James Sinclair: A Friend or Foe?

...lakini si zinauzwa online na wote tuko online? Bado nakumbuka maneno ya kutia moyo kwamba, we can buy the shares from these investors and get to make a difference. Kulikuwa na plan ya kuwatumia NICO kununua shares...sikumbuki vizuri.
Hivi kama JK ana shares(example) na kampuni ambayo ana share imekuwa ya kwanza kukubali vipengele vipya.
Apongezwe kwa kuweza kumake difference as a shareholder of that company? AU...?
Nashindwa nimpongeze au nimbeze...
 

Insurgent.. hivi unaelewa kitu kinachoitwa mgongano wa kimaslahi?
 
Insurgent,

Wazo zuri sana unaposema nasi tumnunue share! kama hatutapenda kulitazama swala hili kwa undani zaidi.

Unajua kwamba Share za Barricks zinauzwa ktk soko la Canafa TSE ambao kila unaponunua shara yako kwao ni faida kwa soko la Canada, pili hizo share wewe mlalahoi utanunua ngapi?..kwa fedha gani tulizokuwa nazo ikiwa mishahara zenyewe ndio hiyo laki moja mwa mwezi!..

Tatu kumbuka kwamba ni mali yako inauzwa kwa watu wa dunia nzima na mchuuzi anayedai kuwa mali yake!... yaani kila mtu duniani anakuwa na chake ktk mali ambayo haitengenezwi bali kuchimbwa toka ktk ardhi yako!.. kwa nini sisi tusiwe na soko letu? Mbona South Africa makampuni yao mengi wanayo ktk soko lao!..Je, sisi ndio tunauza Dhahabu ama Canada na hivi kweli sisi huwa tunapeleka kitu gani huko sokoni ikiwa mali zetu zinauzwa na wageni?..

Kisha nina hakika kabisa kwamba Mkapa ndiye mwenye share Barricks na kuna uwezekano mkubwa mgongano ulokuwepo kati ya hawa jamaa zetu umeanzia hapo Barricks baada ya JK kutishia kama hakupewa Urais.

Sina ushahidi wa kuunganisha mambo haya isipokuwa ni lazima tukubali kwamba tumeibiwa. Naifahamu vizuri sana kampuni hii ya Barricks na kifupi ni kwamba kampuni hii inaogopwa duinia nzima kwa ujambazi wake inapofikia maswala ya dhahabu. Toka Sith America hadi makampuni mengi ya Canada wamewahi fikishana mahakamani na kila mara Barricks imeweza kuzima mashambulizi yote kwa sababu ni moja ya makampuni yanayoingiza fedha sana Canada (kwa mali isiyokuwa yao).

Utetezi wa Barrick kwa viongozi wa hapa nisawa na ile kampuni ya UK ya vifaa vya kijeshi iBAE inavyotetewa na Viongozi wa UK. Hii haina maana kwamba hawa jamaa wanatusaidia sisi ama wanatupenda sana...Hiyo Bulyanhulu yenyewe ilinunuliwa kwa mikwara (kinguvu nguvu) na hasa kutokana na lile scandal la kuuawa wananchi!..

Karibu ndugu yangu huu ndio Ukoloni Mamboleo!...tunauzana wenyewe.
 

Kama alivyosema MKJJ kuwa tatizo ni mgongano wa kimaslahi tena kwa kiongozi mwenye dhamana makubwa kama yake.

Kama utakumbuka August 2000, Dick Cheney alijiuzulu kazi yake ya CEO wa Halliburton ili aweza kugombea kama makamu wa rais wa Bush. Cheney ilibidi auze company stock zake zenye thamani ya milioni $30, lakini kisheria haikuwa lazima aziuze. The moral of the tory ni kuwa rais amepewa dhamana kubwa na wanachi na ni vizuri kwa kiongozi kuepuka mgongano wa kimaslahi. Maslahi ya taifa yanapokuwa hataraini wananchi wanategemea viongozi wao wasimame kidete kuwatetea. Kwahiyo, wananchi wanahaki ya kuuliza dealings za kiongozi wao ili kuhakikisha misingi ya utawala bora inalindwa kwani ni hao wananchi ndiyo waajiri wake.
 
