Jambo likitangazwa na Waziri, Jeshi la Polisi linaweza kutengua?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,982
Reaction score
51,157
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi ambaye ndiye waziri anayesimamia pia jeshi la polisi, Patrobas Katambi, alitangaza bungeni pamoja na mambo mengine, agizo kwa IJP kusitisha mikutano yote ya vyama vya siasa nchini.

Jeshi la polisi kupitia msemaji wa jeshi hilo limetangaza kuondoa marufuku hiyo iliyotangazwa na waziri Katambi bungeni.

Jee kiprotokali zuio la Waziri linaweza kutenguliwa na viongozi wa jeshi la polisi?

Kwa kuwa waziri alitoa maagizo yake akiwa bungeni, si lazima pia utenguzi wa maagizo hayo ukatolewa bungeni pia?
 
IGP ana Bajeti kubwa kuliko Huyo Waziri Matambi
Mwenye fedha ndiye anayeamua game lichezwe vipi.
 
Hizo ni drama ili muone kwamba hawaelewani ni kidole na pete.
 
Halafu moja ya sababu zilizotajwa na mazafaka Katambi ilikuwa kuwapa watu muda wa kufanya kazi. Mazafaka wa TANPOL hajatumbia kama watu wameshamaliza kazi zao!
 
Gentleman,
zingatia ukimya wa wanasheria na mawakili walevi, wanaharakati uchwara na viherehere itakusaidia sana kusense hilo likoje 🐒
 
Kwa Tanzania inawezekana. Hata ya rais tu yanapinduliwaga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…