James Sinclair: A Friend or Foe?

tatizo wanatudhoofisha sana hawa jamaa ndo maana tunakata tamaa baada ya kuona wapigania haki wanavyotendewa.

Mkuu

Mapambano ya kubadisha mifumo ya kiutawala huwa siyo rahisi, kumbuka usemi wa Anna Kilango. Siyo wote wapambanao ufika mwisho.
 
Kwani uwanja wa ndege ndani ya Serengeti umesha anza kujengwa?

Umeshamalizika. Tunangoja tu ndege ya mheshimiwa itue kule kuufungua rasmi. Pia mwulizeni ana uhusiano gani na jamaa mmoja Mmarekani anaitwa Tudor. Huyu ana hotel ya 5 stars katikati ya Serengeti. Na kule raia wazalendo wamepigwa marufuku kuvinjari.
 
Inategemea kama tuna mpango wa kuamka au tunasubiri tuamshwe.. maana kuna wengine wakilala fofofo hata treni lipite juu ya nyumba yao hawawezi kuamka.
 

Mhh Mwanakijiji wewe!!


RaiaMwema wamekuwa wema kweli
 
Umeshamalizika. Tunangoja tu ndege ya mheshimiwa itue kule kuufungua rasmi. Pia mwulizeni ana uhusiano gani na jamaa mmoja Mmarekani anaitwa Tudor. Huyu ana hotel ya 5 stars katikati ya Serengeti. Na kule raia wazalendo wamepigwa marufuku kuvinjari.

Hivi kumbe na yeye ameisha kuwa mfanyabiashara mashuhuri alisema tofautishaneni biashara na kazi halafu ndiye anakuwa wa kwanza, wengine watafanyaje?

Hii nafikiri inatakiwa iende mbali hili 2010, aweze kupashwa. Miaka mitatu tu?
 
Miye nimeaiweka tu kwenye PDF na kuedit kidogo.. lakini barua hiyo ni ufundi na wazo la ndugu yetu Kuhani Mkuu... ndiye mwenye kustahli kudos zote. Si mimi, si mimi!
 
Hi Kuhani.

Jambo linaelekea kuwa jambo. Karibu linawiva ..tutaepua..tutakaa mezani..tutasheherekea..Tanzania ..tanzania..nakupenda... Nimesoma kwenye Raia mwema ....amesikia kilio chetu..kama ilivyokuwa kwenye ile thered yako..ilituliyoanzia.. chimbuko.

I hope vyombo vingine vya habari havitalaza damu.

Gazeti ambalo hawataitoa hii barua ..tutawahesabu ..kutusaliti. Why not?

Wasiitoe hii na comment fresh...watatoa ipi?

Good work Raia mwema.

Good work Kuhani Mkuu

Good work MMK

Nisisahau... and I am not Jocking. Huu Ni mtizamo wa Uma wa Kitanzania..hapa ni kwa niaba!

Kwa wabunge....Mmeanza kikao ..make sure hamfanyi mzaha ndani ya ile nyumba...Barua hiyo someni..na mchukue hatua stahili, vinginevyo hatutaelewana.

Viongozi wakuu wa Taifa la Tanzania na Mawaziri...Mkitaka tuelewane,tuheshimiane na kuwa marafiki wa watanzania na kuishi salama kwenye Nchi yetu..hii ya upendo na utu..tuliyopewa na Mungu....,

Please stop deal daling na DHAMANA tuliyowapeni..fanyeni kazi...Wacheni ubinafsi, wacheni porojo, mnaona dunia inavyokwenda...Mafuta ..chakula..etc havishikiki...Tumeieni dhamna zenu ipasavyo...Mambo yakiwa magumu..bado tunawaamini..do your best.

Tuna macho na akili sahihi za kumuona anaye jitahidi na mkweli...Lakini hatutakuwa na simile na ambaye ataendelea kutufanyia mzaha.

Nafiki tumeelewana.

Get Back to the line. Fanyieni kweli vile viapo vyenu.

