James Sinclair: A Friend or Foe?

James Sinclair: A Friend or Foe?

mimi kilichonichosha ni kuwa yeye kaweza kuona mapendekezo yote hayo na kuhakikishiwa kuwa asiiwe na wasiwasi kwani mwenye uamuzi wa mwisho ni "Rais na si Kamati" whichi is true na ndipo mazingaombwe yanapolala.
 
Haya Ya Sinclair Na Kampuni Zake Ni Ya Aibu Hata Kuyasoma Tu. Kweli Wadanganyika Tumefikishwa Hapa????????????!!!!!!!!!!
 
Kifupi ni kwamba Sinclair ni hussler sasa katukuta tumelala au niseme kawakuta viongozi wetu wamelala, Mungu ampe nini tena... na mnajua ile methali ya "alalaye usimwamshe..." kwa hiyo mpaka tutakapoamka wenyewe yeye ataendelea kugegeda vya kwetu... inauma lakini ndio ukweli wenyewe huo!
 
Ningependa kufahamu historia ya mizani ya magari tanzania ilianza lini na kwa madhumuni gani?Halafu nani haswa anapaswa mwangalizi wa mizani hizi
 
Kifupi ni kwamba Sinclair ni hussler sasa katukuta tumelala au niseme kawakuta viongozi wetu wamelala, Mungu ampe nini tena... na mnajua ile methali ya "alalaye usimwamshe..." kwa hiyo mpaka tutakapoamka wenyewe yeye ataendelea kugegeda vya kwetu... inauma lakini ndio ukweli wenyewe huo!

Nimechukia sana! grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr!!!

Nachukia sana mtu mwenye daharau kubwa kiasi hiki, kwa kiongozi mwenye mamlaka ya kuongoza nchi, yaani raisi wangu kikwete, Hivi dharau kiasi gani Sinclair unadiriki kusema eti wasiwe na wasi wasi mwenye maamzi ya mwisho si kamati bali ni raisi JK? una taka kutueleza nini? kwamba Jk yuko kiganjani kwako? ama kila usemacho wewe ndicho atatenda??

JK, kwanini uruhusu mtu akudharau kiasi hichi?? do the needful please!
 
Hivi dharau kiasi gani Sinclair unadiriki kusema eti wasiwe na wasi wasi mwenye maamzi ya mwisho si kamati bali ni raisi JK? una taka kutueleza nini? kwamba Jk yuko kiganjani kwako? ama kila usemacho wewe ndicho atatenda??
Mkuu Rwabugiri hapo unaulizia samaki feri...

JK, kwanini uruhusu mtu akudharau kiasi hichi??
JK akisoma hayo maneno ya Sinclair anaona kamwagiwa sifa kweli, yeye ndio mwamuzi wa mwisho, ndio mwenye mamlaka, haoni dharau mwenzio anaona mbia wake anajigonga...
 
Lakini maneno ya Sinclair yana ukweli ndio maana hawakuta kuunda Kamati Teule ya Bunge wakaamua kuunda ya Rais..!
 
Uswahiba huu wa Rais Kikwete na Bw. Sinclair!

Lula wa Ndali-Mwananzela Juni 4, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

KUNA tabia imeanza kuzoeleka na ambayo kwa hakika haina budi kukemewa, kubezwa, kupingwa, na kukataliwa na kila Mtanzania mwenye kupenda utawala wa uwazi na ushirikishwaji wa wananchi katika mjadala wa taifa lao.

Tabia hiyo ni ile ya wageni a.k.a. Wazungu kupata nafasi ya kujua kinachoendelea ndani ya serikali yetu kuliko sisi raia wenyewe - ni tabia ya ajabu na ya kushangaza.

Sijui ni kitu gani kinaashiriwa pale ambapo Watanzania wanahangaika kupata taarifa kutoka asasi mbalimbali lakini wageni tena wakiwa mbali kabisa wanaonekana kupata habari za ndani kabisa ya nyumba yetu wakati wenyewe wenyeji tukiwa tumekaa nje na vikamera vyetu na rekoda kusubiri habari hizo hizo.

