James Mbatia: Viongozi wengi wa Serikali wamekumbwa na upunguani wa uelewa wa mambo

James Mbatia: Viongozi wengi wa Serikali wamekumbwa na upunguani wa uelewa wa mambo

Nashauri wapinzani wakajipangia issue na mikakati yao wenyewe badala ya kudandia issue zinazoibuka. Napata picha kama hakuna concrete strategic plans za kuendesha shughuli za upinzani.

Issue ya Ndugai ni kuachiwa wana CCM wakamaliza wenyewe. Wacha wamuite kwenye kamati wammalize n.k. Sioni sababu ya wapinzani kujiweka katika saga hili.
 
Nashauri wapinzani wakajipangia issue na mikakati yao wenyewe badala ya kudandia issue zinazoibuka. Napata picha kama hakuna concrete strategic plans za kuendesha shughuli za upinzani.

Issue ya Ndugai ni kuachiwa wana CCM wakamaliza wenyewe. Wacha wamuite kwenye kamati wammalize n.k. Sioni sababu ya wapinzani kujiweka katika saga hili.
Siasa ni agenda za kudumu pamoja na issues za kila siku.
 
Rejea hotuba ya SSH siku wanapokea pesa, alisema nchi nyingi ziliomba hiyo oesa ya uviko, ila Tanzania waliomba hiyo oesa itumike kuboresha elimu na Afya,, na walikubaliwa,,
So logically kuboresha vyoo na madarasa mashuleni inaitwa kuboresha elimu,
Mi sioni kosa hapo, iliekezwa tangu mwanzo kabisa

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Hoja ya Mbatia ni wazi. Kukopa pesa benki kwaajili ya kununulia pampasi ya mwanao ni ujinga na fedheha. Kopa kwaajili ya mambo ambayo unaona huna uwezo wa kuyamudu kwa pesa yako.

Kama tunashindwa hata kujenga vyoo, tunaweza kitu gani?
 
Kwakweli inashangaza sana fedha za mkopo wanajengea madarasa na vyoo

Wakati tuliambiwa tozo hiyo ndio kazi yake.

Tozo inatumika katika nini???

Kwanini serikali badala ya kujikita katika kukusanya mapato inakimbilia kukopa tu??

Kwanini serikali inawaogopa wafanyabiashara mpaka wakipandisha bei kiholela ipo kimya tu??

Je ndio tuseme kwamba wafanyabiashara ndio wanaoongoza nchi kwa sasa??
Hao viongozi wana hisa zao huko
 
Atahoji kama tu akusoma kwenye madarasa hayo na kunyea kwenye vyoo hivyo.
Atahoji kwanin vitu vya kufanya kwa nguvu zetu za ndani tunaomba msaada kutokwa kwa wazungu ni uzuni na uvifu wa kufikili wa viongoz wetu Yan kiongoz ina vaa suti na tai una tumia Kodi unaenda kuomba mkopo wa kujenga vyoo kweli Yani serikali imerudi miaka kumi nyumba na mawazo ya hajabu kama ndo hivyo Mwendazake angeomba mkopo wa kununua madawati mashuleni na kununua vitanda ya hospitalini na angekopa pesa za kununua ndege.
 
Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi bwana James Mbatia akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Leo hii ametolea ufafanuzi wa mambo mbalimbali yaliyojitokeza kwenye hotuba ya Rais na kauli ya Spika Job Ndugai

Mosi, Suala la akiba ya pesa za kigeni ameiomba serikali wabadili kauli yao ya kuwa tuna dola za marekani bilioni elfu sita yaani kimahesabu ni trilioni sita, China tu kama Taifa lenye pesa nyingi za kigeni wana dola za marekani trilioni tatu tu

Mheshimiwa Mbatia amesisitiza mahesabu ni tatizo kubwa sana kwa viongozi wetu kwani hata pesa za mkopo wa uviko wanazojengea vyoo vya wanafunzi wanamshukuru Rais kwa msaada wakati hilo ni deni la Taifa, Hata Rais akiondoka kama alivyoondoka Magufuli na deni kubwa la Taifa, Deni la Taifa ameliacha kwa wananchi na serikali yao

Wananchi ndio watatakiwa kulipa madeni haya tena kwa pesa za kigeni, Hivyo James Mbatia anashangaa Rais kusema Tutaendelea kukopa bila kuangalia nani atalipa madeni haya ambayo pesa zake hazizalishi kitu, Mbatia amesisitiza ni lazima kuangalia uwezo wa wananchi kulipa madeni hayo

