James Mbatia: Kwa kiasi kikubwa CCM ndio iliratibu Vurugu za Oktoba 29

James Mbatia: Kwa kiasi kikubwa CCM ndio iliratibu Vurugu za Oktoba 29

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mwanasiasa mkongwe nchini, James Mbatia, amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinabeba laana na uwajibikaji mkubwa kutokana na kuratibu matukio ya vurugu na maafa yaliyotokea tarehe 29 Oktoba.

Akizungumza katika mahojiano cha Chief Odemba, Mbatia ametumia mfano wa maandiko ya kidini kueleza uzito wa umwagaji wa damu nchini, akisema kuwa damu ya raia wasio na hatia inalilia haki sawa na ilivyokuwa kwa Kaini alipomuua ndugu yake Abeli.

"Kwenye maandiko, Kaini alivyomuua Abeli na kumwaga damu yake, Mwenyezi Mungu alimwambia damu ya ndugu yako uliyomwaga imelaaniwa. Tukirudi hapa kwetu, haya mambo yametokea kisiasa ndani ya vyama vya siasa, hasa vyama vikubwa vyenye nguvu," alisema Mbatia.

 
Back
Top Bottom