Wiki iliyopita nilishangazwa na kitendo cha Benki Kuu kuwakataza waandishi kuingia eneo la Benki Kuu kufuatilia ziara ya Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi iliyokuwa inatembelea Benki Kuu. Kwa asasi ambayo imegubikwa na kashfa za upotevu wa mabilioni ya shilingi kuanza tena kitendo cha usiri hakiwasaidii bali zaidi kinaonesha ni jinsi gani uongozi wa benki hiyo bado umekita kwenye kiburi.

Hivi hizo fedha wanazozizungumzia ni za nchi gani? Na hii benki inaitwa Benki Kuu ya Taifa gani? Sasa iweje hawa ndugu zetu wanapojadili fedha za nchi yetu kwa kutumia chombo cha Bunge la Taifa letu, kwanini sisi wenye fedha hizo hatutakiwi kusikia wanachozungumza?

Benki Kuu ni benki ya Watanzania na kuna mambo yanatakiwa kuwa ya siri lakini suala la chombo cha wawakilishi wa wananchi kufanya mikutano kwa siri ni kitendo cha kupingwa kabisa na kulaaniwa. Prof. Ndullu ujumbe wangu kwako ni kuwa fungueni milango ya Benki Kuu ili hewa ya uwazi na ukweli (siyo kama wa Mkapa) ianze kuingia ili usiri uliozoeleka upotee daima.

Lakini cha kushangaza mambo ambayo Watanzania wanafichwa yatakuja kujitokeza kwa wageni, na hili ndilo linalonisumbua hasa.

Iweje Watanzania tuwe watu wa mwisho kujua nini kinaendelea katika utawala wa nchi yetu? Kwanini tuwe wa mwisho kujua kinachoendelea na inapotokea kujua inakuwa hadi watu wa nje watuambie? Nitakupa mifano.

Suala la ununuzi wa rada lilianza kutajwa na vyombo vya kigeni hasa lilipoanza kujadiliwa katika Bunge la Uingereza. Wakati Bunge letu likijiweka pembeni kabisa na kugoma kuliangalia jambo hili kwa ukaribu, Waingereza wakiwa na uchungu na fedha zao wakalivalia njuga suala hili. Si wao tu; bali hata mashirika yasiyo ya kiserikali kama Oxfam yalianza kupigia kelele ununuzi wa rada hii kabla yetu.

Ilikuwaje Wazungu wenye kutuuzia rada wajue kabla ya sisi wanunuzi kujulishwa? Kinachoshangaza ni pale ilipogundulika kuwa mpango wa kununua hii rada ulianza tangu enzi za Mwinyi! Sasa inakuwaje Watanzania tuje kufahamu dakika za mwisho? Inakuwa kama vile viongozi wetu walikuwa wanatununulia zawadi ya kutushangaza nayo.

Nakumbuka Prof. Lipumba (Mwenyekiti wa CUF) alikuwa ni miongoni mwa watu walioashangazwa na jinsi gani ni ripoti za kikao cha Bunge la Uingereza ndicho kilichotujulisha kile kilichokuwa kinaendelea.

Mfano mwingine ni jambo linalotokana na uchunguzi huu wa rada ambapo wiki chache zilizopita tumesikia kuwa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu anachunguzwa na asasi ya SFO ya Uingereza kuhusiana na madai ya rushwa katika mchakato wa ununuzi wa rada hiyo.

Cha kushangaza ni kuwa wengi wetu tulisikia juu ya Chenge kuchunguzwa baada ya ripoti iliyoandikwa kwenye gazeti la The Guardian la Unigereza. Kwanini Waingereza walijua kwanza kuhusu Chenge na sisi kudokezwa baadaye?

Kama hilo halitoshi ni pale ambapo habari ya mtuhumiwa mkuu wa sakata hilo Bw. Vithlani alipotajwa na gazeti hilo hilo kudaiwa kupokea karibu shilingi bilioni 21 kama malipo ya udalali wake. Inakuwaje wageni wajue wahusika wa mambo yanayolihusu taifa letu na vyombo vyetu vya habari ndivyo vinajikuta vinarudia majina hayo kama kasuku?

