Jambo gani ulishalifanya likakupa aibu ambayo hautaisahau?

Jambo gani ulishalifanya likakupa aibu ambayo hautaisahau?

Mi kuna siku bwana nimebaki ndani ya gari ya mtu, akashuka kuchukua chipsi funga. Nikamuambia nnataka kubreak ze wind mi nabaki garini. Full kipupwe, afu tinted ya maana. Tukawa tumeblock gari, nikawaona jamaa wanahangaika nikahamia kwa driver ili nilisogeze. Jamaa wakanigongea kioo kwa abiria nikashusha kioo. Dah, harufu ya ze wind hapo na kumbe ni mshkaji namjua. Yaani hatujawahi kuiongelea hiyo embarrassment manake dah! Im sure mshkaji aliskia harufu yaani. Na sijui why sikushusha kioo kwanza harufu ikatoka. Mtu akinitania about this ntaua aisee.

he he he hii kali.....pole!

mi nakumbuka nilipokuwa msichana mbichi kuna vibrazamen vilikuwa vinakaaga kona fulani mtaani, kila nikipita they sing praises mi bichwa hiloo sasa si kujipitisha uko.
Sasa kuna kipindi mvua ilinyesha na kuacha madimbwi ya maji, wenye maarifa yao wakawa wanaweka vitofali watu wakanyagie. Siku hiyo mwenyewe na madoido yangu napita kona ya wale mabishololo nikakutana na dimbwi la maji nikakanyaga kitofali cha kwanza cha pili yarabi tobaa! kumbe kuna wahuni wametegesha kipande cha kigodoro, niliingia dimbwini mzima mzima......niliwasikia wale mabishoo wakicheka, si aibu hiyo! sikugeuka nyuma na pozi lote lilikata
Nikabadilishaga na njia

ha ha ha aibu yangu ni ndogo sana kwa hii!pole
 
Gari busy ndo nini na wewe? Afu si ulisifiwa umeokoka wewe?

afu wewe una kiherehere, nilishasema staki huu utani. Aisee sijawahi kuhadithia mtu na huyu mshkaji ni mshkaji damdam yaani. Na hajawahi nitania!

hivi unajua siwezi hata kulitamka hilo tendo kwa.kiswahili. Haya maadili ya Mtambuzi yananitesa! Afu ze wind yenyewe ilikuwa kama kimbunga ivan!

unanisingizia mie mpoleeee. Sina hata vituko.

Jamani unarudisha nyuma juhudi za NEMC
 
Last edited by a moderator:
Kwa kweli sina tukio la aibu.. Ngoja nisome tu vituko vya watu...
 
Nilipokosa penalt katika
mpira wa miguu,ambayo ingeipa timu yangu ushindi uwanja wa ushirika
moshi,wakati huo tulikuwa tuna ahadi nono kama tungeshinda

Hujui kulenga!
 
Hii ndo kubwa kuliko
yani aibu ya maisha......
nlikuwa mdogo kama 6 yrs hivi, nimetumwa shop kupita mtaa wa pili
nikakuta kitoto kinacheza cha kike kidogo zaidi yangu enzi hizo mi
nikimuona mtoto lazma nimchokoze sijui pepo! nikakiambia kile kitoto "we
ntakugegeda" bila hata tafsida!!! kile kitoto kikapiga kelele mamaaa
huyu anataka kunigegeda, maza akatoka nje na dada mtu....ikabidi nitoke
nduki niko peku gauni linapepea tu kumbe wakanijua aggggrrrrr! muda si
mrefu wakahama mtaa huo nikajua aibu imeisha kumbe ndo inaanza....
Yule dada mtu akaja kusoma primary school nilokuwa nasoma nilikuwa
nakosa raha kila nikimuona make alikuwa ananiangalia, nilivomaliza
nikafurahi heee kwenda o'level yule dada huyu hapa agggrrr, nikafurahi
tena nlivomaliza pia na A'level hatukusoma wote nikajisemea ehuu
afadhali....niko zangu chuo mwaka wa 2 huyo dada huyu hapa afu it seems
na yeye anakumbuka!!!

Yani nikikumbuka hili natamani siku zirudi nyuma nisitamke
nilichomwambia huyo dogo aaah!!!!!!!!!sitasahau!

Utoto kazi! Yaani unatamani ku undo... Pole mwaya.
 
Na wewe! Yaani unaenda kupiga maji ugenini? Duh, sikuwez. Pole sana, na hao jamaa wazinzi sana seems, wanaogopa wakwe kama ukoma. Hata kupita mbele ya baba mkwe hairuhusiwi.

Huu ni mjadala mpya lakini mila za kwetu haungelala kwao kijana. Ungelazwa kwa jirani ama ndugu mwingine. Na hata kukiwa na msiba Paw hawezi kulala kwa babangu, analala kwa kaka. Kiasi kwamba kituko kama hicho hakina impact.

