Vitisho vya aina yoyote ile na Lobbying yoyote ile kwenye Media kuelekea Press conference ya Mhe. Freeman Mbowe @freemanmbowetz havina nafasi kwenye Uhuru wa Habari.
Kwani Freeman Mbowe hapaswi kupewa nafasi ya kusikika na Watanzania kupitia vyombo vya habari? Kama kurusha Matangazo ya Mkutano wa Freeman Mbowe na waandishi wa Habari ni kinyume na Sheria za Nchi bila kujali anazungumza nini basi tuko tayari kubeba gharama ya kufanya hivyo.
Tunaamini kwenye Uhuru wa kujieleza na tutasimama na hii imani yetu bila kujali matokeo, mtu asihangaike kupiga simu, JamboTV tutakuwa Mubashara/ Live kuanzia saa tisa kamili.