James Mbowe ambaye ni mwanachama wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), anasema pamoja na CHADEMA kukubalika kwa wananchi lakini hata watu 300 hawafiki mahakamani kusikiliza kesi ya mwenyekiti wa chama hiko Tundu Lissu.
Nafikiri huwa unasema bila tafakuri. Hivi waingereza waliingiaje Tanganyika? Kwa taarifa yako Tanganyika haikuwa koloni la Uingereza kwa sheria za League of Nation. Uingereza ilikabidhiwa Tanganyika baada ya Ujerumani kushindwa kwenye vita ya kwanza 1919. Hivyo Uingereza ilikuwa kama muangalizi wa Tanganyika mpaka tutakapoweza kujitawala.
Tanganyika katika historia imepigana vita ya kumwaga damu zaidi na Wajerumani kwani ndio walikuwa wakoloni halisi wa Tanganyika baada ya kigawana makoloni kwenye Berlin conference 1887.
Unaweza kuonyesha chochote alichofanya muingereza baada ya kupewa Tanganyika? Hata Ikulu ya Magogoni ilijengwa na Wajerumani.
Kuna tofauti kubwa kati ya Kenya na Uganda. Hizo zote ziligawiwa Kwa waingereza,ndio maana kwenye nchi hizo Uingereza iliwekeza zaidi kuliko Tanganyika.
Tanganyika lilikuwa ni eneo la kuchuma malighafi zaidi lakini viwanda vilijengwa Kenya mpaka Reli kutoka Mombassa mpaka Uganda.
Someni kwanza historia kabla hujakurupuka kujibu humu.
Uingereza haikuhitaji nguvu kuitaawala Tanganyika.
Reli ya kati walijenga Wajerumani. Hivyo basi Wasingejinganya kwenye vita ya kwanza ya Dunia, Tanganyika lingebakia kuwa koloni lao kihalali kufuatia makubaliano ya Berlin.
Kwa hiyo kwa akili unafikiri ungekaa meza moja na Wajerumani ili wakupe Uhuru wako?
Maridhiano hutegemea na mazingira yaliyopo.
Hayo majadiliano ya Mbowe Na ccm yalisaidia nini? Kama hayo maridhiano yangekuwa na tija akina Mzee Kibao na kina Soka na wengine si wangekuwepo!!
Kwa Mbowe aliridhiana na ccm hao wapotee?