 
Zelothe Stephano ameshastaafu hapahapa Dodoma baada ya kazi kubwa ya kuusafisha Mji huu, ingawa alifiwa na mtoto wa ke aliyekuwa akisoma UDOM, alianza kunyong'onyea akipunguza makali kwa wale tena majambazi na matapeli hasa ya Viwanja vya CDA, Tunaye Misile naona anakomaa nao.
Ila kwa Arusha hao kina Nyari watafutiwe Dawa kwani mauaji ya Wafanyabiashara wa Madini ndio wanahusika sana (kuna Story ya Wodini walikolazwa huko babati walisikika akisema kuwa Msuya lazima auawe na watu wakasikia)
Mpaka leo wanatafuta Ushahidi ni nani atajitokeza na huyo Banjoo kaja?
Poleni Arusha Mji wa kidemokrasia kubalini ubabe uingie

Mkuu Ukwaju, nilisikitika sana nilipopata taarifa za msiba wa yule dogo. Hosuasani niliposikia kwamba amekunywa sumu. Kwa mzazi yeyote, kumzika mwanao, tena ghalfla huwa ni huzuni kubwa sana. Sasa hivi nasikia kapelekwa Mtwara kuwa RPC. Kwa nini asipelekwe Arusha ili ausafishe ule mji huku akijitayarisha kuvua uniform jumlajumla?
 
huyo kama ataendelea na wizi atakutana na mziki wa askali mmoja hapo arusha ambaye ameusafiaha sana mji wa arusha kwa kuwapiga majambazi risasi anaitwa msauzi nasikia jamaa ni noma kichizi.
 
unamjua huyo jamaa? aisee inabidi tukae meza moja tunywe bia ngongo, halafu banjoo mwenyewe siku hizi joka la kibisa tu, hajitokezi mjini, "Anless pub" ndio bar yake kubwa, mle ndani si unajua palivyo?
kumbe banjoo mnayemsema ni huyo wa unless Pub?mbona nina namba zake za simu!
 
Duh Nyamayao hivi kweli unaweza kudai wewe ni mwenyeji wa Arusha bila kufahamu mavitu ya Sadiki Mkindi ?.Sadiki Mkindi ni balaa nyingine ila siwezi kumsamehee hata siku moja kwa kutoa uhai wa Baby mtoto wa marehemu Major Makange.Nitafute Jmosi aise nitakuwa East Africa Hotel naangalia ligi ya UK.

Baby yule alikuwa anakaa Kaloleni......? Kumbe huyo jamaa ndio alimuua......?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mwana Kwetu

Banjoo si hatari kihivyo,huyu hana vigezo vya majambazi yaliyosifika kwa uwezo mkubwa wa kupanga mipango ya kijambazi.Kifupi huyu ni mtu wa kutumwa na kutumiwa huwezi kumweka kundi moja na akina Marehemu Juma Kipisi au mfungwa wa maisha Sadiki Mkindi.

Matukio ya ujambazi wa Banjoo mengi ni ya kutumwa si mipango yake mwenyewe.Hakuna ujambazi uliowahi kufanywa na Banjoo ukasema kweli huyu jamaa ni kichwaa sana sana anatumiwa fedha nyingi zinaingia anakatiwa kiasi cha mboga anachapa mwendo sasa huyu kamwe hawezi kuwekwa katika kundi la majambazi sugu ni kumkweza kwa sifa asizokuwa nazo.Mimi namwona kama mshamba fulani asiyekuwa na uwezo wa kusoma alama za nyakati.

Najaribu kusoma hizi post........na thread yenyewe ilivyojaa woga......na nikimwangalia Banjoo mwenyewe......nashindwa kupata uwiano kabisa........
 
Last edited by a moderator:
Zelothe Stephano ameshastaafu hapahapa Dodoma baada ya kazi kubwa ya kuusafisha Mji huu, ingawa alifiwa na mtoto wa ke aliyekuwa akisoma UDOM, alianza kunyong'onyea akipunguza makali kwa wale tena majambazi na matapeli hasa ya Viwanja vya CDA, Tunaye Misile naona anakomaa nao.
Ila kwa Arusha hao kina Nyari watafutiwe Dawa kwani mauaji ya Wafanyabiashara wa Madini ndio wanahusika sana (kuna Story ya Wodini walikolazwa huko babati walisikika akisema kuwa Msuya lazima auawe na watu wakasikia)
Mpaka leo wanatafuta Ushahidi ni nani atajitokeza na huyo Banjoo kaja?
Poleni Arusha Mji wa kidemokrasia kubalini ubabe uingie
Nasikia huyu kamanda Misile ndio next IGP
 
Najaribu kusoma hizi post........na thread yenyewe ilivyojaa woga......na nikimwangalia Banjoo mwenyewe......nashindwa kupata uwiano kabisa........
hata mimi nashindwa kuoanisha!hivi wanamuongelea banjoo aka elvis au ?
 
Mi niko Zanzibar nakula tizi la kumwaga tindikali ya uso, nikirudi Arusha majambazi wote watanikoma.
 
Banjoo mbona alitoka kitambo sana,
ana nyumba za kupangisha, anashinda kwenye bar wanazokaa polisi hasa maeneo ya kijenge na moshono.
anapiga watu na kuwahi polisi na kusubiri ukireport mnamalizana kwa makofi hapo mbele ya polisi ila ukiwa mjanja unalipwa hela ya usumbufu.
inasemekana anatumiwa na polisi kuvujisha siri za majambazi na matukio yao kama anavyofanya jambazi mstaafu kwa jina Mojaa ambaye pia ni rafiki wa uyo Banjoo mara ya mwisho walikua pamoja Blue House Fire Sinoni.

Hakuna polisi mkubwa mwenye uwezo wa kumuua Banjo labda askari wa chini sana au raiya wa mtaa aliyechafukwa sana.

Iweee.......Mojaa kastaafu lini.......? bahati mbaya hii ID ya Preta sio ya siri sana........ ngoja nije na nyingine nijibu hii post.........
 
Najaribu kusoma hizi post........na thread yenyewe ilivyojaa woga......na nikimwangalia Banjoo mwenyewe......nashindwa kupata uwiano kabisa........
Waambie waje Dar tuwafundishe jinsi tulivyoliteketeza kundi la Commando Yosso.
 
ndo ushangae sasa, ila habari ndo ivyo.
kama mtu anapata billion 1 alafu hajabarikiwa kuwa mipango anaishia kumiliki room 1 na gari moja na nina ona kawaida sana.
Kweli kaka. Nimewaona wengi na nawafahamu,hadi leo wanapiga deal mpaka za bank lakini nyumba 1 isiyokuwa na ramani na gari ya kazi kila siku gerage tena ya mkopo. Na mtaani wanaogopeka sana. Halafu ni wakarimu sana,na ni watu wa kusikitika na kusononeka pale unapomweleza jambo la huzuni.
 
Vipi na yule jombaa mwenye 7eleven maeneo ya stand. Chonjo naye kapotelea wapi?
 
Jamani, mbona mna mashaka hivo? Sasa hivi atakuwa ameshakuwa mtu mwema...
 
Back
Top Bottom