He.......

Mzee Mwanakijiji mbona unachezea akili za watu hapa kama alivyofanya Karamagi? Yaani unaibuka na kudai una mkataba na unaonyesha kuwa hawa jamaa wana hisa na hayo mengineyo halafu bila ya kuonyesha huo unaoita mkataba tayari umeshapata washabiki humu...

Lete mkataba hapa la sivyo utakuwa mzushi na hawa wanaoshabikia sitashindwa kuwatofautisha na kina Mudhihir na wenzie wanaotafutwa na mayai viza na watanzania..

Tanzanianjema
 
hahhahaha.. sikusema ninao mkataba nimesema nimeuona. Huko nilikouona hawaniruhusu kuuchukua.... unless someone will be able to assist me... but in that I need a patner in crime.
 
MJJ,
Mzee wangu huna haja ya kuweka ushahidi wowote hapa kwani mambo anayoyafanya Sinclair utadhani yeye ndiye Karamagi.
Hawa jamaa hadi wanahodhi ardhi hapa nchini kama mali yao na wanaingia mikataba wao. Kisha hii kampuni haipo kwenye soko letu ila nje na hakuna Mdanganyika hata mmoja anayefahamu kulikoni kampuni hii inatuingizia kiasi gani ktk mfuko wa Taifa letu zaidi ya kuchukua kidogo tulichokuwa nacho!..
Ebu tazama mkataba kama huu hapa:-
http://www.prnewswire.com/cgi-bin/stories.pl?ACCT=104&STORY=/www/story/06-05-2007/0004601904&EDATE=

Wanabodi naomba somo hapa kidogo!...
Hivi kweli serikali yetu na hasa wizara ya Madini inashindwa kuwa na wataalam wenye uwezo huu maanake actual exploration haifanywi na hawa jamaa ila hukodisha makampuni mengine. Hizi properties wamezipata vipi?...na hii kampuni ipo registered wapi hasa. Kusema kweli hadi leo sijaweza kuelewa vizuri connection ya Sinclair, dhahabu na Tanzania.
Hivi South Africa, Ghana na huko South America pia wanamtumia huyu jamaa? Je tusipomtumia kuna athari gani?
 
News Release - Monday, November 05, 2007
Title: Proposed US Mining Law Reinforces Tanzanian Royalty's Strategy to Focus on Republic of Tanzania

--------------------------------------------------------------------------------
Tanzanian Royalty wishes to announce that the recent passing of a bill by the U.S. House of Representatives requiring hard-rock mining companies to pay non-profit based royalties on minerals extracted from public lands will have no material impact on the company whatsoever.

The Company's mineral assets are located in Tanzania whose laws are designed to foster development of its mineral resources under a fiscal regime that returns real benefits to all stakeholders without compromising the country's environment.

"Similar laws have been put forward in the United States many times before and it will face strong opposition in the Senate and a White House veto as well," noted Tanzanian Royalty CEO, Jim Sinclair. "The enactment of this shortsighted legislation would only serve to increase American dependence on foreign sources of industrial commodities just like the nation has for oil."

Tanzanian Royalty has operated in the Republic of Tanzania for well over a decade and its exploration assets are located in some of the country's most prospective mineral belts. Tanzania sees the minerals industry as a key driver behind its efforts to improve the economic well being of its people at a time when demand for mineral commodities has reached historic levels.

Respectfully Submitted,

"James E. Sinclair"

James E. Sinclair Chairman and Chief Executive Officer
 
Tunapoenda hakueleweki...I wont be suprised with the headline "Tanzanians seek refuge after sale of it's land"
 
Mwalimu alitaifisha, tunasubiri tuone kama kweli watafanikiwa kuwanyamazisha walalahoi.
 
How low can we go...mimi inaniuma sana maana hawa hawalipi hata kodi...!!! Hivi sisi si tuna makabila yanasifika sana kwa uchawi; sasa hao wachawi wapo wapi wafanye vitu vyao kwa hawa mafedhuli. Wanatufanyia mbaya sana...uchawi upo wapi Taifa linapouhitaji..
 
