wakati wa sakata maarufu kama escrow ambalo liliwapatia hawa ndugu zetu mabilioni..kulikuwa na pande mbili zikibishana.
upande wa kwa kwanza ulikuwa wa serikali ukiongozwa na aliyekuwa kiongozi mkuu wa serikali waliosema "hiyo pesa siyo ya umma"
upande wa pili ulikuwa wa wabunge wengi wa kipindi hicho wakati Bunge likiwa bado Bunge la wananchi likiongozwa na mama semamba na baadhi ya viongozi wa serikali...hawa walisema " pesa hizo ni za umma"
mabishano hayo yaliendelea kwa kipindi kirefu sana..hata hivo waliokuwa wanasema pesa si ya umma walikuwa wanaongoza serikali,basi watuhumiwa hawakufanywa kitu chochote
Baada ya muda,baadhi ya waliokuwa wanaamini kuwa pesa ile ni ya umma,wakashika madaraka 2015, wakawatia ndani watuhumiwa kutokana na imani waliyokuwa nayo kuwa pesa ni ya umma
kwa bahati nzuri kwa watuhumiwa,baadhi ya wale walioamini kuwa pesa ni ya umma, hawapo tena madarakani, madaraka yamerudi kwa wale walioamini kuwa pesa si ya umma,hapo lazima huyo DPP aagizwe asiendelee na kesi.
tusubiri watakapoingia madarakani wale wa imani ile nyingine,labda DPP ataagizwa tena aone sababu ya kuendelea na kesi
Lakini hata hivo mjadala unapaswa kuanza tena kuwa ile pesa ilikuwa ya umma au siyo ya umma, na wala siyo kuimba wimbo wa DPP ambao tunaamini ameagizwa aimbe walau kwa sasa