Siku ambayo nilipata aibu ni Pale Nilipoenda kutembelea Ukweni, Bunda-Mwanza
Mida ya Jioni nikatolewa Out na Mchumba, Nilipiga Maji kisawasawa, Mida ya Night nikaenda zangu kulala kwenye chumba nilichotayarishiwa (sikutaka kulala na mchumba Ukweni).
Night kali mkojo ukanibana,nikatoka zangu mpaka chooni, mida ya kurudi chumbani si nikasahau chumba nikaingia chumbani kwaBaba Mkwe (Mke alienda kwao) nikajitupa kitandani na kuuchapa usingizi.
Kulipopambazuka ile nafumbua jicho tu nakutana na kundi la Mawifi, Mama mkwe mdogo, Mchumba na Wajomba zao, kujipapasa hv kumbe niko chumbani kwa Baba Mkwe.
Unadhani nini kilifuatia....................Changamsha Ubongo wako.
Ila nikilikumbuka lile tukio,Afanaleki.......!!!!!!! Maana huyo aliyewahi kuwa mchumba wangu aliwahi kuja field kazini kwetu, nilionaje aibu thatha.