James Mbatia: Viongozi wengi wa Serikali wamekumbwa na upunguani wa uelewa wa mambo

James Mbatia: Viongozi wengi wa Serikali wamekumbwa na upunguani wa uelewa wa mambo

Kwakweli inashangaza sana fedha za mkopo wanajengea madarasa na vyoo

Wakati tuliambiwa tozo hiyo ndio kazi yake.

Tozo inatumika katika nini???

Kwanini serikali badala ya kujikita katika kukusanya mapato inakimbilia kukopa tu??

Kwanini serikali inawaogopa wafanyabiashara mpaka wakipandisha bei kiholela ipo kimya tu??

Je ndio tuseme kwamba wafanyabiashara ndio wanaoongoza nchi kwa sasa??
Mwezi huu December serikali imekusanya trilion 2.5,, record breaking

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Mwezi huu December serikali imekusanya trilion 2.5,, record breaking

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Kwanini walikopa 1.3 kujenga vyoo kama pesa hiyo ilikusanywa.

Au ni lazima tu tukope hata kama hatuhitajiki kukopa.

Hapa tutaanza kuulizana kwamba kama hela zipo halafu bado tunajilazimisha kukopa basi kutakua na watu wananufaika na hiyo mikopo inayokopwa kwa lazima.

Nashauri tusiwe tunakopa kama fedha tunazo za kutosha.
 
Mbatia ali ingizwa king na mwenda kuzimu kwamba chama chake kitakuwa chama kikuu cha upinzani akapandisha mabega. Kumbe aliingizwa choo cha kike, alicho kutana nacho kwenye uchaguzi ana jua yeye na alie mkuta huko chooni. Magu kitu ingine
Unaendeleza upunguani wa kuchanganua mambo anaouzungumzia Mbatia, jadili hoja zake wacha kelele zako.
 
James Mbatia, Ni aibu kwa viongozi karne hii ya ishirini na moja kujenga vyoo kwa pesa za 7mkopo wa uviko halafu wanaandika kwenye ukuta wa Choo "Ahsante uviko 19" kama jambo la Furaha kumbe ni vichekesho
Ni hivi, ile pesa ilikua itumike kuoam ana na uviko,,, sasa wao wakati wakiomba walitoa hoja kuwa huwezi kupambana na uviko bila ku create awareness,
Yaani Elimu ndicho chombo kina create awareness,, so miundombinu ya kuwezesha elimu ndo ni pamoja na madarasa na vyoo,,
Hiyo hoja ilueleweka kwa watoa pesa na wakatoa pesa wakijiua itaenda pia kuimarisha elimu kwa kuboresha miundombinu ya elimu,
SSH aliliweka hili wazi..

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Kwanini walikopa 1.3 kujenga vyoo kama pesa hiyo ilikusanywa.

Au ni lazima tu tukope hata kama hatuhitajiki kukopa.

Hapa tutaanza kuulizana kwamba kama hela zipo halafu bado tunajilazimisha kukopa basi kutakua na watu wananufaika na hiyo mikopo inayokopwa kwa lazima.

Nashauri tusiwe tunakopa kama fedha tunazo za kutosha.
Tozo ndo ilianza kabla ya oppotunity ya pesa za covid,,, lakini tozo haingeweza kujenga kwa haraka nationalwide,
So fursa ya mkopo wa covid ilipikuja,, wakatake advantage,
From day one mkopo wa covid ilikuwa uende pia kuimarisha elimu,, hata Rais alisema hilo siku anasaini

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
NOTED: Pesa za mkopo tena kiasi kikubwa "KUTUMBUKIZWA KWENYE MIRADI ISIYOZALISHA"
kujenga choo, madarasa, huduma za afya, walipaji ni wale wale wananchi na uwezo wao wa
awali hafifu wa kuzalisha...

Hakika Ndugai yuko sahihi sana anatutetea sisi wananchi....
 
Hakuna ulazima huo wa kutumia fedha za mikopo kwa ajili ya kujenga vyoo.

Kama unatumia akili sawa kufikiri utalitambua hilo ila kama unaamua kujitoa ufahamu na kuendeleza mjadala kutetea matumizi ya fedha za mikopo kujenga vyoo nitakua nimemalizana na wewe.
 
