Jambo limezua Jambo.

huyo mtoto ni wa kwako bro,usikwepe majukumu msaidie kwa namna yeyote ile.
 
Mtoto huyo kama ni wako una wajibu wa kumtunza kwa gharama yoyote uwezayo. Acha kukimbia majukumu. Tafadhali, forget about the past and take your responsibilities.
 
Ulifanya kosa hapo mwanzo kuzaa na mke wa mtu ingawa mlikubaliana lakini si kisheria ndio maana hiyo kesi imekurudia wewe kwa sasa ulifanya kosa kubwa sana tena bila kufikiria anyway maji yameshamwagika

Nakushauri usimchukue huyo mtoto na kuishi nae ila umtunze kwa kumtumia fedha kila mara na kugharamia matibabu yake pindi yatakapohitajika ila usifanye kosa la kuishi nae hapo Zambia si mbali na dunia kwa sasa ni kijiji popote hela unatuma na inapatikana on time fuata ushauri wangu usije kuvuruga ndoa yako bure kwa mtu ambae hayuko responsible na majukumu yake (mzazi mwenzio) nahisi anachotaka kukifanya ni kuenda Zambia akiwa peke yake ili aolewe huko na ameona sehemu rahisi ya kumbwaga huyo mtoto ni kwako kataa kabisa mpk mpelekane mahakamani

navyokuona unaonekana kama huna maamuzi binafsi ndio maana unayumbishwa simama imara usitake kumvuruga mkeo kwa hayo mambo yako ambayo uliyafanya nahisi bila ushauri wala kufikiria mbali simama imara be a man usikubali kubaki na mtoto
 
Na wewe mwenyewe inaonekana unataka kuendelea kurina asali,kama mtoto ni wako kweli mzee huna budi lea mtoto tuondolee watoto wa mtaani
 

kwa kweli hata mie nakubaliana na mke wa mtoa mada, hata mie nicngekubali kulea tena, kulea shughuli jamani, tena bahati mbaya mtoto ndio ana matatizo kama hayo, sasa kama walikubalianaga huko kwanini mama mtoto actafute njia mbadala ya kumlea mtoto kuliko kumlazimishia kwa mama wa watu? huyo mama mtoto kama baba mtoto amekubali kulea bac ampeleke mtoto hata kwa mama yake, mdogo wake na mtu wake yoyote wa karibu(ndugu)
 


Chief MAN UP!

Unatafuta ushauri upi hapo..................hao nduguzo unayajua ya kwao............yapo mengi tu unaweza kuja jua na usijue ...the matter on hand ni huyu mtoto wako.....na malaika wa Mungu............ndo maana wadau huko juu wanakuona kuwa unakwepa majukumu; kama wife yuko tayari kusaidia katika level hiyo wewe unashindwaje kusaidia zaidi..........na inavyoonekana mzazi mwenzio anataka kukwepa majukumu kama wewe sijawahi sikia Mama akisema nitamwacha mwanangu anayeumwa mie nikafanye kazi sehemu nyingine .................na hilo wife wako kaliona!

Kama mwanaume huyo mzazi wako asisafiri kwenda Zambia mpaka mtoto atakapopata nafuu au la aende naye; hilo la wife wako kubebeshwa mzigo ilhali mama wa mtoto yu hai si jema hata kidogo; Hiyo kazi ya mzazi mwenzio huko Zambia ni kwa manufaaa ya nani sasa kama si huyo mwanawe?:mad2:
 

