James Sinclair: A Friend or Foe?

James Sinclair: A Friend or Foe?

Sidhani kama Sinclair anastahili kuchukuliwa hatua! Kwani yeye (Sinclair) amepewa hiyo ripoti na rafiki yake (Rais, JK)! Sasa tatizo la Sinclair lipo wapi?

Wa kuchukuliwa hatua ni Rais (JK), kama sio yeye basi Ofisi ya Rais. Kwani wameweza kuonyesha kuwa wananchi (waTZ) hawana thamani zaidi ya wawekezaji marafiki wa Rais!

Cha kufanya ni kumuomba Rais yeye mwenyewe alitolee kauri suala hili!
 
Huyu Heyo anazeeka vibaya sana.Yaani huyu Sinclair ainunue hii report(maana na uhakika hajaipata bure bila kitu kidogo!) halafu wamuajibishe?Unachekesha wewe babu.Wakumuwajibisha ni huyo baba lao ambaye haishi jipya kila leo.Ni kero tupu kazi kujichekesha kwa wazungu na kuitikia 'yes sir'
 
Kwanza awajibishe aliyemwezesha kabaila sinclair kupata hiyo ripoti na kufanya kazi iliyofanywa na kamati teule ya madini kuwa ya kujungujiko.
Si ajabu hata hotuba ya waziri wa madini sinclair anayo na anajua kinachoendela
 
naomba kusahihisha ni ripoti ya jaji bomani na wal siyo jaji makani

Kama alivyosema Mama,think BIG,NA Steve D..Wachukuliwe hatua kwanza waliompa...Kwasababu hakuikwapuwa wala kuiiba!
ALIPEWA!
 
Who are the shareholders of Tanzania Explorers apart the two who are friends?
 
Binti yake Sinclair na mamia ya washirika wao wenye hisa kwenye Barrick Gold pia...
 
Huyu Heyo anazeeka vibaya sana.Yaani huyu Sinclair ainunue hii report(maana na uhakika hajaipata bure bila kitu kidogo!) halafu wamuajibishe?Unachekesha wewe babu.Wakumuwajibisha ni huyo baba lao ambaye haishi jipya kila leo.Ni kero tupu kazi kujichekesha kwa wazungu na kuitikia 'yes sir'

Sinclair hawezi kuachiwa, lazima achukuliwe measures kama yule mgiriki aliyepigwa persona non grata na Nyerere mpaka akaenda ku enlist msaada wa Archbishop Makarios.

Tatizo ni kuwa anayetakiwa kumuwajibisha ni rafiki yake aliyempa ripoti ambayo by virtue of the circumstances na yeye anatakiwa kuwajibishwa, lakini nani atamfunga paka kengele?
 
Lakini ripoti si ya Rais... si anao uhuru wa kumpa yeyote amtakaye... hiyo ripoti haikuagizwa na Bunge hata sielewi kwanini wabunge wanakuja juu. Kama walikuwa wanataka si wangeunda kamati yao teule walipoombwa?
 
Lakini ripoti si ya Rais... si anao uhuru wa kumpa yeyote amtakaye... hiyo ripoti haikuagizwa na Bunge hata sielewi kwanini wabunge wanakuja juu. Kama walikuwa wanataka si wangeunda kamati yao teule walipoombwa?

Mwanakijiji,

Rais ana operate katika a political environment.Hata kama rais yuko juu ya sheria, haina maana kuwa rais anaweza kwenda Mnazi Mmoja akawapiga watu risasi kisha akatoweka, watamu impeach na kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye.

Hii move nayo, in our own subtle way, ni expression ya kutokuwa na imani na rais.
 
Kwanza awajibishe aliyemwezesha kabaila sinclair kupata hiyo ripoti na kufanya kazi iliyofanywa na kamati teule ya madini kuwa ya kujungujiko.
Si ajabu hata hotuba ya waziri wa madini sinclair anayo na anajua kinachoendela

Ndiyo maana siku hizi hata hotuba zake za mwisho wa mwezi hazipo tena, maana dalili za yeye kuwa fisadi zinazidi kuongezeka. Utaamua vipi kumpa ripoti muhimu ya kamati ya madini mzungu ambaye si mwananchi wa Tanzania kabla ya Watanzania wenye mali zao ambao mashinikizo yao dhidi ya mikataba ya madini ambayo haina manufaa yoyote kwa Watanzania na badala yake inawanufaisha wageni ndiyo yaliyosababisha kuundwa kwa kamati hiyo? Sirikali hii haitufai kabisa!!!
 
