Jambo gani ulishalifanya likakupa aibu ambayo hautaisahau?

Heh, yeshakuwa hayo? Kwani haukumuambia ulinipenda kabla yake? Haya nirushie laki 2 ya taxi, chipsi funga na kinywaji.
Haahahaaaa akikufukuza nenda Bilikanaz leo ni ladies free hahahaaa kwangu najishaua leo Amyner wangu yupo
 
Last edited by a moderator:
Lilikua gari busy nini?
 
Unajua kuna tukio ukilikumbuka unapata ile embarrassment kabisa hapo hapo, unakunja hata sura. Afu watu wanauliza vipi unakosa jibu.
Heheheheeee mnanifanya na mimi nicheke mwenyewe hapa coz naliona tukio kichwani lol
 

Hahahahaaaa mamaaa wa Air Polution
Copy kwa Paw
 
Last edited by a moderator:

hahahaha 'ze wind'
 
mi nakumbuka nilipokuwa msichana mbichi kuna vibrazamen vilikuwa vinakaaga kona fulani mtaani, kila nikipita they sing praises mi bichwa hiloo sasa si kujipitisha uko.
Sasa kuna kipindi mvua ilinyesha na kuacha madimbwi ya maji, wenye maarifa yao wakawa wanaweka vitofali watu wakanyagie. Siku hiyo mwenyewe na madoido yangu napita kona ya wale mabishololo nikakutana na dimbwi la maji nikakanyaga kitofali cha kwanza cha pili yarabi tobaa! kumbe kuna wahuni wametegesha kipande cha kigodoro, niliingia dimbwini mzima mzima......niliwasikia wale mabishoo wakicheka, si aibu hiyo! sikugeuka nyuma na pozi lote lilikata
Nikabadilishaga na njia
 
Hahahahahahahahaahahahaaha

 
Hahahaaaaaaaaa aiseeee dah we walikukamata aisee dah
Btw mzima?
Miss you
 

Hahahahaa aibu ya karne hahaa pole sana
 
Samahani sana Lizzy kumbe ulikua ni wewe, dah...nawe ulikua waringa sana hata tukikusalimu unakausha.

 
"My mom and dad are very religious.
At night I hear them scream "Jesus"! "


Hayo ni maneno yaliyomtoka binti yangu siku tupo mezani wakati wa "dinner" ya familia, baada ya uncle kumwomba aseme neno lolote kumhusu baba na mama.
Mwanaume kichwa chini unaambiwa !!!
 
Ni zaman lkn nakumbuka nilichomwa sindano ya crystapen na nurse mmoja hiv nilijikojolea hapo hapo daaah!! Baada ya hapo nurse alinipa karanga kujipoozea.
 

Hahahahaha, umenikumbusha kwenye vogue yangu nyeusi.
Kama ni kuua anza na mie. Tehe tehe .
 
Ni zaman lkn nakumbuka nilichomwa sindano ya crystapen na nurse mmoja hiv nilijikojolea hapo hapo daaah!! Baada ya hapo nurse alinipa karanga kujipoozea.

Hii kitu crystapen sitaki hata kuisikia yani. . .dah. . .
 
Nilipokosa penalt katika mpira wa miguu,ambayo ingeipa timu yangu ushindi uwanja wa ushirika moshi,wakati huo tulikuwa tuna ahadi nono kama tungeshinda
 
Siku ambayo nilipata aibu ni Pale Nilipoenda kutembelea Ukweni, Bunda-Mwanza
Mida ya Jioni nikatolewa Out na Mchumba, Nilipiga Maji kisawasawa, Mida ya Night nikaenda zangu kulala kwenye chumba nilichotayarishiwa
(sikutaka kulala na mchumba Ukweni).
Night kali mkojo ukanibana,nikatoka zangu mpaka chooni, mida ya kurudi chumbani si nikasahau chumba nikaingia chumbani kwaBaba Mkwe (Mke alienda kwao) nikajitupa kitandani na kuuchapa usingizi.
Kulipopambazuka ile nafumbua jicho tu nakutana na kundi la Mawifi, Mama mkwe mdogo, Mchumba na Wajomba zao, kujipapasa hv kumbe niko chumbani kwa Baba Mkwe.
Unadhani nini kilifuatia....................Changamsha Ubongo wako.
Ila nikilikumbuka lile tukio,Afanaleki.......!!!!!!!
Maana huyo aliyewahi kuwa mchumba wangu aliwahi kuja field kazini kwetu, nilionaje aibu thatha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…