..sina hata la kusema!nikiisoma hii huwa nachoka vidole mpaka mawazo!nabaki kutoa laana tu!

..unajua,wazungu wanatushangaa jinsi tunavyoiuza nchi!ndio maana hawatuheshimu!
 
Kikwete, Sinclair na Barrick😛embetatu ya machozi?

Lula wa Ndali-Mwananzela Desemba 19, 2007
Raia Mwema

KWA mwaka mzima sasa hakuna kitu ambacho kimegusa hisia za umma wa Watanzania kama suala la madini.

Na kwa namna ya pekee suala hilo la madini lilifikia kilele chake pale mbunge kijana toka Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe alipojikuta anapigwa “stop” kwenye Bunge baada ya kudai uundwaji wa Kamati teule ambayo ingechunguza mikataba ya madini na kuona kama “kuna sheria zilizovunjwa” na kuwatambua ni kina nani waliohusika.

Kitendo cha Wabunge wa CCM wakiongozwa na Waziri Mkuu, Edward Lowassa na waziri mkuu mstaafu John Malecela kumfungia kijana huyo kilisababisha si tu hisia ya uonevu, bali pia hisia ya ukandamizaji kwa kutumia nguvu ya Bunge.

Baadhi ya watu walionekana kukerwa na hali hiyo na wengine wakishikwa na madonge kooni ambayo yaliwafanya hata washindwe kusema. Kwa mara ya kwanza katika historia yetu wananchi walishuhudia jinsi gani wingi wa wabunge wa chama kimoja bungeni unavyoweza kutumika vibaya kuhalalisha na kuficha mapungufu ya Serikali.

Siku zikapita na miezi ikenda; Na wananchi wakiwa wamekata tamaa Rais Jakaya Kikwete akatangaza kuwa ameunda tume ya ushauri juu ya sekta ya madini ambayo itaongozwa na aliyewahi kuwa mwanasheria mkuu wa Tanzania Jaji Mark Bomani. Kuundwa kwa kamati hiyo kulipokewa kwa shangwe na baadhi ya watu hasa wale ambao ni mashabiki wa chama tawala wakiamini kuwa hatimaye “Rais kafanya kweli”. Na kwa watu wa kawaida habari hizo zilikuwa kama mvua iliyokuwa ikusubiliwa jangwani kwa miongo hasa pale kati ya wajumbe wake lilipotajwa jina la Zitto.

Hata hivyo, baada ya muda kupita na habari sahihi kutiririka, wananchi wakaambiwa kuwa Kamati hiyo si majibu ya hoja ya Zitto bungeni na kwa hakika “haihusiani moja kwa moja” na hoja hiyo ya Zitto.

Jaji Bomani mwenyewe akizungumza na mojawapo ya vyombo vya habari vya nje ya nchi alinukuliwa kukiri kuwa kamati hiyo kimsingi ni Kamati ya ushauri na haina nguvu za “kisheria” kama Kamati ya Bunge na hivyo haina uwezo wa kuita mashahidi au kuwalazimisha kisheria kusema ukweli au kutoa taarifa sahihi.

Wananchi wakiwa wanajikuna vichwa kufikiria mambo hayo wakaambiwa kuwa Kamati hiyo imeanza kuangalia kazi zilizofanywa na Kamati nne zilizotangulia kabla yake. Kwa mara ya kwanza (natumaini ni mara ya kwanza) ndani ya wiki chache Serikali ikaunda Kamati kuangalia kamati nyingine bila kuondoa uwezekano kuwa huko mbele kamati nyingine itaundwa kuangalia kazi za kamati iliyoundwa kuangalia kazi za Kamati nyingine! Watanzania waliokuwa wamejawa na matumaini kama walivyotumaini ushindi wa Taifa Stars, wakajikuta wamefungwa goli la kutolewa Challenji!