Kwanini inakuwa vigumu kwa waandishi na vyombo vyetu vya ndani kupata taarifa lakini wakija hawa Wazungu na kimombo chao milango inafunguliwa kama mlango wa nyumba ya mlevi?

Lakini kilele cha wageni kupata taarifa za ndani za mambo ya taifa letu kimetokea wiki iliyopita mara baada ya Rais Kikwete kukabidhiwa ripoti ya Kamati ya Rais ya Ushauri kuhusu Sekta ya Madini. Wakati Watanzania wanasubiri kusikia kilichomo ndani ya ripoti hiyo na kama yaliyopendekezwa yatafanyiwa kazi, huwezi kuamini ni nani amejitokeza kudai kuwa ameona yote yaliyopendekezwa, tena mtu mwenyewe yuko Marekani! Nitakukumbusha.

Desemba 19, mwaka jana, niliandika makala kwenye gazeti hili nikizungumzia “Pembetatu ya Machozi”. Katika makala hiyo nilimtaja mtu mmoja ambaye kila Mtanzania kuanzia sasa anapaswa kulijua jina lake kama anavyolijua jina la Chenge au Lowassa, au Bangusilo! Si mwingine bali ni James Sinclair. James Sinclair ni rafiki wa karibu wa Rais Kikwete na urafiki wao msingi wake tangu mwanzo ulikuwa madini.

Bw. Sinclair na binti yake waliingia nchini miaka ya mwanzo ya tisini na akaanzisha urafiki wa karibu na aliyekuwa Waziri wa Madini wa wakati huo Bw. Jakaya Kikwete. Ni urafiki ambao umekuwa wa kudumu na sitoshangaa kama nikisikia siku moja kwamba Kikwete, au familia yake ya karibu, wanakuwa na hisa ya aina fulani katika makampuni ya Sinclair.

Kilele cha urafiki huu kilikuja pale ambapo Bw. Sinclair alikuwa ni mmoja wa wageni rasmi wa Kikwete walioalikwa siku ya kuapishwa kwake na yeye mwenyewe (Sinclair) amekuwa akibeba bango la “Urafiki na Kikwete” kila aendapo na anazungumza kana kwamba na yeye ana ka-ubia katika urais wa Kikwete na hasa kwenye sekta ya madini.

Ni vipi Sinclair anazipata mapema habari nyeti kuhusu sekta ya madini ambazo Mtanzania wa Maneromango, au Kigonsera au wa Itumba hawezi kuzipata mapema?

Ijumaa iliyopita Bw. Sinclair aliandika waraka wake wa kila Ijumaa kwa wanahisa wake na katika waraka huo alioupa kichwa cha habari “Mabadiliko sheria ya madini hakika kunufaisha watafutaji wa madini”, anawatuliza wanahisa hao kuwa wasiwe na wasiwasi na mapendekezo ya Kamati ya Bomani.

Katika barua yake hiyo Bw. Sinclair anawaandikia wanahisa hao na kuwaambia pasipo kigugumizi chochote kile “Nimepata nafasi ya kupitia mapendekezo ya kamati hiyo pamoja na mapendekezo ya wadau wa madini na sina matatizo nayo makubwa” (kana kwamba angekuwa nayo angepinga).

Lakini kilichonichefua mwenzenu ni maneno yake hayo ambayo naamini atakuwa ameyasema pengine baada ya kuzungumza na swahiba wake Rais Kikwete. Sinclair aliendelea kuandika hivi “Jambo la kuzingatia ni kuwa mtu atakayefanya maamuzi ya mwisho kuhusu mapendekezo hayo ya Kamati ya Bomani ni Rais na si hiyo kamati”.

Binafsi naweza kuhisi kuwa wakati wa mazungumzo kati ya Rais Kikwete na Sinclair alimtoa wasiwasi Bw. Sinclair kuwa mapendekezo hayo hayataharibu shughuli za watafutaji madini. Na hilo linadhihirishwa na kile ambacho Bw. Sinclair anakijua kwani ananukuu kutoka mapendekezo hayo ambayo bado ni siri kwa Watanzania wenyewe.

