GE2025 James Mbatia asisitiza "Tupeni miili ya vijana wetu tuwazike"

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, James Mbatia amesema hali iliyojitokeza siku na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 nchini Tanzania, si suala la kisiasa pekee bali ni “maumivu ya wananchi walio wengi dhidi ya wachache”, kutokana na hali hiyo kugubikwa na maumivu, vifo- miongoni mwa mambo mengine.

Akizungumza na Jambo TV tarehe 5 Novemba 2025, Mbatia amesema hali hiyo haiwezi kufananishwa na migogoro ya kawaida ya kisiasa bali ni mwelekeo unaohitaji “fikra pana na pevu” ili kurejesha umoja wa kitaifa.

Amesema ni muhimu kila mwenye nafasi na sauti nchini kuzungumza wazi bila woga juu ya matukio hayo, akisisitiza kuwa hatua ya kwanza ya uponyaji wa taifa ni kurudisha utu kwa familia za waliopoteza maisha.

“Sasa tunajiuliza tufanye nini? Hatua ya kwanza ya maafa haya, kwenye maumivu haya, tupewe miili yetu, mashujaa wetu waliouawa ambao ni utamaduni kwenye utamaduni wetu, uungwana wetu wa kiimani na vinginevyo ili tuweze kuwasitiri vinginevyo ili tuweze kuwasitiri ndugu zetu, tukawazika kwa heshima mashujaa wetu bila kuendeleza ghadhabu zaidi kwakuwa mdharau mwiba mguu huota tende”, ameeleza.

Kauli ya Mbatia imekuja siku chache baada ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo, kueleza kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa sheria katika sehemu chache za nchi wakati wa uchaguzi, lakini vyombo vya usalama vilichukua hatua haraka, kitaalamu na kwa uthabiti kukabiliana na hali hiyo.

Aidha, katika hotuba yake ya kuapishwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, alionesha masikitiko yake kutokana na kile alichokitanabaisha kama matukio ya uvunjifu wa amani, upotevu wa maisha na uharibifu wa mali za umma na za watu binafsi, hasa katika majiji na miji, vilivyojitokeza kipindi cha uchaguzi

WhatsApp Image 2025-11-05 at 2.02.51 PM.jpeg
 
Miili mingi tiyari imekuwa dumped, sidhani kama watatoa hiyo nafasi Kwa ndugu kusitiri miili ya wapendwa wao
 
Ndo kitu gani hiki mkuu make kimesemwa sana kuwa miili imepelekwa huko ila sjafahamu ni eneo lipi hasa
Hiyo ni tanuru ya kuyeyushia object ngumu kama chuma au mabonge ya cement... yaan ukiingiza kitu chochote kinatoka majivu tu ndani ya dk tano tu.
 
Hawa ndio viongozi wenye weledi na ujasiri.

Sio hawa wa CCM wa mchongo. Wanashindwa hata kuthamini uhai wa bin Adam? Wanajali mali na wizi tu, ila uwezo mdogo. Hovyo kabisa.
 
Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, James Mbatia amesema hali iliyojitokeza siku na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 nchini Tanzania, si suala la kisiasa pekee bali ni “maumivu ya wananchi walio wengi dhidi ya wachache”, kutokana na hali hiyo kugubikwa na maumivu, vifo- miongoni mwa mambo mengine.

Akizungumza na Jambo TV tarehe 5 Novemba 2025, Mbatia amesema hali hiyo haiwezi kufananishwa na migogoro ya kawaida ya kisiasa bali ni mwelekeo unaohitaji “fikra pana na pevu” ili kurejesha umoja wa kitaifa.

Amesema ni muhimu kila mwenye nafasi na sauti nchini kuzungumza wazi bila woga juu ya matukio hayo, akisisitiza kuwa hatua ya kwanza ya uponyaji wa taifa ni kurudisha utu kwa familia za waliopoteza maisha.

“Sasa tunajiuliza tufanye nini? Hatua ya kwanza ya maafa haya, kwenye maumivu haya, tupewe miili yetu, mashujaa wetu waliouawa ambao ni utamaduni kwenye utamaduni wetu, uungwana wetu wa kiimani na vinginevyo ili tuweze kuwasitiri vinginevyo ili tuweze kuwasitiri ndugu zetu, tukawazika kwa heshima mashujaa wetu bila kuendeleza ghadhabu zaidi kwakuwa mdharau mwiba mguu huota tende”, ameeleza.

Kauli ya Mbatia imekuja siku chache baada ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo, kueleza kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa sheria katika sehemu chache za nchi wakati wa uchaguzi, lakini vyombo vya usalama vilichukua hatua haraka, kitaalamu na kwa uthabiti kukabiliana na hali hiyo.

Aidha, katika hotuba yake ya kuapishwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, alionesha masikitiko yake kutokana na kile alichokitanabaisha kama matukio ya uvunjifu wa amani, upotevu wa maisha na uharibifu wa mali za umma na za watu binafsi, hasa katika majiji na miji, vilivyojitokeza kipindi cha uchaguzi

Duh...
"Mama Tanzania"..
 
Back
Top Bottom