RAIS Jakaya Mrisho Kikwete

Kitu kimoja ambacho Watanzania wengi hawajakifahamu au hakijawekwa hadharani inavyopasa ni sababu kubwa kwa nini Rais Kikwete hawezi na hatoweza kamwe kusafisha sekta ya madini nchini. Nia yake ya kutaka tuwe na kile anachokiita “win-win situation” haiwezi kukamilika na haitatokea kwa sababu yeye mwenyewe ni mdau kwa namna moja au nyingine na hali iliyopo sasa (status quo).

Hivyo wale wanaokaa wakiwa wanatumaini kuwa mapendekezo ya Kamati ijayo YOTE yatafanyiwa kazi na yatachangamkiwa, huyo bora ajiandae kukata tamaa na kushika tama. Kwanza kabisa mapendekezo yote hayatawekwa hadharani; kwa sababu ni mapendekezo tu na hiyo tume haitakiwi iyaweke mapendekezo yake hadharani bali kuyawasilisha kwa Rais kwanza na Rais halazimiki kuwaambia ni nini kimependekezwa.

Jambo la pili hata kama ataamua kutekeleza baadhi ya mapendekezo maslahi ya kwanza atakayoangalia na ambayo hadi hivi sasa ameyaangalia ni maslahi ya “wawekezaji” ili tusiwatishe. Hivyo mapendekezo yoyote ambayo kwa namna moja au nyingine yatatashia uwekezaji katika sekta ya madini yanakufa kabla hayajafika kwenye deski la Rais ofisini kwake.

Kwa kadiri Serikali ya Rais Kikwete inavyojaribu kutengeneza mizani ya mafanikio kati ya wawekezaji na wananchi kuwa ni lazima iwiane kwa hakika wanakuwa kama watwangao maji kwenye kinu. Je, ni lazima manufaa ya wawekezaji yalingane na manufaa ya wananchi wa nchi/maeneo ambapo wawekezaji wanafanya biashara zao?

Kwa kadiri ilivyo sasa inaonekana wazi kabisa kuwa wanaonufaika na uwekezaji ni makampuni na wananchi wanapata “viperemende” vya shule, zahanati n.k Je, yawezekana kupindua modeli hiyo na kuhakikisha kuwa mafanikio ya wananchi yanazidi yale ya makampuni?

Hata hivyo, kuna sababu nyingine na kubwa zaidi ambayo inamfanya Rais Kikwete kuwa na kigugumizi na wakati mwingine kusita kuchukua hatua za kijasiri, madhubuti, na zenye lengo kamili kuibadilisha sekta ya madini. Jambo hilo ni lile ambalo naweza kuliita ni pembetatu ya machozi. Pembetatu hii inamhusu Rais Kikwete mwenyewe, rafiki wa miaka 13 sasa James Sinclair, na kampuni kubwa kabisa ya uchimbaji dhahabu duniani ya Barrick Gold (kutoka Canada).

Kuweza kukaa chini na kuielewa pembetatu hii ndiyo mwanzo tu wa kuelewa ni kwa nini Rais Kikwete licha ya ahadi zake kuhusu mabadiliko katika sekta ya madini hawezi, hatoweza na hana sababu ya kuweza kubadilisha sekta hiyo ili iwe na manufaa zaidi kwa wananchi.

James Sinclair aliingia nchini akiwa na kampuni ya Sutton Resources na alianza shughuli zake za utafiti na uchunguzi wa madini. Baada ya kugongana na bodi ya wakurugenzi wa bodi hiyo Sinclair aliachana (alilazimishwa kuacha?) nayo na kuamua kuanzisha kampuni yake ya Tan Range Exploration iliyotokana na kampuni yake nyingine ya Tanzanian American Development.