Sinclair anaandika kwamba anafurahishwa na pale ambapo inapendekezwa “sera (mpya ya madini) itoe motisha kwa watafutaji madini (kina Sinclair) kuliko kwa wachimbaji”. Sasa tunaweza vipi kuamini kuwa hicho ndicho kilichopendekezwa wakati bado ripoti hiyo haijawekwa wazi kwa Watanzania?

Sasa hii si mara ya kwanza kwa Bw. Sinclair kudai kujua mambo yanayofanywa na serikali yetu kuhusu Sekta ya Madini. Ni hii access ya wageni katika habari za nchi yetu ndiyo jambo linalonisumbua sana.

Kama Watanzania hawajapata kuyaona hayo mapendekezo (ukiondoa wanakamati) iweje wageni wajue yanayoendelea na kutunukulia sisi? Ni lini tutambua kuwa wageni wako hapa kuchuma na kulinda maslahi yao, na siku mambo yakiharibika watatokomea makwao; wakati sisi tutabakia kubanana wenyewe kwa wenyewe hapa hapa.

Ombi langu kwa wanaohusika, kama mnatunyima Watanzania taarifa zinazohusu nchi yetu na mna haraka kutuambia tusubiri “uchunguzi” ufanyike au “serikali ipitie”, nadhani wakati umefika pia wa kuwanyima marafiki zenu habari za taifa letu na zile zinazohusu maslahi ya Watanzania.

Hatutaki tena kusikia sijui “fulani ana vijisenti Ulaya” na tunasikia kwenye magazeti ya “Wazungu”. Huu mtindo wa kuabudu na kupiga magoti kwenye altare ya Wazungu lazima uanze kukoma.

Ombi langu kwa Rais Kikwete; kwa vile rafiki yake James Sinclair amepata nafasi ya kupitia mapendekezo ya Kamati ya Madini na kuwatangazia wadau wake angalau jambo moja lililopendekezwa, tunaomba wiki hii na sisi wananchi wenzake na raia wenzake, tuone mapendekezo hayo kwa yeye (Rais) kuruhusu yawekwe hadharani. Haiwezekani mgeni ajue kinachoendelea na sisi wengine tuendelee kusubiri.

Na hili linawahusu viongozi wengine ambao wana haraka ya kutoa habari kwa wageni lakini kwa sisi wenyewe hadi tushikane mashati. Kama ni vigumu kwenu kuwa wa wazi kwa wananchi wenzenu lakini mna haraka ya kuwaambia “kila kitu” wageni, basi, kwanini msiamue kuwapa uraia tu ili angalau tujue Watanzania wenzetu wamehabarishwa. Vinginevyo, kabla hamjawaambiwa wageni yanayohusu nyumba yetu, tuambieni kwanza wenye nyumba. Ni ushauri tu.

Niandikie: lulawanzela@yahoo.co.uk
 
Namkumbuka Nyerere kila kukicha... "Huyu jamaa ana mfuko mkubwa kiasi gani?"
 
Katika yote nachukizwa na dharau ya sinclair kwa Kikwete! sijui JK haoni hili? si bora kubaki masikini kuliko kufedheheshwa?
 
Katika yote nachukizwa na dharau ya sinclair kwa Kikwete! sijui JK haoni hili? si bora kubaki masikini kuliko kufedheheshwa?

Unajua inawezekana JK alimwambia mshirika wake in confidence jamaa akaenda kumwaga mtama..
 
Ndio maana ipo haja ya kukubali hoja ya CHADEMA kuhusu utawala wa majimbo, haiwezekani mtu au watu wachache wanauza ardhi yetu kijinga jinga tu, halafu anayemiliki yuko nje ya nchi.

Utawala wa majimbo utatoa mamlaka kwa watu kuwa na usemi juu ya ardhi yao!

NA ATARUDISHA ARDHI YETU APENDE ASIPENDE, HAPA HAKUNA CHA SINCLAIR AU
KIKWETE, LAZIMA ARDHI IRUDI, NI SUALA LA MUDA TU!!
 
Lakini kwa upande mwingine, kuna ubaya gani kwa rahisi kuzungumza na marafiki zake na kupenyeza habari fulani kwao ili kuwaondoa wasiwasi....? Labda jamaa alikuwa na wasiwasi kuwa mabadiliko makubwa yako njiani na akaamua kuwahhi kupata neno la Rais...
 