Be seriouse and much more important..kuweni makini na MARAFIKI wa ndani na wa Nje ya nchi...Marafiki wengine wanatutia aibu..kwa viburi vyao na kiu ya kulitafuna Taifa huku wananchi wakinyauka kwa "jua kali" Nafikiri nimejiweka wazi na kueleweka vema.

Mungu Ibariki tanzania ...na viongozi wake.
 
Azimio.. una maana ile makala ya leo au unazungumzia ile ya Lula ya wiki iliyopita kwenye Raia Mwema.. maana nimeangalia Raia mwema na halipo mtandaoni.
 
Azimio.. una maana ile makala ya leo au unazungumzia ile ya Lula ya wiki iliyopita kwenye Raia Mwema.. maana nimeangalia Raia mwema na halipo mtandaoni.

Kwani leo kuna makala mpya ya Sinclair kwenye Raia Mwema? Naona hakuna toleo jipya la gazeti zaidi ya lile lenye picha ya Ballali juu na makala ya Lula Wa Ndali.

Kuna nyingine kwenye gazeti lolote?

Na unaonaje katika moja ya Makala zako siku za karibuni uongelee hili swala kirefu? Manake ukisoma makala ya Lula Wa Ndali imeongelea Mkuu wa Kaya alivyovujisha ripoti yake kwa Sinclair, lakini haijagusia lile dokezo la Sinclair kwa Rais kwamba hayo yaliyosemwa na Commissioners kwenye ripoti asiyasikilize! Na hilo ndilo baya.
 
Pundit you are right hata mimi nimeshindwa kuifungia wajameni na sijui nasadiwaje hapa. Hata hivyo mwanakijiji ubarikiwe sana kwa kazi yako nzuri.
 
Pundit you are right hata mimi nimeshindwa kuifungia wajameni na sijui nasadiwaje hapa. Hata hivyo mwanakijiji ubarikiwe sana kwa kazi yako nzuri.


Tunatakiwa kiweka online kama link na kuweka maneno kama "If you have trouble opening the attachment click here"

However paranoia ya virus prone pranks inaweza ku play I might add.
 
Kuhani Mkuu na MJJ asnteni kwa kazi yenu hiyo nzuri tunahitaji watu kama nyie......Bob Woodward alimuangusha Nixon sembuse....
 
... hata mimi nimeshindwa kuifungia wajameni na sijui nasadiwaje hapa.

Una PDF reader?

Kuna wakati Adobe PDF reader ikichengua ni vyema kui uninstall na kuinstall upya. Kabla huja uninstall hakikisha ume download program mpya (pata the latest, Adobe PDF reader 8.1).

Kawaida sio lazima ku uninstall ya zamani unapokuwa unafanya program version update, lakini kama ilikuwa inachengua ina maana ishaanza kuwa blotted. Ifutilie mbali (uninstall, not delete files) na uanze upya na program mpya (adobe PDF reader 8.1)
 

Kwa wengine unaweza kuwa unaongea kigiriki kama si kichina.

On top of your suggestions, kwa wale watakaoona kichina

Kwa nini isipigwe kwenye website (KLH News for example) na kuwapa watu wenye matatizo ya kuifungua option ya kuifungua kwenye browser via a URL link?
 
Watanzania wamjia juu swahiba wa Kikwete

Mwandishi Wetu Juni 11, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

WATANZANIA kadhaa wamejitokeza na kumshutumu rafiki wa karibu wa Rais Jakaya Kikwete, ambaye ni mwekezaji katika sekta ya madini, James Sinclair, kwa kuanika hadharani kwa wawekezaji wenzake, ripoti ya Kamati ya Rais ya Madini ambayo bado ni siri.

Wananchi kadhaa wamekuwa wakipiga simu katika ofisi za gazeti hili na kueleza kushangazwa kwao na hatua ya Bw. Sinclair kuweka hadharani yale yaliyomo katika ripoti hiyo ikiwa ni siku chache tu baada ya Rais Kikwete kukabidhiwa ripoti hiyo.