Kampuni hii ya TRE liingia nchini ikiwa na lengo la kufanya ugunduzi wa madini mbalimbali (hasa dhahabu) na baadaye inapogundua eneo lenye madini hayo basi huliuza kwa makampuni makubwa ya uchimbaji madini na wao huanza kulipwa kiasi cha fedha kutokana na uchimbaji utakaofanywa pale. Kimsingi kampuni hiyo ya Sinclair haifanyi uchimbaji wa biashara bali wa utafiti na baadaye wakigundua madini basi hujitangaza kwa makampuni makubwa. Kampuni hii ina mikataba mbalimbali na baadhi ya makampuni na mkubwa zaidi ni ule kati yake na kampuni ya Barrick Gold ya Canada ambao wanaupendeleo maalum pale ambapo TRE wanagundua madini.

Akiwa na kampuni ya Sutton Resources Sinclair ndiye aliyesimamia utafiti wa eneo la machimbo ya Bulyanhulu ambayo kama wengi wanavyofahamu yanahusisha kuondolewa kwa nguvu kwa wachimbaji wadogo wadogo na madai ya kuwa baadhi yao walifukiwa wakiwa hai. Ni uhusiano huu ndio ulioifanya Sutton Resources kuuza machimbo hayo kwa Barrick Gold. Na kama nilivyosema hapo juu, kampuni yenyewe ya Sutton baadaye ikanunuliwa na Barrick.

Kuingia kwa Sinclair katika Tanzania kulikuwa kumepigiwa mahesabu ya kina na kubwa zaidi ni kujenga uhusiano wa karibu na wanasiasa na wadau wakubwa wa sekta ya madini. Yeye na binti yake, Marlene, wakaingia Tanzania mmoja akijenga uhusiano na wanasiasa na binti akijushughulisha na shughuli za kijamii. Lengo lao, hata hivyo, likiwa moja tu nalo ni kulainisha nyoyo za Watanzania ili hatimaye watakaposema wanachotaka wanapata.

Kuelewa upendeleo huu ni kuelewa kuwa wakati kampuni ya TRE inabadilishwa kutoka Tan Range kampuni ya Barrick Gold ilinunua hisa za mtaji kwenye kampuni hiyo mpya na hivyo kusaidia katika kuanza kwake. Pamoja na ushirikiano wa kibiashara na Barrick kampuni ya TRE ina ushirikiano na makampuni mengine ya uchimbaji ambayo yanafuatilia shughuli kwa uangalifu.

Leo hii TRE ni mojawapo ya makampuni/watu wachache wenye kumiliki eneo kubwa la ardhi. Ikiwa na leseni zaidi ya 120 za uchunguzi kuzunguka eneo la Ukanda wa Ziwa Victoria, kampuni hii kwa wengine inaonekana ndiyo kiini cha matatizo ya madini katika eneo hilo kubwa hasa kutokana uhusiano wake na kampuni ya Barrick Gold.

Kampuni ya Barrick Gold imekuwa ikikabiliwa na upinzani mkubwa sehemu mbalimbali duniani kama Australia, Chile, Argentina, na Peru. Kitu kimoja ambacho hadi hivi sasa ni dhahiri ni kuwa kile ambacho Barrick inataka, Barrick inapata.

Katika kuhakikisha kuwa hilo linafanikiwa Tanzania, James Sinclair alijitahidi kuwa na urafiki wa karibu na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini kati ya miaka ya 1990, Jakaya Kikwete. Kwa mujibu wa mmojawapo wa wasaidizi wa karibu wa Sinclair ukaribu wake na Waziri Kikwete ulijenga uhusiano wa karibu, kuaminiana na uwazi zaidi na matokeo yake ni urafiki ambao yeye mwenyewe Sinclair anauita ni wa “Karibu”. Urafiki huo ulidhihirishwa pale Rais Jakaya Kikwete alipomualika Sinclair katika sherehe za kuapishwa kwake!

Pembetatu hii inaendelea kuzunguka kila wakati na hasa hivi karibuni ambapo Rais Kikwete alirejea kutoka katika ziara yake ya “kikazi” ya ki Vasco Da Gama huko Marekani. Ziara hiyo ya Rais Kikwete ilitokana na mwaliko wa Mwenyekiti wa Bodi ya H. Sullivan Summit Balozi Andrew Young. Balozi Andrew Young ni mtu ambaye katika jamii ya watu Weusi wanamuona kama ni shujaa ambaye alishirikiana na marehemu Dk. Martin Luther, siku hizi ameanza kuonekana kwa mwanga mpya na tofauti.

