Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Kifupi ni kwamba Sinclair ni hussler sasa katukuta tumelala au niseme kawakuta viongozi wetu wamelala, Mungu ampe nini tena... na mnajua ile methali ya "alalaye usimwamshe..." kwa hiyo mpaka tutakapoamka wenyewe yeye ataendelea kugegeda vya kwetu... inauma lakini ndio ukweli wenyewe huo!
Mkuu Rwabugiri hapo unaulizia samaki feri...Hivi dharau kiasi gani Sinclair unadiriki kusema eti wasiwe na wasi wasi mwenye maamzi ya mwisho si kamati bali ni raisi JK? una taka kutueleza nini? kwamba Jk yuko kiganjani kwako? ama kila usemacho wewe ndicho atatenda??
JK akisoma hayo maneno ya Sinclair anaona kamwagiwa sifa kweli, yeye ndio mwamuzi wa mwisho, ndio mwenye mamlaka, haoni dharau mwenzio anaona mbia wake anajigonga...JK, kwanini uruhusu mtu akudharau kiasi hichi??
Katika yote nachukizwa na dharau ya sinclair kwa Kikwete! sijui JK haoni hili? si bora kubaki masikini kuliko kufedheheshwa?
Lakini kwa upande mwingine, kuna ubaya gani kwa rahisi kuzungumza na marafiki zake na kupenyeza habari fulani kwao ili kuwaondoa wasiwasi....? Labda jamaa alikuwa na wasiwasi kuwa mabadiliko makubwa yako njiani na akaamua kuwahhi kupata neno la Rais...