Katavi
Platinum Member
- Aug 31, 2009
- 42,023
- 12,811
Hahahaah! Jamani mbavu zangu.Kura yangu ya 2005 nilimpa JK sababu ya haiba yake. Hili limenitia aibu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahahaah! Jamani mbavu zangu.Kura yangu ya 2005 nilimpa JK sababu ya haiba yake. Hili limenitia aibu
:majani7:Ladies & Gentlement habari za usiku!!!!!!!
Jamani mie kuna mambo nishayafanya yani aibu zake siwezi kusahau!!!
Miaka ya juzi kati hapa ndo nimejiunga na chuo,jumamosi moja nikaingia zangu mtaani hospitali, nikakutana na mdada mmoja tumekaa kwenye foleni akaona file langu limeandikwa jina la chuo...akaniuliza kumbe unasoma chuo flani?
Mdada wa first year mi ndo mimi nikajibu kwa pozi ndio, unasoma kozi gani? kwa manjonjo zaidi nikadanganya nasoma Bcom marketing mi nimemuona wa kawaida nkajua wa kitaa tu.....
Jumatatu hiyoo nimekaa zangu nasubiri pindi mdada niliekutana nae hospitali huyu hapa akanisalimia kuonesha ananikumbuka tunasoma wote faculty moja Education yani nilihisi aibu isoelezeka nikatamani nipite chini ya viti niishie zangu, siku zote nilizokuwa chuo nilikuwa nakosa amani nikikutana nae nikikumbuka nilivojishaua nasoma Bcom kumbe Education!!!!
Haijaishia hapo.....ila niambie kwanza aibu yako na wewe!!!!!!!
Nikiwa darasa la sita nilimuandikia barua ya kimapenzi dada mmoja wa darasa la tano. Bahati mbaya ikanaswa na mwalimu mkuu, barua ilisomwa mbele ya wanafunzi wa shule nzima na nikaishia kuchapwa bakora sita mbele ya wanafunzi....
Hahahaah! Hiyo ni ajali kazini.lol! imefanana na yangu
darasa la sita mimi na rafiki yangu tukawaandikia barua ya mapenzi mabinti wawili classmate ambao dada yao ni mwalimu hapo hapo shuleni.......wenyewe tumeandika maneno matamu ,kwenye karatasi ya vimaua na bahasha ya vimaua.
kesho yake darasani kila nikimwangalia mtoto anaona aibu na kuchekacheka ,nikajua yes nimeshang'oa mtoto.
tumerudi darasani kutoka kwenye mapumziko ya saa nne ,mara walimu wote ofisini wamehamia darasani lol! kumbe barua walizipeleka kwa dada yao,si ndo kuambiwa tusome mbele ya darasa halafu zile sehemu za maneno ya kimahaba unashadadiwa na walimu kuwa utoe sauti na kurudia tuache kumumunya maneno...baada ya hapo tukala khamsa wa thalatha(viboko).......ilikuwa aibu kweli kweli ,ila baada ya hapo nikawa poa tu tena nikajiona kidume mimi hiyo ajali kazini .....baadae nikamg'oa yule mmojawapo aliyeandikiwa na mwenzangu, ila mpaka leo hata sioni aibu tena,nahisi kama nilionewa tu au ilikuwa ajali kazini
mi nakumbuka nilipokuwa msichana mbichi kuna vibrazamen vilikuwa vinakaaga kona fulani mtaani, kila nikipita they sing praises mi bichwa hiloo sasa si kujipitisha uko.
Sasa kuna kipindi mvua ilinyesha na kuacha madimbwi ya maji, wenye maarifa yao wakawa wanaweka vitofali watu wakanyagie. Siku hiyo mwenyewe na madoido yangu napita kona ya wale mabishololo nikakutana na dimbwi la maji nikakanyaga kitofali cha kwanza cha pili yarabi tobaa! kumbe kuna wahuni wametegesha kipande cha kigodoro, niliingia dimbwini mzima mzima......niliwasikia wale mabishoo wakicheka, si aibu hiyo! sikugeuka nyuma na pozi lote lilikata
Nikabadilishaga na njia
Hii ndo kubwa kuliko yani aibu ya maisha......
nlikuwa mdogo kama 6 yrs hivi, nimetumwa shop kupita mtaa wa pili nikakuta kitoto kinacheza cha kike kidogo zaidi yangu enzi hizo mi nikimuona mtoto lazma nimchokoze sijui pepo! nikakiambia kile kitoto "we ntakugegeda" bila hata tafsida!!! kile kitoto kikapiga kelele mamaaa huyu anataka kunigegeda, maza akatoka nje na dada mtu....ikabidi nitoke nduki niko peku gauni linapepea tu kumbe wakanijua aggggrrrrr! muda si mrefu wakahama mtaa huo nikajua aibu imeisha kumbe ndo inaanza....
Yule dada mtu akaja kusoma primary school nilokuwa nasoma nilikuwa nakosa raha kila nikimuona make alikuwa ananiangalia, nilivomaliza nikafurahi heee kwenda o'level yule dada huyu hapa agggrrr, nikafurahi tena nlivomaliza pia na A'level hatukusoma wote nikajisemea ehuu afadhali....niko zangu chuo mwaka wa 2 huyo dada huyu hapa afu it seems na yeye anakumbuka!!!
Yani nikikumbuka hili natamani siku zirudi nyuma nisitamke nilichomwambia huyo dogo aaah!!!!!!!!!sitasahau!
Jamani unarudisha nyuma juhudi za NEMC
Hamna, kwanza mie ndo nasaidia kubalance gases. Hujui hydrogen sulphide niliyotengeneza ikichanganyika na kabondioksaidi inatengeneza nini?
Kwani wewe ulesbian umeujua yoka kinda! Umedata ujue! Sipayi picha, ungekuwa tu ragiki na huyo dadake aisee.
Aisee mie ninalo nakumbuka miaka mingi iliyopita nilipokua shule nilikuwa na kiherehere sana cha kuuliza maswali hasa nikiwa darasani.Siku moja bwana ikatokea siku moja shule nzima walikusanyika kwa ajili ya kuchagua viongozi na wanafunzi walitakiwa kuwauliza maswali hao wagombea ili kujua ufanisi wao sasa basi nakuambia ilipofika saa ya kuuliza maswali mie wa kwanza kidole juu sikupiontiwa nikakasirika sana,swali la pili mie tena kidole juu angalao mwalimu akaniona akanipoint niulize,nikasimama bwana walikuwa wanafunzi kabao zaidi ya elfu 1 mara swali nililokua nataka kuuliza nikalisahau nikabaki nimeduaa mwisho nika kaa chini bila kuuliza hilo swali watu walinicheka sana niliona aibu ya mwaka mpaka mademu walikuwepo yaani mpaka leo naikumbuka hiyo.
Hahahaah! Jamani mbavu zangu.
nasubiri mmalize nije niwafunike wote..