Wakili wa shetani
JF-Expert Member
- Nov 22, 2022
- 1,726
- 3,391
Huu ni ukweli ambao wengi hawapendi kuusikia, hata Mods humu hawaupendi. CCM ni chama pekee cha siasa ambacho hakiwezi kunyooshewa kidole cha udini. CUF ilikuwa na nguvu sana, lakini kila mtu aliona kupitia safu yake ya juu kilivyoegemea dini fulani. CDM kilikuwa na nguvu, na hata leo kina nguvu lakini kupitia safu ya uongozi wake watu wanaona wazi kina muelekeo wa dini fulani. ACT wazalendo ni kama CUF B, kila mtu anaona muelekeo wake wa kidini.
Chama chochote cha siasa kinachotaka kufanikiwa nchi hii kinatakiwa kwanza kibalance suala la dini ndani yake kwa dhati kabisa.
Lazima watu wakiangalia picha ya uongozi wa juu washindwe kunyoosha kidole cha udini.
Hizi siasa za kiongozi wa upinzani anakaa madarakani miaka kumi, ishirini- watu wanaona kama ni mtu au watu wa dini fulani tu ndiyo wapo kwenye hicho chama.
Chama chochote kipya kinachokuja lazima kiliangalie suala hili kwa makini sana, vinginevyo kitafeli hata kabla yua kuanza.