Gazeti hili liliripoti katika moja ya safu zake, toleo lililopita, kwamba Bw. Sinclair ameandika waraka na kuuweka katika tovuti ya kampuni yake akiwaeleza wawekezaji wenzake katika sekta ya madini Tanzania kwamba amefanikiwa kuisoma ripoti hiyo ambayo bado ni ya siri, na kwamba ina mambo ambayo ni ya manufaa kwao.

Aidha, kufuatia taarifa iliyomo kwenye safu hiyo ya Raia Mwema ya Lula wa Nzela Mwananzela, mtandao wa JamiiForums.com ambao mwanzoni ulikuwa unajulikana kama Jambo Forums, ulianzisha kampeni kamambe ya kumtaka Bw. Sinclair kuacha kutoa siri za serikali kwa kuweka hadharani mambo ambayo hata Watanzania wenyewe hawajapata nafasi ya kuyajua.

Mpaka sasa haifahamiki ni vipi Bw. Sinclair aliweza kuiona ripoti hiyo ya Kamati ya Rais ya Madini ambayo bado ni siri, na pia kwa nini aliamua kueleza yaliyomo kwenye ripoti hiyo katika ovuti ya kampuni yake wakati akijua kuwa bado ripoti hiyo ni siri.

Kampeni hiyo ya JamiiForums ilianza wiki iliyopita baada ya makala hiyo ya Lula kufunua waraka wa Bw. Sinclair kwa wanahisa wa kampuni yake kuhusu mapendekezo ya Kamati hiyo ya Madini iliyoongozwa na Jaji Bomani.

Katika waraka huo wa Mei 30, wiki moja tu tangu Rais Kikwete kukabidhiwa ripoti hiyo, Bw. Sinclair anadai kwa ujasiri wote kuwa amepata kuyaona mapendekezo ya Kamati hiyo na maoni ya Chemba ya Biashara ya Tanzania na kuona kuwa yatawanufaisha watafutaji wa madini wanaolipwa kwa mrabaha kama yeye.

Katika waraka huo ulioandikwa kwa Kiingereza, Sinclair anasema hivi: "Wapendwa rafiki,…Mwaka jana Rais Kikwete wa Tanzania aliunda Kamati kupitia sheria ya Madini.

Kamati hiyo ambayo ilipewa jina linaloashiria majukumu na mipaka yake, ilijulikana kama "Kamati ya Rais ya Kupitia na Kuishauri Serikali Kuhusu Usimamizi wa Sekta ya Madini"

Nimepata nafasi ya kupitia mapendekezo ya Kamati hiyo – pamoja na maoni ya Baraza la Madini – na sina matatizo makubwa nayo. Hata hivyo, jambo la muhimu kujua ni kuwa uamuzi wa mwisho wa mapendekezo hayo uko kwa rais – na si Kamati.

Rais Kikwete ana ufahamu na uwezo mkubwa na hatafanya jambo lolote ambalo linaweza kuvuruga uwiano wa sera za kusisimua uchumi na matumizi ya Serikali ambazo zimesababisha ukuaji mkubwa wa msingi wa uchumi wa Tanzania, ukuaji ambao kwa kiasi kikubwa umetokana na wawekezaji wa kimataifa.

Kuna pendekezo moja lililotolewa ambalo limenivutia, linasema ‘sera (mpya ya madini) ielekeze kutoa manufaa kwa watafutaji wa madini (kama Sinclair) na si kwa wachimbaji.'

Sina shaka mawazoni mwangu kuwa mapendekezo ya Kamati hiyo yana lengo la kuboresha mazingira na faida kwa makampuni ya utafutaji (kama ya kwake) ambayo kwa ugunduzi wake wanaleta utajiri mpya kwa taifa na wananchi wake."

Baada ya yaliyomo kwenye barua hiyo kuanikwa na Raia Mwema ndipo wanachama wa JamiiForums, mtandao ambao ni maarufu duniani kwa wazungumzaji wa Kiswahili, walipoandika barua ambayo wamekuwa wakiisambaza kwa vyombo mbalimbali vya habari duniani, wadau wa mambo ya kiuchumi na kwa Sinclair mwenyewe, kumtaka aombe radhi kwa kutoa nje siri za Serikali.

