Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ndio ......sasa tatizo kitu gani?
mama mtoto si yuko tayari kuthibitisha kuwa mtoto ni wako? na kuna dna tests ambazo zitathibitisha kuwa mtoto ni wako?
kama mama mtoto anataka kuwatupia mtoto na yeye ende zambia, basi mumu adopt kabisa kabisa na asiwe na uwezo wa kurudi na kudai mtoto wake.
Ndugu zangu wanamjua huyu mama wa mtoto kwa sababu alikuwa GF wangu zamani na wanajua aliolewa na kuzaa mtoto sasa leo nitaanzaje kuwaeleza mimi ndio baba wa huyo mtoto? nitaanzaje kuwaambia nilimpa mimba huku mumewe akijua na kuafiki kwa mazingira yetu?
kwa kweli hata mie nakubaliana na mke wa mtoa mada, hata mie nicngekubali kulea tena, kulea shughuli jamani, tena bahati mbaya mtoto ndio ana matatizo kama hayo, sasa kama walikubalianaga huko kwanini mama mtoto actafute njia mbadala ya kumlea mtoto kuliko kumlazimishia kwa mama wa watu? huyo mama mtoto kama baba mtoto amekubali kulea bac ampeleke mtoto hata kwa mama yake, mdogo wake na mtu wake yoyote wa karibu(ndugu)
Na kwanini ndugu wabebeshwe huo mzigo? An ulemavu gani huyu...............anaweza kufanya kazia na bado akishi na mwanwe kwa kuajiri msichana ama kukaa na mtu wa kumsaidia kumwangalia..........ivi mtoto ana matatizo namna hii kweli nitalala usingizi nisimwone hata siku 1; namimi ni mwanaume.ivi ule uchungu wa mwana huyu mwanamke hanao kabisa?:mad2:
Wakuu muda flani hapo nyuma nilikuwa na GF ambaye tulipendana, tukakosana kwa mambo ya kitoto tu, sasa kuna muda akapata mtu wa kumuoa kwakuwa bado tulikuwa marafiki wa kawaida akaja kwangu na jambo la ajabu kidogo.Huyo jamaa anaetaka kumuoa alishapima akajua hawezi kuzaa yaani mbegu zake zina matatizo,wakawa wameelewana apatikane mtu wa kumpa mimba ili aolewe na mimba ndogo jamaa ijulikane anaweza.Alinionyesha picha ya jamaa ambaye kwa mbaali tumefanana kidogo.
Nikamwambia nitafikiria na pia nikikubali nataka nisikie kauli ya jamaa na pia sitaki kuhusika na kitu chochote baada ya hapo.Zoezi lilifanyika mimba ikapatikana na mtoto wa kike kuzaliwa tukapoteza mawasiliano kama tulivyoelewana.Juzi kati bibie kanifata(baada ya miaka mitano) mumewe alifariki mwanzoni wa mwaka huu na yeye hana uwezo wa kumtunza mtoto peke yake,mtoto ana matatizo ya kiafya kibao asthma,tumbo nk kwa kifupi ni high maintenance kila wiki hospitali.Familia ya mumewe wamechukua kila kitu na hana nguvu wala muda wakupigania mali.Kapata kazi Zambia anadai hawezi kwenda na mtoto na kwakuwa mimi ni baba nimchukue.
Nimemweleza wife kila kitu kasema hana tatizo la mimi na yeye kumsaidia kifedha lakini swala la kubwagiwa mtoto mgonjwa hataki kulisikia na maelewano si yalikuwa tusijuwane tena?Tusaidiane mawazo wakuu.
Chief MAN UP!
Unatafuta ushauri upi hapo..................hao nduguzo unayajua ya kwao............yapo mengi tu unaweza kuja jua na usijue ...the matter on hand ni huyu mtoto wako.....na malaika wa Mungu............ndo maana wadau huko juu wanakuona kuwa unakwepa majukumu; kama wife yuko tayari kusaidia katika level hiyo wewe unashindwaje kusaidia zaidi..........na inavyoonekana mzazi mwenzio anataka kukwepa majukumu kama wewe sijawahi sikia Mama akisema nitamwacha mwanangu anayeumwa mie nikafanye kazi sehemu nyingine .................na hilo wife wako kaliona!
