Jambo gani la kijinga ulikuwa unatamani litokee ukiwa mtoto?

Jambo gani la kijinga ulikuwa unatamani litokee ukiwa mtoto?

Nilikuwaga nawaza Arnod ndio angekuwa baba angu, ningekuwa nawatiaje makonzi watoto mtaani. Mi mgomvi kitambo
 
Nilikuwa napenda kusikia kesho sikukuu hatuendi shule au mwanafunzi mwenzetu kafariki au kafiwa,sasa ile walimu kusema Leo rudini nyumbani,nilikuwa nafurahi sana
Kwa hiyo ulikuwa husikitiki mtu akifariki we unafurahia tu kurudi nyumbani[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa hiyo ulikuwa husikitiki mtu akifariki we unafurahia tu kurudi nyumbani[emoji23][emoji23][emoji23]
Naam,saa mbili tu,mpo home,burudani sana,ila baada ya kufika darasa flani,mwalimu wangu wa sayansi alitutoka,niliumia zaidi ya ndugu zake,pia mwaka unaofata classmate alitutoka kwa kugongwa na nyoka,iliniuma mno yule msichana.
 
Nilikuwa natamani niote matiti
Nilikuwa natamani niwe mkubwa,niliona kama wanafaidi sana kumbe kawaida tu
Nilikuwa nawatamani makomandoo wa kwenye movie ndio wawe bwana zangu wanioe,mfano sunil shet,salman khan, Jason sta,Dolf Lundgren ndio maana mpaka leo mwanaume awe hana mwili wa mazoezi hata kidogo hapana kabisa,awe na mwili umejaa jaa kama dolf ndio roho yangu inafurahii na kutulia tuliii
 
Mmmmh hapo kwenye kuota matiti sasa
 
Niliwahi kutamani mwalimu afariki, ili asinichape kesho yake

Aise hakuna mtoto ambae hatamani kuwa mkubwa.
 
Nilikuwa natamani nikiwa mkubwa nije kumnaniliu demu wa jirani, sasa baada ya kukua na yule demu kaja kuzeeka kupitiliza yaani hata sina tena mzuka naye mpaka najishangaa nilikuwa nawazaga nini juu yake.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wala humtamani tenaa
 
Me furaha yangu ilikuwa nisiende shule tuu ..ukitokea msiba au mwl anaumwa mie burudaniiiii
 
We baba ako alikuwa mkatili
Siwezi kumlaumu aisee, mungu ambariki sana mshua... mi nlikua na fujo za kufa mtu... Nshampiga mwalimu na manati ya kichwa pindi nipo darasa la pili, na kuna siku nlitumwa nikanunue vitumbua asubuhi nikaanza mchezo mchezo nikamwaga hot-pot zima la vitumbua...... ishu ilikua kurudi home, njia nzima ni kumwomba mungu ashushe kiama muda huo huo
 
Kwani ticha ulimpiga makusudi?
 
Back
Top Bottom