Nafikir tatizo letu hapa sio Sinclair, tatizo let ni Kikwete, kama umepewa report na unajua inawahusu share holders wako, ujaapishwa for secrecy au kitu kingine nafikiri hata mie ningewapa shareholders wangu information. Kikwete ndio mwenye matatizo hapa, badala ya kuweka mbele interest za nchi na wananchi waliompa kura yeye kaweka interest zake mwenyewe na rafiki zake. sio ajabu ukakuta kuwa huyu bwana Sinclair alipoiona hii report alimuuliza Jk sasa vipi mbona iko hivi, akajibiwa kuwa final decision maker ni yeye Jk ndio maana Sinclair akaweza kuwahakikishia wenzake. Tatizo letu sisi ni JK!!!!!!!!!!!
 
Lakini ripoti si ya Rais... si anao uhuru wa kumpa yeyote amtakaye... hiyo ripoti haikuagizwa na Bunge hata sielewi kwanini wabunge wanakuja juu. Kama walikuwa wanataka si wangeunda kamati yao teule walipoombwa?

Ingawa ripoti ni ya raisi, nafikiri wabunge wanayo haki ya kuiweka kitimoto serikali na kama kuna miiko either ya kiutendaji au kisheria iliyokiukwa, wahusika wanaweza hojiwa na kamati mbalimbali za bunge.
 
Ni nani atakayejibu hoja ya Cheyo?? Waziri Mkuu, Mwanasheria mkuu au baadhi ya wajumbe walioko kwenye kamati ya Jaji Bomani?? Umefika wakati kwa Serikali kutoa tamko rasmi juu ya jinsi ripoti yake ilivyomfikia Bw. Sinclair kabla ya wahusika wengine muhimu nchini na hatua gani zimechukuliwa kuziba mapengo na kuwawajibisha wahusika. Ningefurahi kumsikia Waziri mkuu anasemaje kuhusiana na hili??
 
Ni nani atakayejibu hoja ya Cheyo?? Waziri Mkuu, Mwanasheria mkuu au baadhi ya wajumbe walioko kwenye kamati ya Jaji Bomani??
Tutegemee majibu ya mkato kama yale ya meremeta

Umefika wakati kwa Serikali kutoa tamko rasmi juu ya jinsi ripoti yake ilivyomfikia Bw. Sinclair kabla ya wahusika wengine muhimu nchini na hatua gani zimechukuliwa kuziba mapengo na kuwawajibisha wahusika. Ningefurahi kumsikia Waziri mkuu anasemaje kuhusiana na hili??

Wakati huu serikali imeamua kabisa na imeonyesha kuwa haijali wabunge na wananchi.

Angalia majibu ya EPA,TICTS...yote ni ya kibabe kabisa....Mimi nilisema NEC ilpokaa Dodoma,waliamua wazibe masikio ya malalamiko na kuanza kuwasafisha Rais mtarajiwa.....

Tusingojee Muungwana kuwajibika au hata kukaripia hawa mafisadi marafiki zake...yeye sasa amekuwa foreign minister a.k.a president
 
john cheyo, yule mbunge wa bariadi yuko bungeni anazungumza sasa hivi, anashangaa ripoti ya tume ya madini ya jaji makani kuwa kwenye web site ya mtu anayejiita rafiki wa kikwete. anataka achukuliwe hatua kama yule mauritius aliyefukuzwa na nyerere baada ya kusema ameiweka serikali mfukoni.....

Tulishamweleza ile siku alipohojiwa na MKJJ na sisi kuruhusiwa kuuliza maswali!
Tuliipinga vikali kauli yake ya madai kuwa Sinclair ashitakiwe kwasababu hata Cheyo mwenyewe ni BEPARI TU!
Anaweza kuwa ni yeye kampa!
Kwani kama si yeye..Basi asingemlaumu Sinclair bali Mh Rais mwenyewe!
 
Jamani hiyo ripoti siyo ya raisi bali ni ya taasisi.
Ikulu ni taasisi ya umma na si mali ya binafsi ya rais.
Rais ni kiongozi tu kwenye hiyo taasisi.
Kama ametoa siri za taasisi inabidi awajibishwe.
 
Jamani hiyo ripoti siyo ya raisi bali ni ya taasisi.
Ikulu ni taasisi ya umma na si mali ya binafsi ya rais.
Rais ni kiongozi tu kwenye hiyo taasisi.
Kama ametoa siri za taasisi inabidi awajibishwe.

