GE2025 James Mbowe: Kesi ya Lissu Watu 300 hawafiki Mahakamani

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
James Mbowe ambaye ni mwanachama wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), anasema pamoja na CHADEMA kukubalika kwa wananchi lakini hata watu 300 hawafiki mahakamani kusikiliza kesi ya mwenyekiti wa chama hiko Tundu Lissu.

Kwa hiyo Baba yake akiwa Mwenyekiti ndio Watakuwa 300 ,na ndio CDM itakuwa na mwelekeoo
 
wengi wanakuwa online. Na haiwezekani maakamani pia wakaenda alfu moja na zaidi.. Hana akili huyo kijana
Na watu hawaendi Old Trafford kwa sababu mpira unaonyeshwa live kwenye luninga.

Amandla...
 
Anawasanuenu kwamba uk8jufanya kuipinga serikali, watanzania watakukimbia, utabaki Mwenyewe na familia yako.

Kwa k8fupi ametoa code kwamba kwa tabia za watanzania ndiyo maana baba yake akaamua kuwawahi na kwenda kuwauza kabla hawajamuacha kafilisika
Makengenza ni mfanyabiashara wa kisiasa kuanzia awamu zote za jk ila kwa jiwe alifinyiliwa mbali akarudi tena kwenye awamu hii kufanya biashara ila ile no reform no election ya nairobi ikaharibu biashara yake baada tal kuwa mwenyekiti
 
Hana hoja, alishafanya sensa virtually wanafuatilia wangapi? Ingekuwa sio virtually hoja yake ingekuwa na mashiko, kwa taarifa yako na huyo dogo, wafuasi wengi wa Lissu wanafuatilia virtually zaidi ya hao 300
Na hilo ndio tatizo. Ni watanzania wangapi wako online? Na wana VPN? Support inaonyeshwa live on the ground. Mbowe alishtakiwa na watu walijaa Mahakamani. Na wanachama wa Bawacha walikaa sana rumande kwa kukataa kunyamazishwa on the ground. Wakina Ruge walianzisha jogging Club kushinikiza aachiwe. Wakina mama wengine wakaandamana nje ya ubalozi wa Marekani. Na waliendelea kujazana Mahakamani hata baada ya miezi saba! Nilitegemea moyo huo huo ungeonyeshwa na hawa wa siasa za nginja nginja.

Amandla...
 
Mbona mahakama ilitoa maelekezo ya idadi ya watu wanaotakiwa mahakamani?
Ambapo ilisema wataoruhusiwa kuingia ni 60 pekee na wegine wote wataangalia kupitia mtandao
 
Uwanja una idadi yake pia vile vile mahakamani, pale mahakamani umeona kuna mapengo ya siti?
Huyo jamaa akili hana hajui kwamba wanaruhusu watu idadi kadhaa waingie pia polisi walipiga sana watu siku za mwanzo hiyo ikaleta uwoga kwa wengine.
 
Uwanja una idadi yake pia vile vile mahakamani, pale mahakamani umeona kuna mapengo ya siti?
Mengi tuu. Ukweli ni kuwa wafuasi wameufyata baada ya kuambiwa wasijazane Mahakamani.

Amandla...
 
Anamaanisha makamanda wamejaa mitandaoni hivyo siasa za nchi hii si za kupush watu waingie barabarani kama Kenya, utajikuta mwenyewe ndo maana mahakamani TAL yupo mwenyewe hata watu 300 hawafiki. Siasa za nchi hii ni kupush maridhiano unless unataka shida ukiwa peke yako.

Ndivyo nilivyomuelewa
 
Sio tatizo , nataka kukujulisha serikali walijua mahakamani pasingetosha ndio maana walikubali kesi iendeshwe virtually, wakati awali waligoma.

Jaribu kuvuta picha isingefanyika virtual, ingepata wahudhuliaji wangapi? Pale tu ukiangalia watu wamejibana kwenye mabenchi, je nje unajua wapo wangapi?

Kumbuka pale ni mahakamani kuna taratibu zake sio kiwanja cha mpira na hata huko pia kuna taratibu zake.
 
Huyo jamaa akili hana hajui kwamba wanaruhusu watu idadi kadhaa waingie pia polisi walipiga sana watu siku za mwanzo hiyo ikaleta uwoga kwa wengine.
Sasa kama unakiri kuwa watu wanaogopa kupigwa mnadhani nani atawaletea mabadiliko? Polisi hawajaanza leo kuwapiga wapinzani lakini hapo awali hawakukubali kunyamazishwa. Vijana wa leo mkiona polisi anafanya usafi mnajifungia ndani! Halafu bila aibu mnawategemea wakina Mbowe na Lissu ndio wawapiganie. Hopeless kabisa.

Amandla...
 
Huyu dogo mpuz anataka kujifanya na yeye gwiji wa siasa

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…