Lakini kwa upande mwingine, kuna ubaya gani kwa rahisi kuzungumza na marafiki zake na kupenyeza habari fulani kwao ili kuwaondoa wasiwasi....? Labda jamaa alikuwa na wasiwasi kuwa mabadiliko makubwa yako njiani na akaamua kuwahhi kupata neno la Rais...

Rais anatakiwa aanze kutuondoa sisi wasiwasi kabla ya kuwatuliza rafiki zake wa nje. Kinyume na hivyo, ni kukiuka kiapo chake cha uaminifu kwa Jamhuri.

Ni kutokuheshimu Katiba!

Halafu ingekuwa ni nchi za watu, access access na Rais kama hizo huwa zinachukiwa. Huwezi kujadili pembeni pembeni habari za mambo ya Kitaifa na rafiki zako ambao wana masilahi kuhusu jambo hilo hilo. Haileti picha nzuri.

Ndio haya juzi tuliyajadili, swala la Maadili ya Conflict of Interest, nikasema ni mambo mapya kwetu. Labda utakubaliana na mimi kwamba, japo hapa haijavunjwa sheria, ule msingi wa Conflict of Interest, ile "roho" ya ile sheria, ule uelewa wa kuepuka taswira ya ufisadi, umevunjwa na Rais. Hii ni concept ngeni mno kwetu.
 
Huyu jamaa ana free pass pale Ikulu. Majasusi wangu wamenitonya kuwa kila mara anapotinga Dar hufanya kikao cha chemba kati yake, JK na Joseph Kahama.
 
Ukichagua kiongozi mnafiki ndio matokeo yake hayo.
 
Tan Range established its presence in Tanzania in 1993. Today, it holds over 70 prospecting and reconnaissance licenses totaling some 3800 square kilometers. Over the past decade, the Lake Victoria greenstone belts of Tanzania have evolved as one of the best regions in the world to host gold deposits greater than 3 to 4 million ounces (considered the minimum threshold to attract the senior gold producers). Tan Range is well focused and well positioned in this gold-rich region of East Africa.

Mr. Sinclair provides Tan Range with the strategy for its corporate growth and is primarily responsible for providing the leadership necessary for the Company to complete its evolution into a gold royalty company.

Mr. Sinclair became Chairman of Tan Range following a Special Meeting of Shareholders held in April 2002 in which shareholders voted 98% in favor to approve a transaction for Tan Range to acquire Tanzania American International Development Corporation 2000 Limited, a Tanzanian gold exploration company controlled by the Sinclair family.

Mr. Sinclair is primarily a precious metals specialist and a commodities and foreign currency trader. His past experience includes that of founder of the Sinclair Group of Companies (1977), which offered full brokerage services in stocks, bonds, and other investment vehicles. The companies, which operated branches in New York, Kansas City, Toronto, Chicago, London and Geneva, were sold in 1983. Mr. Sinclair served as a Precious Metal Advisor to Hunt Oil and the Hunt family from 1981 to 1984 for the liquidation of their silver position as a prerequisite for the $1 billion loan arranged by the Chairman of the Federal Reserve, Paul Volcker. Mr. Sinclair was a general partner and member of the executive committee of two New York Stock Exchange firms and also President of Sinclair Global Clearing Corporation (Commodity clearing firm) and Global Arbitrage (derivative dealer in metals and currencies). Mr. Sinclair was President of James Sinclair Financial Research SARL in Luxembourg. Mr. Sinclair held the position of Chairman of Sutton Resources from 1989 to 1995.

Jim Sinclair is the author of numerous magazine articles and three books, which deal with a variety of investment subjects, including precious metals, trading strategies and geopolitical events and their relationship to world economics and the markets.

Expert Contact Information
James E. Sinclair, Chairman & CEO
Tan Range Exploration Corporation
93 Benton Hill Road
Sharon, CT 06069 USA

860.364.1830 Tel
860.364.0673 Fax
www.tanrange.com
 
Actually nimegundua kua tanrange na tanzania royalty exploration is the same company!
 
Back
Top Bottom