Tutamuwajibishaje? sheria yetu si inasea raisi asiguswe? huenda kumpa hii ripoti alikuwa anatimiza majukumu yake kama raisi wa Jamhuri ya TZ lol!

sheria zetu nazo zina walakini!
 
Tatizo ni huyu Mr Kisura jamani
Hivi mimi sielewi yeye anawafanyia nini Watanzania zaidi ya kujipendekeza kwa wazungu tu
alafu na mijibunge yetu inakaa kumsifia tuuuuu, wakati hakuna lolote analofanya la maana, itakuwaje report ambayo bunge haina mpaka leo hii, huyo sinclair tayari anayo, na hata hawaulizi na wala Kikwete aanaona sawa tuu

Hii nchi bwana inatia hasira sana tena sana ndugu zangu, maana kila kitu kimegoma, njia sahii ya nguvu ya hoja naona haina nguvu tena kwa sababu nguvu ya mafisadi na pesa a wizi ndivyo vilivyoshika nafasi katika nchi yetu
sasa sijui solution tutaitafuta vipi hapa

Solution ni kura yako mwaka 2010. Ukipenda mpe tena huyo kisura wako ili uendelee kulaumu tena kama kawaida yetu watanganyika.

Tujipe pole wenyewe kwani inawezekana hatujui tulifanyalo hapa duniani!
 
Haya Wana jf nimeonelea niuanzishe huu mjadala hapa kwani mambo yaenda yakiongezeka!

Na kwakuwa Mh Zitto alitakiwa kuwe Bungeni leo lakini kwa bahati mbaya hakuweza kufanya hivyo kwani aliuguwa na kulazwa Muhimbili.

Ila taarifa ni nzuri kuwa sasa anaendelea vizuri na tunamshukuru Mungu kwa hilo.

Wote tunajuwa wazi kuwa mambo sasa yamekwiva mara baada ya G8 Summitt. Na tunajuwa kuwa sasa Msimamo wa USA ni kuwa mafisadi washughulikiwe na tupewe uhuru wetu wa kunegotiate mikataba ya maana na yenye kumnufaisha Mtanzania.

Tunajuwa pia kuwa mvutano ni mkubwa sana kati ya Canada kwa kupitia Sinclair ambao sasa wanaimiliki nchi yetu kwa Ridhaa za viongozi wetu wakuu ambao kwa kudhihirisha hilo walimpenyezea RIPOTI YA MADINI KABLA YA WANANCHI.

Ripoti ya Madini ilikuwa na umuhimu mkubwa sana.Na pia licha ya kwamba tulijuwa haikuwa vyema kwa Zitto kushiriki kwasababu ya Iddi Simba kuwemo kamatini..Lakini ni wazi kuwa uwepo wake pale kamatini ni MUHIMU SANA KAMA ATAZINGATIA UKWELI.

Kwani ni wazi kuwa yawezekana madhumuni halisi ya ripoti hii kutoka kwa Rais hayakuwa na maana ya kufanya mabadiliko yoyote.

Je...JK KUMTEMA SINCLAIR?

JE..WAMAREKANI WATATUPA DILI NZURI!?

Kwa mtizamo wangu binafsi..Mimi nafikiri tumuondoe Sinclair...Ukweli uwekwe wazi...Mapendekezo ya wazalendo yapewe kipaumbele.

Na sheria zibadilishwe ili kukidhi maslahi ya Taifa na Wananchi wake.

Tik tak tik tak....
 
Zitto
user_offline.gif

Zitto has no status.
JF Senior Expert Member
Join Date: Fri Mar 2007
Posts: 325
Rep Power: 22
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif

Thanks: 42
Thanked 643 Times in 150 Posts
Credits: 28,429


icon1.gif
Re: GEORGE KAHAMA na ANDY YOUNG wamegombana?
........sasa hivi TZ kuna mnyukano mkubwa sana kwa ahadi za huyu kikwete kwa weupe hao alipokuja waziri mkuu wa canada haikuwa ziara nyepesi kama vyombo vyetu vilivyoripoti bali ni kubomolewa kwa ngome ya makampuni ya marekani na canada kuna kitu kimewagonganisha haya majitu, na hata hii inayoitwa kamati ya madini inatafutwa ili kumfunga paka kengele ili asilaumiwe kikwete bali mapendekezo ya kamati kikwete anayahitaji kujifichia ili afanye kinyume na yale aliyowaahidi waliomfadhili......

You cant be more right!!!!!!
 
Back
Top Bottom