Barua hiyo ya Watanzania hao inaonyesha ni jinsi gani wanajihisi kudharauliwa na kutendwa vibaya na wawekezaji wageni ikizingatiwa kuwa suala la madini ni jambo nyeti nchini.

Aidha Watanzania sehemu mbalimbali nao walijitokeza kueleza hisia zao kuhusu suala hilo. "Inawezekana alichofanya Bw. Sinclair ni kuingilia ununuzi wa hisa kwa kampuni yake kwa kuwapa habari za ndani (inside trading) wawekezaji wake; hasa kwa kuwahakikishia kuwa hakuna mabadiliko makubwa yatakayo vuruga kazi za kampuni yake", alisema mtaalamu mmoja wa masuala ya fedha anayeishi Dallas, Marekani.

Hakuna taarifa yoyote, ama ya Sinclair mwenyewe au ya Serikali iliyokwisha kutolewa kuhusu hatua hiyo ya mwekezaji huyo. Baadhi ya Watanzania waliochangia wamesema wanatarajia Bunge lifanye kama lilivyofanya wakati wa tukio la sinema ya "Mapanki "ya Hubert Sauper.

" Natumaini wabunge wenzangu wataonyesha mshikamano na kumkemea Sinclair kwa kitendo chake hicho cha kudhalilisha nchi yetu kama tulivyofanya kwenye suala la mapanki, " alisema mbunge mmoja aliyekuwa anajiandaa kwenda Dodoma kwenye kikao cha bajeti.

Rais Kikwete na Sinclair ni marafiki wa muda mrefu, yapata takribani miaka 20. Sinclair alikuwa akimiliki kampuni ya madini ya Sutton Resources aliyoiuza baadaye.

Moja ya ripoti zilizopatikana inasema Sutton Resources ilikuwa na kampuni tanzu, Kahama Mining Corporation Ltd., ambayo Agosti 5, 1994 iliingia mkataba na Serikali ulioonyesha wazi kwamba ulikuwa unahusu eneo la Butobela, Wilaya ya Geita, Mwanza.

Agosti mwaka 1996 Kahama Mining Corporation iliingia eneo la Bulyanhulu, Wilaya ya Kahama, Shinyanga na kuwaondosha wachimbaji wadogo wadogo takriban laki nne waliokuwa wakiishi na kuchimba dhahabu katika eneo hilo.

Baadaye, Sutton Resources iliiuza Kahama Mining Corporation na Bulyanhulu kwa Kampuni ya Dhahabu ya Barrick Gold Corporation ya Toronto, Canada kwa dola za Marekani milioni 280. Leo Bulyanhulu ni moja ya migodi tajiri kwa dhahabu katika Bara la Afrika.

Kampuni hiyo ya Barrick Gold ndiyo ambayo ilihusika kwa kuchangia mtaji katika uanzishwaji wa kampuni mpya ya Tanzania Royalties Exploration ambayo inaongozwa na Sinclair na wana makubaliano maalumu ya utendaji wa kazi zao. Na uhusiano huu pia unadaiwa kuonekana kwenye mkutano ulioisha juzi huko Arusha wa Sullivan ambao Mkuu wake Balozi Andrew Young ni mwanabodi katika kampuni hiyo ya Barrick.

Barua hiyo ya Watanzania kuhusu Sinclair inaweza kupatikana kwenye mtandao huo wa JamiiForums.com au kwenye mtandao wa habari wa Klhnews.com ambapo watanzania wameombwa kuichukua na kuituma katika barua pepe kadhaa ili kuonyesha kuchukizwa na kukerwa kwao na kitendo hicho cha Sinclair.
 

Wakome!

Washindwe na walegee!
 
Tutazidi kukandamiza hapo hapo na kusugua hadi JK na Sinclair watueleze .Kama walipeana Urais kwa mgongo wa kuwatetea wanyonge basi kitaeleweka .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…