Na kwanini ndugu wabebeshwe huo mzigo? An ulemavu gani huyu...............anaweza kufanya kazia na bado akishi na mwanwe kwa kuajiri msichana ama kukaa na mtu wa kumsaidia kumwangalia..........ivi mtoto ana matatizo namna hii kweli nitalala usingizi nisimwone hata siku 1; namimi ni mwanaume.ivi ule uchungu wa mwana huyu mwanamke hanao kabisa?:mad2:
 

mie nakuelewa kabisa, lakini watu tumetofautiana kama hivi, mie ningehakikisha mwanangu nipo nae sambamba, sasa huyu anataka kumwacha, ndio ushauri niliompa huo ndugu yangu, kuliko amsumbue mwanamke mwenzie kwa makubaliano yao ambayo mwanamke wa watu hakuwepo walipokubaliana bac kwa sasa na watafute njia mbadala....mke wa mtoa thread nae ana roho nzuri kweli, mpaka anajitoa kumtafutia mwanamke mwenzie kazi ili asiende huko mbali amtunze mwanae mwenyewe lakini bado mama mtoto hataki, mama mtoto ni mkorofi tu!na wanapataga pa kuchezea.
 

Maji uliyavulia nguo sasa ni shurti uyaoge huyo ni mtoto wako biologically and you have to deal with I sense kwamba unataka kuagree na mawazo ya mkeo wewe ndio mwenyewe maamuzi ya mwisho I dont see the hardest part right there kama mkeo aliisha acknowledge the situation and she knows everything why would she disagree simply because your son is sick what the hell ! Chukua mtoto na umelee no any other excuse
 
Ongea na Wife, jaribu kumshawishi amkubali mtoto aishi na wewe mzazi. Huko mbele huwezi jua, si ajabu ndio atawaokoa huyo binti.. huyo anaekwenda Zambia, hataki mtoto kwa nia kuwa, ataolewa na mtu mwingine na atamwambia hajawahi kuzaa. Chukua mtoto, tunza! PERIOD.
 

Huyu Mzazi mwenzie ni mwehu...

Kwanza, kashasema kwamba huko Zambia amepata kazi itakayolipa hela nyingi, which means hatakuwa na shida ya hela.... kwa maana nyingine ni kwamba ataweza kumtunza mtoto wake bila matatizo...

Mi naona huyo mama hasemi ukweli... Sawa mume wake amefariki, lakini kwa sheria za sasa hakuna ndugu ambaye yuko entitled kukunyang'anya mali za mume wako. Kama hana nguvu za kufatilia mali za mume wake, nguvu za kurafuta kazi Zambia amezitoa wapi??..Aggggrrrrrrrrrrrrrrrrrrr.... Some women bwana....:mad2::mad2::mad2:
 
Ukidhani una ma MBINU, wanawake wana MITEGO.
Ndio umesha tegeka na mambinu yako.
 

amchukue amlelee vipi sasa kama bado hajaafikiana na mkewe?...mctake kumuweka mke kwenye matatizo ya huyu mumue wake, mume alishusha suruali mwenyewe kupanda mbegu huko nje bila kumshirikisha mkewe, sasa hivi ndio mke aonekane kikwazo?....hapo red labda nikuulize kama kaka umeoa?
 


shida zote zipo kwa huyu mwanamke....watulie wapange watakachofanya kwa makubaliano yao waliokubaliana kipindi kile wakivuana gagulo, mke mie nimemuelewa kabisa hata ingekuwa ni mie wangeleleana wanakokujua wenyewe.
 
Ukidhani una ma MBINU, wanawake wana MITEGO.
Ndio umesha tegeka na mambinu yako.

Samwea humu jamvini nilikisema kitu hiki

Wanaume huwa tunajidanganya sana........oh sie Ma-PLAYER ooh sie .........wapi bwana; at the end of the day we real SUCKERS like Uporoto anavyoonyesha hapa..........he is now being beaten at his own game!:mad2:
 
Ulikuwa unafikiria nini wakati unakubali kuiacha damu yako ipotee kwa mwanaume mwingine wakati unampa mimba?Hiyo ni damu yako na huna haja ya kutaka kuanza mashauriano na mtu,mchukue mtoto na umtunze maana ndio matunda yako.
 

kwanini huyo mama yeye aclee mtoto wake mwenyewe ""huko mbeleni hawezi jua ndio atamuokoa?""....hivi mnadhani kulea mchezo nini..
 
