Jambo Limezua Jambo: Mifano Hai katika Siasa zetu...

Jambo Limezua Jambo: Mifano Hai katika Siasa zetu...

Kama wewe umekuwa mfuatiliaji mzuri wa siasa zetu unaweza kukumbuka jambo moja ambalo lilianzia padogo lakini mwisho likaishia kuwa jambo kubwa kwelikweli....Sakata la Dowans ni mfano mmoja liliishia kuondokana waziri mkuu...

Jambo gqni liliwahi kuanzia padogo likaja na makubwa...nitarudi.
MACHINGA KWA SASA NI BOMU LA NYUKLIA
 
Swala la watu wasiojulikana.

Ilianza kwa akina Ben Saa Nane, akaja Lissu wakafata akina Azory.

Mpaka na sasa hatujui mabaki ya mifupa yao ipo wapi.

Lakini, iwe duniani au akhera, waliowatenda watawajibika.
Unafikiria jambo hilo lilianza na kina Ben Saanane kweli?
 
MACHINGA KWA SASA NI BOMU LA NYUKLIA
Linakuwa bomu kwa sababu tu ya kutojua namna ya kushughulika nalo.

Badala ya kuwa "BOMU LA NUKLIA", Machinga wanaweza kuwa NEEMA kubwa sana kwa kiongozi mwenye maono mahsusi anayeweza kutumia hali ya hao jamaa na kuigeuza kuwa neema kubwa kwa nchi yetu.

Maana ya uongozi ni kuwa na uwezo wa kubadili hali hafifu kama hiyo na kuifanya kuwa ya kuvutia. Kiongozi wa aina hiyo ndio huacha alama katika uongozi wao. Anakuwa kiongozi wa kukumbukwa.
 
Tuliharibu shamba lake,aliyetatibu akapandishwa cheo DC hadi RC kazi nzuri.

Tukaharibu Hotel yake na biashara zake kumdhoufisha kiuchumi na kisiasa.

Tukamfunga kwa kusabanisha kifo cha Asquiline aliyempiga risasi hana kosa wala hatia.

Tukanunua wabunge,madiwani na viongozi wote tumbakishe mpweke.

Tukawaingiza bungeni wabunge 19 bila ridhaa wala baraka za chama.

Tukahakikisha hana mwakilishi mjengoni

Yote hayo hayatoshi!.

Tukamtengenezea kesi ya ugaidi,tunataka kumpoteza kabisa asiwepo,asisikike wala asionekane hatutaki kusikia mambo ya katiba mpya tunataka tutawale tutakavyo.

Mipango yetu yote ipo chini ya kamanda shupavu na Shujaa kweli kweli ACP Kingai,Mahita na Luteni Urio si hao tuna vizibiti vya hali ya juu eg Shangazi kaja na Jaji wa kimkakati.
Hakika hii inaweza kuishia kwenye kuzaa jambo kubwa litakalobadilisha kabisa hatma ya Tanzania.

Lakini vuta subira kidogo, maana mada kaiweka kwa yaliyokwishatokea.

Au hata yanayotegemewa kutokea, kama anguko la CCM?
 
Yule aliyebwagiwa mchakato wa kugombea urais... Akafurahia kususiwa... Akafurahia kutangazwa mshindi... Yaliyomkuta kwa sasa anawasimulia malaika.
Alifurahi kuchukua fomu moja peke yake na kuzimu akaondoka peke yake
 
Back
Top Bottom