Kuna baadhi ya watu ambao wanaamini kuwa Balozi Young amekuwa ni “mbeba mifuko ya ubepari wa Marekani” hasa kwenye nchi za Afrika. Imani ambayo imekuwa ikijengeka siku za karibuni kuwa Balozi Young amenunuliwa na anatumika kama kibaraka wa ubepari na hajali mambo mengine yoyote isipokuwa kutengeneza pesa kupitia migongo ya Waafrika.

Leo hii Andrew Young amepigia debe mkutano ujao wa Sullivan ufanyike nchini Tanzania jijini Arusha. Pamoja na sababu nyingi, bila ya shaka, Young atatengeneza ngawira kidogo. Kampuni ya Young inahusika moja kwa moja na umiliki wa hoteli ya Mt. Meru mjini Arusha.

Lakini zaidi ya yote, Young ni mjumbe wa bodi ya Ushauri ya kampuni ya Barrick Gold. Hivyo bila ya shaka uhusiano wake wa karibu na Rais Kikwete, Waziri wa Madini Nazir Karamagi, Sinclair na watu wa Barrick unamsaidia sana katika kuhakikisha kuwa mambo hayaendi vibaya kwa Barrick hasa yanapokuja kwenye maamuzi ya Serikali.

Kwa kuangalia mambo hayo tunaweza kuona pembetatu ambayo ndani yake kuna mambo mengi ambayo kwa hakika yameshikamana na kufuatana kama lila na fila. Tunaweza kuona jambo moja dhahiri kuwa Rais Kikwete, Kamaragi, James Sinclair, na Andrew Young wote wanaunganishwa kwa namna moja au nyingine na kampuni kubwa kabisa ya madini duniani ya Barrick Gold. Na tukiangalia mifano ya nchi mbalimbali ambako Barrick imekuwa ikilalamikiwa na kupata upinzani tunaona kuwa Barrick haiko katika upande wa kushindwa.

Hakuna sheria au taratibu ambazo zinaweza kutengenezwa na nchi yoyote inayoendelea ambazo zinaweza kuweka matatani maslahi ya kampuni hiyo kubwa ya madini. Kile ambacho Barrick inataka, Barrick inapata.

Kwa kuangalia ukweli huo basi ni wazi kuwa kikwazo kikubwa cha mabadiliko katika sekta ya madini itakuwa ni kampuni hiyo kwani wao wakigoma hakuna kitakachofanyika. Ndiyo maana kutokana na pembetatu hiyo ilikuwa ni rahisi kuishawishi kampuni hiyo kubadili baadhi ya vipengele vya mikataba yake kiasi cha kwamba walikuwa ni wa kwanza kutangaza “kukubali” mapendekezo ya Serikali (ambayo wao wana uhusiano wa karibu nao).

Pembetatu hii kwa hakika imesababisha Watanzania walie sana mwaka huu unaoisha na sitashangaa wakawa tena sababu ya machozi zaidi mwaka ujao. Rais Kikwete hana ubavu wa kusimama mbele ya kampuni kubwa kama hii hata kama atapata ushirikiano kutoka kwa wananchi. Barrick imekuwa ikitamalaki sehemu mbalimbali duniani licha ya pingamizi toka kwa watu mbalimbali.

Ndiyo maana watu kama kina Tundu Lissu wanavyojitahidi kupambana na kampuni hii wanakuwa wamejiweka katika kundi la kushindwa. Tundu Lissu hana ubavu wa kupambana na kampuni iliyozungukwa na pembetatu hii. Kamati ya Madini ya Bomani haina ubavu huo pia kwani haina nguvu zozote na Rais Kikwete alijua ni kwa nini hakutaka iundwe kamati Teule ya Bunge isipokuwa kamati ya ushauri tu; ushauri ambao watekelezaji wake wakubwa watakuwa ni Barrick Gold.