Unafikiri, yaani ni ubishi wangu tu, maana niliambiwa kbs kuwa tutafute gesti mitaa ya Bunda stendi mimi nikamkatalia,
Maana nilitaka wakwe zangu na mawifi wanione jinsi nilivyo na Adabu (mambo ya kupalilia ndoa)
Matokeo yake, yamekuwa kinyume, na aibu shuuuuuuu..... King'asti, acha tuu yaani sitakaa nisahau lile tukio.
 
Last edited by a moderator:
Mmmh kweli hii aibu, mchumba alielewa umekosea mlango kweli?
he he he nadhani asubuhi ulifungasha vyako!!!!!!

We Evelyn Salt Unafikiri hapo kuna kusubiria mchana ufike, thubutuuuuuu....
Saa 3 ileile tu, Nnshaaaaaa.........stendi
Mpaka mchuchu nikamuacha kwenye mataa, fanya mchezo na Nusu fumanizi nini...........!!!!!!!
Na ujanja wangu wote huu wa Mjini, nilibaki mdogo kama kifungo.
 
Last edited by a moderator:
Shhhhhhhh! Na wewe hauna siri? Afu uliporudi ukakausha si nikajiona mshindi. Nikajua haujasniff, lol.

Nianzie wapi. . .mf! Uliniachaje hoi. . .kumbe na wewe hua unafanyaga hivyo. . Binti mzuri vile nikawa najiwazia zangu, nikaongeza nguvu ya AC. . .halafu hata huku-notice nilivyo ongeza na nguvu ya perfume.
 
We Evelyn Salt Unafikiri hapo kuna kusubiria mchana ufike, thubutuuuuuu....
Saa 3 ileile tu, Nnshaaaaaa.........stendi
Mpaka mchuchu nikamuacha kwenye mataa, fanya mchezo na Nusu fumanizi nini...........!!!!!!!
Na ujanja wangu wote huu wa Mjini, nilibaki mdogo kama kifungo.

he he he ni matumaini yangu hukumpapasa ba mkwe!!!!!!!
 
Kura yangu ya 2005 nilimpa JK sababu ya haiba yake. Hili limenitia aibu
 
Mmmh TANMO ina maana ulikuwa chekechea! Duuuuuuh!
Karibu white party!

Nakumbuka kufumaniwa redi hendedi na Maza nikimgegeda Hausi Gelo, Wacha nipewe mawaidha kuhusu Ukimwi wakati huo hata la kwanza sijaanza, nikawa naona maza ananiletea Rege tu na stori zake za Ukimwi ambao wakati huo hata nilikuwa sielewi ni kitu gani..
 
Last edited by a moderator:
Hahahahahahahahahahaha

Siku ambayo nilipata aibu ni Pale Nilipoenda kutembelea Ukweni, Bunda-Mwanza
Mida ya Jioni nikatolewa Out na Mchumba, Nilipiga Maji kisawasawa, Mida ya Night nikaenda zangu kulala kwenye chumba nilichotayarishiwa
(sikutaka kulala na mchumba Ukweni).
Night kali mkojo ukanibana,nikatoka zangu mpaka chooni, mida ya kurudi chumbani si nikasahau chumba nikaingia chumbani kwaBaba Mkwe (Mke alienda kwao) nikajitupa kitandani na kuuchapa usingizi.
Kulipopambazuka ile nafumbua jicho tu nakutana na kundi la Mawifi, Mama mkwe mdogo, Mchumba na Wajomba zao, kujipapasa hv kumbe niko chumbani kwa Baba Mkwe.
Unadhani nini kilifuatia....................Changamsha Ubongo wako.
Ila nikilikumbuka lile tukio,Afanaleki.......!!!!!!!
Maana huyo aliyewahi kuwa mchumba wangu aliwahi kuja field kazini kwetu, nilionaje aibu thatha.
 
Hahahahahahahahahaha

Hahaaaa aisee lol
Mi nililala church siku ya jumatano ya majivu pale St. Joseph tukiwa tunangoja misa ianze coz niliwahi sana nikawa naota...nkaota naanguka lol nilikurupuka kwa speed balaa yan full aibu uzuri nilikuwa nimepakana ma wazee so walijua nimechoka tu.
Baada ya hapo sikulala tena na huwa silali church
 
Nianzie wapi. . .mf! Uliniachaje hoi. . .kumbe na wewe hua unafanyaga hivyo. . Binti mzuri vile nikawa najiwazia zangu, nikaongeza nguvu ya AC. . .halafu hata huku-notice nilivyo ongeza na nguvu ya perfume.
Nimekununia hadi mwakani. Na hela zako staki.:shut-mouth:
 
Hahaaaa aisee lol
Mi nililala church siku ya jumatano ya majivu pale St. Joseph tukiwa tunangoja misa ianze coz niliwahi sana nikawa naota...nkaota naanguka lol nilikurupuka kwa speed balaa yan full aibu uzuri nilikuwa nimepakana ma wazee so walijua nimechoka tu.
Baada ya hapo sikulala tena na huwa silali church
Hahahaah!! Ningekuwa mimi na ibada ingeishia hapo, maana ningetoka na nisirudi.
 
Back
Top Bottom