Kama mwanaume huyo mzazi wako asisafiri kwenda Zambia mpaka mtoto atakapopata nafuu au la aende naye; hilo la wife wako kubebeshwa mzigo ilhali mama wa mtoto yu hai si jema hata kidogo; Hiyo kazi ya mzazi mwenzio huko Zambia ni kwa manufaaa ya nani sasa kama si huyo mwanawe?:mad2:
Maji uliyavulia nguo sasa ni shurti uyaoge huyo ni mtoto wako biologically and you have to deal with I sense kwamba unataka kuagree na mawazo ya mkeo wewe ndio mwenyewe maamuzi ya mwisho I dont see the hardest part right there kama mkeo aliisha acknowledge the situation and she knows everything why would she disagree simply because your son is sick what the hell ! Chukua mtoto na umelee no any other excuse
Huyu Mzazi mwenzie ni mwehu...
Kwanza, kashasema kwamba huko Zambia amepata kazi itakayolipa hela nyingi, which means hatakuwa na shida ya hela.... kwa maana nyingine ni kwamba ataweza kumtunza mtoto wake bila matatizo...
Mi naona huyo mama hasemi ukweli... Sawa mume wake amefariki, lakini kwa sheria za sasa hakuna ndugu ambaye yuko entitled kukunyang'anya mali za mume wako. Kama hana nguvu za kufatilia mali za mume wake, nguvu za kurafuta kazi Zambia amezitoa wapi??..Aggggrrrrrrrrrrrrrrrrrrr.... Some women bwana....:mad2::mad2::mad2:
Ukidhani una ma MBINU, wanawake wana MITEGO.
Ndio umesha tegeka na mambinu yako.
Ulikuwa unafikiria nini wakati unakubali kuiacha damu yako ipotee kwa mwanaume mwingine wakati unampa mimba?Hiyo ni damu yako na huna haja ya kutaka kuanza mashauriano na mtu,mchukue mtoto na umtunze maana ndio matunda yako.Wakuu muda flani hapo nyuma nilikuwa na GF ambaye tulipendana, tukakosana kwa mambo ya kitoto tu, sasa kuna muda akapata mtu wa kumuoa kwakuwa bado tulikuwa marafiki wa kawaida akaja kwangu na jambo la ajabu kidogo.Huyo jamaa anaetaka kumuoa alishapima akajua hawezi kuzaa yaani mbegu zake zina matatizo,wakawa wameelewana apatikane mtu wa kumpa mimba ili aolewe na mimba ndogo jamaa ijulikane anaweza.Alinionyesha picha ya jamaa ambaye kwa mbaali tumefanana kidogo.
Nikamwambia nitafikiria na pia nikikubali nataka nisikie kauli ya jamaa na pia sitaki kuhusika na kitu chochote baada ya hapo.Zoezi lilifanyika mimba ikapatikana na mtoto wa kike kuzaliwa tukapoteza mawasiliano kama tulivyoelewana.Juzi kati bibie kanifata(baada ya miaka mitano) mumewe alifariki mwanzoni wa mwaka huu na yeye hana uwezo wa kumtunza mtoto peke yake,mtoto ana matatizo ya kiafya kibao asthma,tumbo nk kwa kifupi ni high maintenance kila wiki hospitali.Familia ya mumewe wamechukua kila kitu na hana nguvu wala muda wakupigania mali.Kapata kazi Zambia anadai hawezi kwenda na mtoto na kwakuwa mimi ni baba nimchukue.
Nimemweleza wife kila kitu kasema hana tatizo la mimi na yeye kumsaidia kifedha lakini swala la kubwagiwa mtoto mgonjwa hataki kulisikia na maelewano si yalikuwa tusijuwane tena?Tusaidiane mawazo wakuu.
Ongea na Wife, jaribu kumshawishi amkubali mtoto aishi na wewe mzazi. Huko mbele huwezi jua, si ajabu ndio atawaokoa huyo binti.. huyo anaekwenda Zambia, hataki mtoto kwa nia kuwa, ataolewa na mtu mwingine na atamwambia hajawahi kuzaa. Chukua mtoto, tunza! PERIOD.
ingenitokea mimi nisingekubali kuishi na mtoto inabidi akakae na mama yake ni mie nitatoa kila kitu ili kumlea kwani makubaliano ya mwanzo ndivyo yalivyokuwa ingawa hayana maandishishida zote zipo kwa huyu mwanamke....watulie wapange watakachofanya kwa makubaliano yao waliokubaliana kipindi kile wakivuana gagulo, mke mie nimemuelewa kabisa hata ingekuwa ni mie wangeleleana wanakokujua wenyewe.
Kaka ukirejea maelezo yangu pale juu nilikuwa 'sperm donor' tu na bibie na mumewe walinihakikishia sitahusika tena,sawa yametokea matatizo namsifu wife kwa kunielewa nilipo mueleza na hata sasa anahusika kumpeleka mtoto hospitali na kukidhi mahitaji yao kwa kuwatembelea kila wiki.Uanamme gani unataka niutumie kwa mtu muelewa hivo?