Kwa hiyo somo la Hesabu ni tatizo hata kwa Rais? Prof Ndalichako naye lugha ya Malkia ni issue
Punguani mkuu namjua😁😁😁
O1r.jpg
mnuy65432.jpg
 
Yeye mwenyewe amshukuru sana jakaya
Ndio matatizo haya haya anayowaambia Mbatia badala ya kujadili hoja mmafanya personal attack. Sasa amshukuru Jakaya kwa lipi? Kuwa mawenyekiti wa NCCR au kuzaliwa kwake? Usinambie kwa sababu ya ubunge wa enzi zile utakua umeshindwa kujadili hoja.

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
NOTED: Pesa za mkopo tena kiasi kikubwa "KUTUMBUKIZWA KWENYE MIRADI ISIYOZALISHA"
kujenga choo, madarasa, huduma za afya, walipaji ni wale wale wananchi na uwezo wao wa
awali hafifu wa kuzalisha...

Hakika Ndugai yuko sahihi sana anatutetea sisi wananchi....
Mkopo wote umeishia kwenye mradi wa elimu bure.
Walipaji ni akina nani kwani wakimaliza vyup hakuna ajira na hawana ujuzi waliotoka nayo vyuoni?
 
Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi bwana James Mbatia akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Leo hii ametolea ufafanuzi wa mambo mbalimbali yaliyojitokeza kwenye hotuba ya Rais na kauli ya Spika Job Ndugai

Mosi, Suala la akiba ya pesa za kigeni ameiomba serikali wabadili kauli yao ya kuwa tuna dola za marekani bilioni elfu sita yaani kimahesabu ni trilioni sita, China tu kama Taifa lenye pesa nyingi za kigeni wana dola za marekani trilioni tatu tu

Mheshimiwa Mbatia amesisitiza mahesabu ni tatizo kubwa sana kwa viongozi wetu kwani hata pesa za mkopo wa uviko wanazojengea vyoo vya wanafunzi wanamshukuru Rais kwa msaada wakati hilo ni deni la Taifa, Hata Rais akiondoka kama alivyoondoka Magufuli na deni kubwa la Taifa, Deni la Taifa ameliacha kwa wananchi na serikali yao

Wananchi ndio watatakiwa kulipa madeni haya tena kwa pesa za kigeni, Hivyo James Mbatia anashangaa Rais kusema Tutaendelea kukopa bila kuangalia nani atalipa madeni haya ambayo pesa zake hazizalishi kitu, Mbatia amesisitiza ni lazima kuangalia uwezo wa wananchi kulipa madeni hayo

James Mbatia, Ni aibu kwa viongozi karne hii ya ishirini na moja kujenga vyoo kwa pesa za mkopo wa uviko halafu wanaandika kwenye ukuta wa Choo "Ahsante uviko 19" kama jambo la Furaha kumbe ni vichekesho

James Mbatia, Ni aibu viongozi wa serikali toka ngazi ya Taifa mpaka kata kila wakati kusema ahsante Rais umetoa pesa za flyover, mara barabara mara afya wakati ni pesa za watanzania na hata kama ni mkopo ni deni la watanzania. Rais yeye hana pesa za kujenga barabara au flyovers labda kama Rais anauza madawa ya kulevya

Pili, Ni upunguani umeshajijenga na tunazidi kuharibu watoto wa Taifa hili kutokana na upunguani wa viongozi wetu ambao wanashindwa kuelewa maana ya mkopo na deni la Taifa, James Mbatia amesisitiza baada ya watu kujibu hoja za Job Ndugai wao wanatafuta personal attack kwa Ndugai

James Mbatia, Anasisitiza upunguani wa viongozi ndio unapelekaea watu kushindwa kujibu hoja na kukimbilia kumtukana Job Ndugai, Tatizo la upunguani linawafanya viongozi washindwe kupima hoja kama Job Ndugai amekosea, Je usahihi ni upi amehoji bwana Mbatia

Tatu, James Mbatia amesisitiza somo la hesabu hata Bungeni ni tatizo kwa wabunge wengi sana, Ndio maana mambo yanaposomwa kuhusu hesabu wengi hawaelewi, James Mbatia amesisitiza Kuwa viongozi wanaandaliwa
Bunge la mazuzu
 
Hii covd na Nani zake ziangaliwe vizuri!

Isije kuwa kazi moja wapo wa hizo niniliu ni kupunguza uwezo wa akili
 
James Mbatia, Ni aibu kwa viongozi karne hii ya ishirini na moja kujenga vyoo kwa pesa za 7mkopo wa uviko halafu wanaandika kwenye ukuta wa Choo "Ahsante uviko 19" kama jambo la Furaha kumbe ni vichekesho
Aaaah,mkuu hizo...Mimi siamini mpaka nione kwa macho yangu hiyo ...Ahasante Uviko!
 
Back
Top Bottom