James Mbatia, Ni aibu kwa viongozi karne hii ya ishirini na moja kujenga vyoo kwa pesa za mkopo wa uviko halafu wanaandika kwenye ukuta wa Choo "Ahsante uviko 19" kama jambo la Furaha kumbe ni vichekesho

James Mbatia, Ni aibu viongozi wa serikali toka ngazi ya Taifa mpaka kata kila wakati kusema ahsante Rais umetoa pesa za flyover, mara barabara mara afya wakati ni pesa za watanzania na hata kama ni mkopo ni deni la watanzania. Rais yeye hana pesa za kujenga barabara au flyovers labda kama Rais anauza madawa ya kulevya

Pili, Ni upunguani umeshajijenga na tunazidi kuharibu watoto wa Taifa hili kutokana na upunguani wa viongozi wetu ambao wanashindwa kuelewa maana ya mkopo na deni la Taifa, James Mbatia amesisitiza baada ya watu kujibu hoja za Job Ndugai wao wanatafuta personal attack kwa Ndugai

James Mbatia, Anasisitiza upunguani wa viongozi ndio unapelekaea watu kushindwa kujibu hoja na kukimbilia kumtukana Job Ndugai, Tatizo la upunguani linawafanya viongozi washindwe kupima hoja kama Job Ndugai amekosea, Je usahihi ni upi amehoji bwana Mbatia

Tatu, James Mbatia amesisitiza somo la hesabu hata Bungeni ni tatizo kwa wabunge wengi sana, Ndio maana mambo yanaposomwa kuhusu hesabu wengi hawaelewi, James Mbatia amesisitiza Kuwa viongozi wanaandaliwa
Mbatia mbunge wa CCM kwa hisani ya watu wa msoga

Sent from my ANE-LX2 using JamiiForums mobile app
 
Kama sio uviko bado watu wangeenda kichakani. Miaka 60 ya uhuru kweli mganga aliye waloga ambao hata kufunga mkanda mkajenga choo ameshakufa.
 
Hoja za Mbatia zilishajibiwa. Kiufupi Mbatia huwa anakuwa mkosoaji mkubwa kiongozi akiwa wa dini flani hivi.
kama fatuma karume au ruyaga sio.

mmeanza kuwaza ujinga.
na bado hayajaanza mawaraka ya akina dkt shoo au tek.

mbona awamu ya jana yalikuwepo malalamiko ya kina mwamakula?
 
Kaongea ukweli ingawa hatukubaliani na huyu mkongwe siku nyingi.
 
Najaribu kuwaza kwamba dhamira ya Rais itakuwa ni kusisimua hali ya uchumi wa mmoja mmoja, na ndio maana
akaiweka hiyo trilion 1.3 mtaani ili kuchangamsha nchi.

Kila halmashauri imepokea fedha hizi za uviko wajenge madarasa, madawati nk

Na kwa kweli, impact imeonekana dhahiri..hela hizi zimesambaa sana.

Ktk krismasi 5 zilizopita hakuna krismas yenye makeke kama hii recent.

Matumizi makubwa kuelekea na siku ya xmas na mwaka mpya ilikuwa ni fujo!

Nauli za mabasi juu, naambiwa mpaka routine za ndege ni busy abiria ni wengi.

Mimi naishi katika wilaya mojawapo tena ndogo tu hapa nchini.
natumia huku kama sampo..

Sasa ukiweka na la kupaa kwa makusanyo ya TRA mwezi desemba, na kuvunja rekord tena kwa hiyo abrupt margin! Nitakuwa sipo wrong

Huu nao unaweza kuwa ni ubunifu mzuri kuweka trilion kwa wananchi.
tatzo tu sijakubaliana na mgawo wa zanzibar kupewa bilion 300 kwa expense ya bara
 
Sema mbatia sema, japokuwa ni baada ya ndoa yako na CCM kuvunjika, Si mbaya waTz wenye akili timamu wanataka watu wenye akili timamu wa kuwasaidia kusema.
 
Kwakweli inashangaza sana fedha za mkopo wanajengea madarasa na vyoo

Wakati tuliambiwa tozo hiyo ndio kazi yake.

Tozo inatumika katika nini???

Kwanini serikali badala ya kujikita katika kukusanya mapato inakimbilia kukopa tu??

Kwanini serikali inawaogopa wafanyabiashara mpaka wakipandisha bei kiholela ipo kimya tu??

Je ndio tuseme kwamba wafanyabiashara ndio wanaoongoza nchi kwa sasa??
Tunamatatizo makubwa sana kwa kweli! Hali hii inashangaza na kusikitisha sana! [emoji849][emoji848]
 
Back
Top Bottom