DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Mwanasiasa James Mbatia ametoa wito kwa Serikali na Viongozi mbalimbali kupata utulivu wa kutatua changamoto mbalimbali zilizopo nchini ili kupata majibu badala ya vuta nikuvute zinazoendelea huku akidai suala la Askofu Josephat Gwajima linapaswa kushughulikiwa kwa hekima ili kupata ufumbuzi sahihi.
Mbatia amesema hayo Juni 05, 2025 alipozungumza na Wanahabari Jijini Dar es Salaam.
Amesema “Naomba chondechonde Viongozi wa nafasi yoyote tuje sasa na wenye dhamana kuu ya kuongoza hili ni Serikali inaweza ikaamua kutumia taasisi yoyote ile ikawaambia basi embu tukae tuzungumze badala ya vuta nikuvute tukiendelea na vuta nikuvute tutakuta Tanzania yetu siyo tena ile tuliyokuwa nayo.”
Video: Torch