Ni kwa sababu hiyo basi yeyote ambaye amekaa kwa moyo wa matumaini kuwa kuna mabadiliko makubwa katika sekta ya madini huko tunakokwenda yuko njozini. Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana hadi leo Serikali imeshindwa kutoa hadharani ripoti za Dk. Kipokola, Mang’enya, Jenerali Robert Mboma na Laurence Masha.

Kwa sababu mapendekezo hayo hayakukubaliwa na “wakubwa”. Hata mapendekezo ya kamati ya kina Zitto ambayo ninaamini yatakuwa mazuri sana yatatupwa nje kama takataka chafu kwani Barrick haiwezi kufanya katika Tanzania kile ambacho imekataa kufanya nchi nyingine.

Niandikie: lulawanzela@yahoo.co.uk
 
Unajua mimi nikiwa nasoma vitu kama hivi huwa naumia sana, mbaya zaidi sina cha kufanya, hivi kwa nini hii nchi isipinduliwe tu halafu iendeshwe kijeshi, hawa wazee wote walio kwenye system watolewe halafu hayo makampuni yote yafukuzwe, then tuanzie hapo. May be i am dreaming. Ila ipo siku
 

watu walishafikiria sana mambo kama hayo,Mdogo wangu Judy punguza munkari,Mapambano ya kifikra yamekaribia kufika tamati,Naamini tutashinda .
 
Judy you're right. Si unaona hata Zaire ilivyofanyika. Watanzania tuwe majasiri, vinginevyo tutaulizwa na wajukuu wetu kuwa "nchi ilipokuwa inaharibika tulikuwa wapi? Hakuna tusi kubwa kama hilo, ila litakuwa siyo tusi bali ukweli. TUAMKE JAMANI
 
huu ni ujinga kwa rais kushirikiana na watu kuhusu uchafu katika nchi , huyu sinclair alithubutu kusema wazi hakuna atakayemzuia asifanye kitu hapa TZ maana ni mshikaji wa kikwete na aliitwa maalum siku ya kuapishwa kwake.
hivi hawa wanaoipenda system ya kikwete wana akili timamu kweli?

mimi nashindwa kujizuia kuamini kuwa niko tayari kuvaa mabomu ya petroli kuwaangamiza wafisadi hawa.

naahidi iko siku mtu atasikia msafara wa kikwete umekula mzinga mbaya sana hasa kutokana na kumkanyaga mtu ambaye atakuwa mimi nyie subirini, bora nitangulie kuliko wote kuishi tena kwa shida namana hii.
 
watu walishafikiria sana mambo kama hayo,Mdogo wangu Judy punguza munkari,Mapambano ya kifikra yamekaribia kufika tamati,Naamini tutashinda .

Bora mapambano ya kifkra badala ya kupindua kwa kutumia majeshi maana walimtry mwalimu kifimbo 4 times wakaishia magereza.Vita iwe ni ya kudai haki kwa kutumia fikra.
 
Re: Chairman's Corner - Friday, May 30, 2008
Title: Changes to Tanzanian Mining Law Certain
to Benefit Mineral Explorers
Author: Jim Sinclair

Dear Friends:

President Jakaya Kikwete of Tanzania formed a
committee last year to review the country's Mining
Law. This body has a name that describes its mission
and limitations: "The Presidential Committee to
Review and Advise Government on Management of the
Mineral Sector."

I've had the privilege of reviewing the Committee's
recommendations - along with comments from the
Chamber of Mines - and have no serious issues with
them. What's important to know, however, is that the
man who will make the final decision on the
recommendations is the President - not the
Committee.

President Kikwete is an extremely knowledgeable and
capable man who will do nothing to disturb the
balanced fiscal policies that have produced enormous
growth in Tanzania's economic base, most of it
fueled by international investors.

There is one recommendation put forth by the
Committee that is very intriguing: "The policy
should direct most of the incentives to mineral
exploration and not to mining."

There is no question in my mind that the Committee's
recommendations are focused on improving the
conditions and privileges of exploration companies
who through the discovery process produce new wealth
for the country and its citizens.

Regards,

Jim Sinclair
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…