shida zote zipo kwa huyu mwanamke....watulie wapange watakachofanya kwa makubaliano yao waliokubaliana kipindi kile wakivuana gagulo, mke mie nimemuelewa kabisa hata ingekuwa ni mie wangeleleana wanakokujua wenyewe.
ingenitokea mimi nisingekubali kuishi na mtoto inabidi akakae na mama yake ni mie nitatoa kila kitu ili kumlea kwani makubaliano ya mwanzo ndivyo yalivyokuwa ingawa hayana maandishi

Huyo m/mke shida yake kubwa ni kuenda kuanza maisha mapya na kutafuta mme huko Zambia na anaona akienda na mtoto atamuwekea kiwingu wakati kulea mwanae ni jukumu lake halali kisheria

Hakuna haja ya kumsumbua mke wake jukumu la kulea ni lenu wote lakini mtoto akakae kwa mama yake mzazi

Mtoa mada ni mtu ambaye anaonekana si mtu wa kufikiria mbali ni mtu wa kukurupukia tu mambo bila kuhusisha watu wenye upeo na wanaoona mbali, kitendo cha kuzaa na mke wa mtu ili kumfichia aibu mumewe ni kitu alichokifanya kwa kutokuona mbali maana katika hali ya kawaida mtu mwenye akili timamu na mwenye kuona mbali hawezi kukubali ilo jambo hata siku moja namlaumu sana kwa kufanya ilo jambo sijui halikuwa haoni mbali nadhani alikurupuka sana na tena bila hata kushirikisha wanasheria yeye alichoona muhimu ni ku-do tu na kumpa huyo m/mke mimba

sasa hivi tena amebadilikiwa anataka kuachiwa mtoto amekosa mwelekeo kabisa, ni kweli yeye ni biological father hivyo hata akipimwa DNA itaonyesha ila anachotakiwa kufanya sasa ni kukataa kuishi na mtoto ila atoe matunzo na huduma zote zinazohitajika kisheria na si zaidi ya hapo na hapo hata akienda mahakamani ndio watakavyosema. Hamna haja ya kuumiza vichwa wakati ili jambo ni dogo sana huyo mzazi mwenzie aende Zambia na mwanae atatafuta housegirl huko na kumtunza mtoto
 
Uporoto01 baada ya kusoma majibu yako na maoni ya watu wengine nina maswali kwako

1. Unampenda huyo mtoto?
2. Unaogopa kumchukua mtoto wako kwa sababu ana matatizo?
3. Unategemea mkeo kukulelea watoto wako au wewe kuwa sehemu ya malezi ya watoto?
4. Unafikiri huyo mtoto ni tofauti na hao ambao mkeo anao?
5. Unaamini kuwa wewe hauhusiki kwa sababu mkataba ulikuwa wa kupena mbegu tu?
6. Ungefanya nini iwapo huyo mtoto ambae 'mkeo' anakataa kukaa nae asingekuwa na matatizo?
7. Utakuwa na amani iwapo la kutokea litatokea kwa huyo mtoto unayemkataa?
8. Utafanya nini siku huyo mkeo mpendwa atakapokuchia watoto mliozaa nae?

Majibu unayo, inawezekana timiza wajibu wako. Kulea kazi ndio, lakini hakuna mtoto wa zaidi kwa mtoto mwingine
 


Mkuu there is nothing like that kwa familia zetu za kiafrika...nadhani hata za kizungu ni ngumu ndo maana kuna sperm bank...sasa wewe upo physically halafu unamwongelea mtoto wako kama vile ni wa mtu mwingine bana?

hebu mchukue mpatie matibabu sahihi atapona tu uwezo si unao? kama ni mtoto tu na mama yake anachapa lapa, sidhani kama kuna tatizo, mtunze huwezi kujua atakuja kukufaa nini huko mbele!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…